NYUMBA YA MFINYANZI
- Mch. Gasper Madumla
- Jun 10, 2022
- 4 min read
Updated: Aug 30, 2022

Nyumba ya mfinyanzi / At the Potter’s house
Ndani ya nyumba ya mfinyanzi kuna vyombo vingi vilivyofinyangwa kama apendavyo mfinyanzi. Kila chombo katika nyumba yake kimefinyangwa kwa ajili ya kazi maalumu,na Kwa sababu hiyo vinatofautiana kimaumbile,aina ya udongo,na hata kimtazamo kutegemea “kusudi” la Kila chombo. Kuna vyombo vingine vimetolewa tayari na kuanza kutumiwa na vingine bado vinasubiri vitolewe,na vingine bado vinasubiri a mchakato wa kufinyangwa ukamilike ili vifae kwa matumizi.
Mungu alimpomchagua Yeremia kama nabii wa mataifa,alimtaka aanze kuelewa mapema kazi “kusudi” aliloitiwa ili kusudi awe yeye kama yeye yaani asije akajaribu kuishi au kuwa kama nabii mwingine kwa maana hawafanani katika kazi / kusudi. Hivyo Bwana akaanza kusema naye angali mtoto mambo makubwa Kwa Habari ya maisha yake mwenyewe. Na alioona anaanza kuelewa,akampeleka katika nyumba ya mfinyanzi kwa lengo la kumfundisha zaidi.
Na hivi,ndivyo afanyavyo kazi Bwana Mungu wetu. Yeye husema nasi mara moja japo mtu hajali,naam mara ya pili katika ndoto. Lakini anaposema nawe,kama hujaelewa uwe na uhakika atakurudia tena ili kusudi “ moyo wako aupate vizuri ” na hapo aweza kukupeleka field/ kwenye karakana upate kuelewa zaidi kusudi lake. Biblia inaema kwa habari ya Yeremia;
Yeremia 18:3-4 (KJV)
“ Basi nikashuka mpaka nyumba ya mfinyanzi, na tazama, alikuwa akifanya kazi yake kwa magurudumu.
Na chombo kile, alichokuwa akikifinyanga, kilipoharibika mkononi mwake yule mfinyanzi, alikifanyiza tena kuwa chombo kingine, kama alivyoona vema yule mfinyanzi kukifanya.”
Kwa mujibu wa andiko hilo,tunaweza kujifunza mambo machache hapo;
01. Kila chombo kimefinyangwa, / hakijajifinyanga chenyewe
Hakuna chombo ambacho kimejiwezesha kujifinyanga kitakavyo isipokuwa mfinyanzi alikifanya atakavyo yeye. Biblia inaema Yeremia alimwona mfinyanzi akifanya kazi yake yeye kama yeye kwa vile aonavyo vyema. Ushauri wa kila chombo kiweje ulitokana na mfinyanzi alikusudia nini katika chombo alichokifanya yeye.
Hapo jifunze kuwa, Bwana Mungu Yeye Kwa mapenzi yake amefanya Kila kitu,na Kila mtu Kwa mapenzi yake vile aonavyo,Yeye haitaji usaidizi katika kufinyanga kile akipendacho,tena wala kilichofingwa hakiwezi kumpangia au kumlazimisha. Mfano bilauli haiwezi ikalalamika na kumwambia mfinyanzi mbona umenifanya nimekuwa bilauli badala ya sahani?
Haiwezekani.!!!!
Sasa ikiwa vyombo vya udongo vinaitii sheria hiyo,kwa nini wewe ufike wakati wa kulalamika vile Bwana alivyokufanya? Maana kuna watu ambao wanajaribu kumkosoa Mungu kwamba Kwa Nini wameumbwa walivyoumbwa!!! Tumeshuhudia wengine wakijibadilisha na kutaka kufanana na watu wangine!!! Kumbuka wewe ni wewe tu!!! Huwezi kuwa mwingine,kubali ulivyofinyangwa na Bwana. Jikubali ulivyo,na kamwe usije kutamani uwe kama fulani. Hivyo ulivyo ndivyo ulivyofinyangwa na Bwana!
02. Kuna maumivu ya kufinyangwa.
Neno linasema mfinyanzi alipoona chombo kimeharibika mkoni mwa mfinyanzi,alikifinyanga tena kuwa chombo kingine. Sasa haikuwa rahisi kubadili kufinyanga tena bila kuacha maumivu ,au usumbufu kwa chombo kilichoridiwa tena. Kawaida ya kufinyangwa ni kuleta maumivu kwa chombo ingawa chombo kinaweza kikawa hakipendi kufinyangwa tena lakini kama kitaachwa kufinyangwa tena ujue hakitafaa kwa kusudi la mfinyanzi kwenye hicho chombo.
Kawaida ya mfinyanzi haangalii namna ya kelele au kilio cha chombo kinaporudiwa,anachoangalia ni “kusudi” na ndio maana mfinyanzi aweza kukirudia chombo kile kile hata Kwa mara kumi,au hata Kwa siku nzima akakesha kwa kukifinyanga – finyanga mpaka pale atakapoona kinafaa.
Wewe ni chombo cha Bwana naye Bwana ndiye mfinyanzi,ni lazima ukubali kufinyangwa na Bwana hata kama kuna maumivu utakayoyapata ili kusudi ufae zaidi ya hapo ulipo. Mfano; Bwana anapokuangalia anagundua kwamba chombo chake kimeharibika kutegemea kusudi alilokuitia basi uwe na uhakika utafingwa tena.
Maumivu hayakwepeki kama utarudiwa na Bwana. !!! Ebu fikiria wewe ni chombo kama chungu cha kuhifadhia maji,na hilo ndilo kusudi kubwa la wewe kuumbwa, lakini kwa bahati mbaya umejikuta badala ya kuhifadhi maji unajikita unatumika kupika. Yaani upo nje ya kusudi uliloitiwa Kwa kufanya hiyo,uwe na uhakika mfinyanzi hawezi kukubali aweza kukurudisha katika kazi Yako,japo Kwa maumivu makali na kulia kwingi Kwa maana hapo ndipo uliloitiwa / ulipofinyangwa.
03. Kufanywa chombo kipya
Ikiwa chombo kimeharibika mkononi mwa mfinyanzi,basi ni dhahiri mfinyanzi atakigeuza na kukifanya chombo kingine kipya. Mfano fikiria mfinyanzi amekifanya chombo cha kikombe na gafla mkono wa kikombe ukakatika,basi aweza kukigeuza na kukifanya upya kuwa chungu cha kupikia.
Hii inatufundisha kwamba Bwana aweza kukufinyanga upya na kuwa chombo kingine Kwa matumizi mengine Lakini Jambo muhimu hapo ni kwamba kama “chombo kiliharibika” . Katika hali ya kawaida, Bwana aweza kukufinyanga upya ili ufae katika makusudi yake. Ni matamanio ya chombo kutamani kutumiwa upya, lakini Bwana ndiye mfinyanzi mwenye maamuzi ya mwisho kumbuka hilo.
Tabia ya nyumba ya mfinyanzi
1. Vyombo vya udongo na vyombo vya dhahabu.
Mfinyanzi yoyote anajua vyombo alivyokufanya tena anajua hata thamani ya vyombo vyake. Kama kukitokea uharibifu wa nyumba yake,basi ni dhahiri atavikimbilia vile vyombo vya thamani bila kujali ni cha namna gani ili kusudi asije akapata hasara kubwa.
Biblia inatuambia ndani ya nyumba ya Bwana kuna vyombo vya dhahabu,fedha pia kuna vyombo vya mti na tena kuna vyombo vya udongo. Tena inaendelea kusema ya kwamba vingine vina heshima na vingine havina! ( 2 Timotheo 2:20)
Lakini ukumbuke vyote hivi ni vyombo vya mfinyanzi mmoja aliyevifinyanga vyote. Swali la kujiuliza,Kwa nini vina utofauti mkubwa huo? Tena kwa nini vingine vina heshima na vingine havina?
Bila shaka, heshima ya chombo ni kutegemea namna ya vile kinavyotumika bila kujali aina ya chombo chenyewe,maana inawezekana kikawa ni chombo cha udongo lakini kikawa na heshima kubwa kuliko chombo cha dhahabu. Kama chombo cha udongo kinatumika zaidi ya chombo cha dhahabu,ni lazima kibebe heshima kwa mfinyanzi.
Kumbe !
Pamoja na aina tofauti tofauti ya vyombo, kikubwa ni “kiwango cha kutumika” Hata Leo ikiwa mtu anayefanana na chombo cha udongo katika nyumba ya Bwana Leo/kanisani lakini akawa ni mtu mwenye bidii ya kujituma na kutumika bila kujali hali au hadhi yake ya maisha,mwonekano wake.
Mi nataka nikwambie mtu huyo ataheshimiwa zaidi ya vyombo vingine vya dhahabu vyenye kukaa tu! Kumbe heshima ya chombo pia hutegemea na kazi ya chombo chenyewe! Jitambue Sasa kwamba u chombo cha Bwana, heshima yako ipo ndani yako kutegemea na kiwango chako unachotumika.
Ikiwa umebarikiwa nifahamishe kwa + 255 683 877 900
What’s app number ni + 255 746 446 446
Na Mch. G. Madumla
UBARIKIWE
Comments