top of page

NI VIGUMU KWAKO KUUPIGA MATEKE MCHOKOO ( Matendo 26:14)

Mfano wa mchokoo (Goads)


Bwana Yesu asifiwe…

Imeandikwa “Tukaanguka nchi sote, nikasikia sauti ikisema nami kwa lugha ya kiebrania, Sauli! Sauli! Mbona waniudhi? Ni vigumu kwako kuupiga mateke mchokoo” Mdo 26:14

Paulo mtume anaeleza jinsi Bwana alivyomtokea pale Paulo alipokuwa akiitwa Sauli mtu aliyekuwa akiwatesa na kuwaudhi wafuasi wa Yesu (Mdo 8:3) ( Maana hapo mwanzo wafuasi wa Yesu waliitwa watu wa Njia hii,kwa sababu Yesu ndio Njia,Kweli na Uzima soma Yoh.14:6). Kabla Sauli hajafika Dameski akiwa njiani gafula Yesu anamtokea na kumwambia maneno hayo kwamba Sauli,Sauli Mbona waniudhi… Na anamwambia “ Ni vigumu kwako kuupiga mateke mchokoo

Sasa ni muhimu kujiuliza kwamba Bwana Yesu alikuwa ana maana gani kumwambia Sauli maneno hayo. Au nini haswa maana ya mchokoo?

Neno hili “ mchokoo” huitwa “goad ” ni aina ya kifaa kilicho na makali ya kukata kama upanga/jembe kali la kulimia. Au ni kifaa chenye ncha kali kama mkuki fulani hivi lakini unaotengenezwa na chuma. Hivyo mchokoo ulikuwa ukitumika kukata kama alivyokitumia Shamagri mwana wa Anathi aliyewapiga Wafilisti watu mia sita kwa konzo la ng’ombe ( mchokoo) kisha akawaokoa Israeli ( Waamuzi 3:31). Soma pia 1 Samweli 13:21.

Na kwa sababu “mchokoo” ni kifaa chenye makali tena kilikuwa wakati mwingine ni kifaa chenye nja kali zaidi ya upanga wa kawaida,kwa sababu hiyo huwezi kukipiga teke maana ni wewe ndie utakaye humia na wala mchokoo hautaumia. Ni kama vile upige mateke ukuta,ni nani atakaye umia? Wewe au ukuta?

Yesu anamwambia Sauli ni vigumu kwako kupiga mateke mchokoo,kwa maana utaumia wewe mwenyewe. Yesu anamueleza Sauli ya kwamba Kweli ya Neno la Mungu ni kama mchokoo ambao hawezi kuupiga mateke,kwa maana ataumia mwenyewe na kamwe hawezi kuzuia Kweli ya Mungu. Maneno haya aliambiwa Sauli kabala ya kuwa Mtume Paulo,nasi leo tunapoyasoma tunajifunza sisi katika maisha tuliyonayo sasa.

Hivyo basi hakuna awezaye kupiga mateke mchokoo,maana ataumia mwenyewe. ukimuona mtu yeyote anayejitahidi kuipinga Kweli ya Mungu kwa uongo,ni sawa kabisa na kuupiga mateke mchokoo,kwa maana Neno haliwezi kupigwa kwa namna yoyote ile. Neno ni Kweli ya Mungu na ya kaa milele.Lakini jiangalie pia na wewe unavyoenenda,Kisha jiulize Je unaikataa Kweli ya Mungu? Je unakataa kile kilichoandikwa katika biblia ? Je unakataa wokovu? Mambo hayo ni Kweli,ambayo ukiikataa na kuiizuia kwa jitiahada zako ujue unaupiga mateke mchokoo!

Na mtu awaye yote akimpinga Mungu aliyeziumba mbingu na nchi kwa Neno lake,basi ujue mtu huyo anatafuta kufa,anatafuta kuumia yeye mwenyewe. Hivi unajua ukikataa Kweli ya Neno katika eneo lolote lile,kule kupinga na kukataa kwako hakubadilishi nafasi ya Mungu? Mungu ataendelea kuitwa Mungu

Wapo watu hata leo wanapiga mchokoo kwa kuzuilia injili isihubiliwe,watu hao kwa kweli wanajisumbua maana wataumia wenyewe na injili itazidi kuhubiriwa. Yaani kwa kadri injili inavyopingwa na ndivyo inavyozidi kuenea.

Na Mch. Gasper Madumla

+255 683 877 900

What’s app number ni+255 746 446 446

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page