top of page

OMBA UKIAMINI.


Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi;

“Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.” Waebrania 11:6

Nataka ukamatie neno hili“mtu akimwendea Mungu lazima aamini…” Kuomba ni moja ya njia ya kumwendea Mungu. Na katika njia hii unaambiwa ni lazima uamini. Neno “lazima” limeandikwa hapo kwa maana kubwa kabisa kwamba sio hiayari ikiwa kama unamwendea Mungu kikamilifu bali lazima uamini uwepo wake. Unajua maombi yasiyoambatana na imani ni kelele tu,bali yale ambayo mtu akiomba huku akiamini ni maombi yenye tija sana. Kila aombaye hana budi aombe akiamini kwamba atapokea majibu lakini ikiwa kama ataomba sawa sawa na mapenzi ya Mungu (1 Yoh.5:14)

Shida iliyopo leo kwenye maombi ni “imani” tu.Maana wengi wanaomba lakini si wengi wanaamini katika kuomba kwao. Unaweza kuona mtu akiomba lakini kwa kweli hana imani timilifu kwa kile kile anachokiomba. sasa utapokeaje ikiwa huna imani.  ” Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. ” Marko 11:23

Yaani ikiwa utaomba kwa jina la Yesu,wewe utakuwa umemaliza kazi yako,na hapo mwachie Bwana atende huku ukiamini kwamba Bwana amekwisha tenda. Yesu aligundua kwamba wanafunzi wake walipungukiwa imani katika kuomba kwao,alipowatazama akawambia hayo maneno. Lakini ndicho kinachoendelea hata sasa kwa watu waombao kwa jina la Yesu. Ukiona shaka wakati wa maombi yako,uwe na uhakika hutajibiwa la!kama umejibiwa basi ni kwa neema na kwa makusudi fulani kwa maana sio utaratibu wa kimaombi. Wapo wakristo wenye kuomba bila shaka na wapo waombao huku wakiwa na shaka mioyoni mwao. Lakini wewe usiwe kama wale wenye shaka mioyoni mwaka,bali omba ukiamini tu,nayo yatosha kabisa!

huitaji kujenga ukuta wa mashaka kabisa! kwa maana si wewe utendaye bali ni Yesu. Kwa hiyo omaba bila shaka wala wasi wasi na amini kutoka moyoni mwako kwamba hicho ulichoomba umekwisha kipokea hata kama hakionekani kwa macho yako ya kawaida,wewe amini tu umepokea. Kuamini si kazi kubwa,lakini shetani amepofusha akili na fahamu za wengi katika eneo la “ kuamini” ili kusudi tusipokee.

Naikumbuka simulizi hii; Kulikuwa na wanamaombi sehemu fulani huko kijijini. Kanisa lilakutana kwa ajili ya kuomba mvua  inyeshe kwa maana kulikuwa na ukame sana hapo kijijini.Walipomaliza,kiongozi wa maombi akawatangazia kwamba “kesho muda kama huu kutakuwa na mvua kubwa kijijini,hivyo sote tuje tumshukuru Mungu…” Kesho yake,walikusanyika ili wamshukuru Mungu;hapo ndipo walimwona kijana mdogo amevalia mavazi ya kujilinda na mvua huku amebeba mwamvuli hali bado mvua wala haikuwepo. Mtu mmoja akamwuuliza “kulikoni kijana?mbona umebeba mwamvuli kwenye jua kali kama hili na umevalia mavazi ya kujilinda na mvua”

kijana akawaambia pamoja na mtu huyo aliyemwuuliza “…mmesahau kwamba jana tuliombea mvua,na mtu wa Mungu alisema mvua itanyesha kubwa leo muda si mrefu kutoka sasa?” wakashangaa! maana kweli waliomba lakini hawakuwa na imani thabiti. Punde si punde mvua ikanyesha…Kijana alikuwa na imani katika maombi,lakini watu wazima waliomba nje ya imani na wakasahau kabisa. Na ndivyo wengi tuombavyo hivyo. Kuwa kama kijana huyu mwenye imani katika kuomba kwake!

Ikiwa kama umebarikiwa nifahamishe, pia Kwa maombi na msaada zaidi , piga +255 683 877 900

What’sapp namba+255 746 446 446 .

Mch. G. Madumla.

UBARIKIWE.

תגובות


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page