NJE NI NDOA,LAKINI HAKUNA NDOA!!! 😭😭😭
- Mch. Gasper Madumla
- Apr 18, 2018
- 5 min read

Hasira haifai ndugu yangu mwanandoa!!!!
Bwana Yesu…
Kwa ufupi..
Kila kukicha vilio vya wanandoa vinaongezeka,hata kufikia wakati wasioingia kwenye agano la ndoa wanaogopa sasa kuingia. Mojawapo ya kesi kubwa iliyoshika chati siku za leo ni kesi za ndoa,maana utakuta wengine wameachana,wengine hakuna unyumba (haki ya msingi ya mwanandoa),wengine hawana maelewano,wengine kila kukicha ni mahakamani kudai hati ya kuachana,n.k. unaweza ukajiuliza kulikoni? Mbona hali inakuwa mbaya kwenye ndoa za leo,kisa nini haswa?au tatizo ni lipi? Wengine wanasema wanawake ndio tatizo,mara wengine husema wanaume ndio tatizo!!!
Kuna ndoa iliyovunjika muda mrefu tu,lakini ukiiona utafikiri ndoa ipo safi. Kwa nje wanandoa wa namna hii ujikaza kuigiza kana kwamba wapo pamoja wakipendana sana lakini kusema ukweli hawapo pamoja na hakuna ndoa hapo,tena cha ajabu walio wengi ni watu wa makanisani! Unaweza ukasema kivipi mambo haya,? Ebu fikiria ukiwa wewe ni mwanandoa lakini hakuna kujaliwa,hakuna unyumba,hakuna maelewano ndani ya nyumba na mwenzi wako,hakuna cha ukaribu wowote na mwenzi wako,hakuna kusikilizana,hakuna heshima,mambo yako ni mambo yako na mambo yake ni mambo yake,hakuna usawa,n.k Je hapo kuna ndoa?
“Ukiiona kama ndoa iliyo hai lakini kusema ukweli imevunjika” ni ndoa ya yenye kubeba taswira ya uhai kwa nje lakini ndani hakuna ndoa. Ni sawa na kaburi lililopakwa chokaa nzuri ya kupendeza lakini ndani kuna mifupa na funza. Lakini hayo ndio maisha ya walio wengi kwenye makanisa tuliyonayo siku hizi. Bwana anataka leo asema na uhai wa ndoa yako,ikiwa ni moja ya ndoa iliyokufa Bwana aifanye kurejea katika uhai,ikiwa kama hakuna maelewano na mwenzako basi Bwana akufanyie kuelewana na ikiwa kama hakuna haki yako ya msingi (unyumba) Bwana arejeshe hayo yote katika Jina la Yesu Kristo Mungu aliye hai.
Nataka ujue kwamba shetani anafanya kazi kubwa sana kuvuluga ndoa kwa sababu akifanikiwa kuipiga ndoa yako basi ujue amefanikiwa kupiga na huduma yako,amefanikiwa kupiga na maendeleo ya watoto wako,amefanikiwa kupiga pia na kazi ya mikono yako. Kwa sababu ikiwa mtakosa kuelewana na mwenzako basi ni dhahiri hata huduma ya Bwana haitasonga mbele vyema,upako hakuna kwenye mafarakano tena watoto wanapowatazama mkigombana ujue mnawaumiza hata wakati mwingine wakijikuta wakilia pasipo kujua na kurudi nyuma kimasomo,kazini huwezi kuwa na amani ikiwa uliondoka nyumbani kwako kwa malumbano. Je hayo si kweli?
Uhai wa ndoa ni Mungu awe pamoja nanyi,akiwapa kuelewana.
Chanzo cha ndoa kuwa hai ni Mungu kuhusika kikamilifu,kwa sababu Yeye ndiye asili ya vyote naye huleta tunda la Roho ; (furaha,amani,upendo,uvumilivu,uaminifu,kiasi,utu wema,upole na kiasi Wagalatia 5:22). Lakini pale uonapo ndoa yako imekosa mambo hayo basi ujue mahusiano yenu na Mungu hayako sawa. Na ibilisi amepata nafasi ya kupanda mabaya ili kuivunja ndoa yako. Lakini inawezekana wewe ukawa unajitahidi sana kukaza kwa Bwana kuliko mwenzako, au inawezekana wote mkawa mnajitahidi kwa Bwana,ila bado unaona mambo ya ndoa yako hayakai sawa,basi ujue bado kuna eneo labda halijashughulikiwa vizuri na kwa kuwa Mungu ni mwema na mwaminifu uwe na uhakika utakujuza eneo hilo ili ulishughulikie’.
Magomvi,kelele na mafarakano ni pando la ibilisi.
Mungu si dhalimu hata apande magomvi bali ni ibilisi ndie aliyepanda hayo yote. Ebu angalia kwa ukaribu kwenye ndoa yako,alafu jiulize;anzia kujiuliza kwa hili,kwa nini mwenzako au wewe unachoka / hujisikii kumpa mwenzako tendo la ndoa? Mbona mwanzo haikuwa hivyo? Kwa nini? Biblia imesema vizuri tu katika hili kwamba “ msinyimane,isipokuwa mmepatana kwa muda….” 1 Wakorintho 7:5 ukichunguza kwa makini utagundua sio hali ya kawaida hii!!! Na hapo pakikosekana tendo la ndoa kwa kadri ya matakwa ya mwenzako,basi ujue ndoa hatatulia ingawa ndoa sio tendo la ndoa tu ndoa ni upendo,lakini kipengele hiki ni moja ya vipengele muhimu kinachoweza kuleta maelewano au mafarakano kutegemea na mnafanyaje.
Siku moja wanandoa walikuwa wakigombana kila mara,na walipokuja kwa mtu wa Mungu ( mchungaji),Mchungaji aligundua tatizo lipo wapi na kabla hajatatua mizozo yao aliwaambia “ebu nendeni kwanza mkapeane tendo la ndoa kisha ndipo mje tuanze kuzungumza kesi zenu” cha ajabu,waliporudi walikuwa wapole,kimya wakiwa na sura changamfu yaani utafikiri walikuwa hakuwahi kugombana kisha mchungaji akawaambia“ sasa tuzungumze” gafla mwanaume akasema“hahahaha…hahaha.. mchungaji bhana.. sawa,mchungaji naona ugomvi umeisha kwa kweli” 😂😂😂😂umeona hapo! Kumbe hawa walikuwa kisa chao ni“ kunyimana tendo” mimi sijui sababu hii kwako kwamba ni moja ya sababu wewe wajua. Lakini ni jambo muhimu sana kuliko maelezo!
Najua kuna wakati mwingine mambo ya ndoa yanachanganya sana,kwa maana kweli kabisa unaweza ukajitoa na kujitahidi kumridhisha mwenzako lakini wapi!! Wala asione, lakini mimi nataka nikuambie leo kwamba ikiwa unajitahidi kufanya hivi na vile kwa lengo la kumridhisha mwenzako na ikiwa hajali,kuna kitu kidogo tu utakuwa unakosea au unakifanya kiulegevu nacho ni “ maombi” nitakueleza kivipi,wala usiwe na wasi wasi! Kwa sababu anapoomba ni kama vile kumkabidhi Mungu mambo yako,na ujue hakuna jambo gumu la kumshinda BWANA.
Ndoa iliyovunjika / yenye mafarakano kwa sababu ya kukosa mtoto
Wapo wanandoa wanaochekeana wakiwa nje ya watu au kanisani lakini wakiwa wenyewe ni ugomvi wa “ kununiana” kwa sababu wamekosa mtoto. Na cha ajabu mwanaume ndio wa kwanza kumlaumu mkewe akisema kwa nini huzai? Jamani! Kwani nani kakuambia matatizo ya uzazi ni ya mwanamke,kha!! Matatizo ya uzazi hayana cha mwanamke wala mwanaume!!!! Sasa kwa nini umfikirie vibaya mwenzako,Je unafikiri yeye hapendi kupata mtoto? Ifike wakati sasa wa kuona kwamba sio mkeo wala sio mumeo ndiye mwenye matatizo!! Kumbuka suala la kupata mtoto linatoka kwa Bwana kama zawadi tu. Ukilitazama jambo hili katika mtazamo huu,basi kamwe huwezi kumuwazia vibaya mwenzako wala huwezi kumshutumu,!!!
Ingawa ninajua wapo wanawake ambao hawashiki mimba kwa sababu waliuchezea usichana wao kipindi kile walipokuwa “wamechetuka na duniani,nayo duniani ikawachetua” na kujikuta sasa kila wakijaribu wapi!!!hakuna cha mimba wala dalili ya mimba! Lakini leo pia ninazo habari njema kwa watu kama hawa kwamba Mungu anaweza kurejesha kizazi chako,haijalishi hapo mwanzo ulikuwa vipi wewe elewa kwamba upo mkono wa BWANA aokoaye ( Zab.68:20). Mwamini Mungu na tufanye maombi pamoja leo kwa kunipigia simu,namba zangu zipo chini.
Ikiwa taasisi ya ndoa ni ya Bwana mwenyewe basi huna budi kumkimbilia Yeye ili ndoa yako irejee. Na kumbuka hili ikiwa kama hutarejea kwa Bwana, kamwe ndoa yako haitaweza kusimama vizuri hata kama utakuwa na pesa kiasi gani kwa sababu ndoa sio pesa! Bwana MUNGU ukiruhusu aingingie kwenye ndoa yako, ujue ataingia tu (Ufunuo 3:20). Jitahidi katika hili ili kwamba ndoa iwe hai na nzuri. Ikiwa kama ulikuwa hujaokoka fanya maamuzi leo ya kuokoka,pia mkabidhi mwenzi wako kwa Bwana. Yafaa kujenga madhabahu hapo nyumbani kwako,yaani pasikauke ibada kila siku!
Ndoa yako ni lazima iwe hai ndani na nje.
Huu ndio wakati muafaka wa kuisimamisha ndoa yako kuwa hai kama alivyokusudia Bwana. Kama kilio umelia sana na kilio hakikusaidia kurejesha ndoa yako,bali Mungu ndiye atakayerejesha ndoa. Inawezekana ukawa kama huamini fulani hivi,au kama unajiuliza kivipi-ninauhakika ya kwamba ukianza upya na Bwana leo itakuwa ni sababu ya kurejesha ndoa yako katika uhai. Vile mlivyokuwa mkigombana sasa yatosha na anza kuchukua hatua chache kama zifuatavyo kurejesha uhai katika ndoa yako;
Omba msamaha kwa mwenzako. – umeyajua makosa yako leo,tafuta kutengeneza na mwenzako,shuka na ukubali makosa yako huku ukiomba msamaha wa dhati.
Omba toba mbele za Mungu pia.
Hakikisha unapata sapoti ya maombi na ushauri zaidi kutoka kwa mchungaji,waweza kunipigia
Sasa;Tengeneza ulipokosea kwa kujitahidi kumpa mwenzako yale ayatakayo – Ikiwa huna ukaribu wa ndani anza leo kutafuta ukaribu,jitahidi katika hilo.
Waweza kumtoa out – jaribu kutengeneza mtoko wa nje wewe na mwenzako,ili mtafute faragha na muongee.n.kKwa maombezi,Na ikiwa kama umejifunza kitu basi usiache kunipigia simu leo nipate kujua.nipigie sasa kwa namba hizi;+255 683 877 900Namba ya What’sapp ni .+255 746 446 446
Mch. Gasper Madumla
UBARIKIWE.
Commentaires