NI KWA NAMNA GANI MUNGU HUJIFUNUA KWETU.?
- Mch. Gasper Madumla
- Nov 20, 2015
- 2 min read

Na Mchungaji Gasper Madumla.
Bwa Yesu asifiwe…
Je wajua njia ambazo BWANA MUNGU hujifunua kwa watu wake?Yamkini waweza usiwe unazijua zoote,au labda yawezekana ukawa huzijui kabisa. Tumeshawahi kusikia na kusikia mara kwa mara watu wakisema “…nimemuona BWANA…” Lakini mara nyingi hatujui ya kwamba mtu huyo amemuonaje Bwana. Ukweli ni kwamba MUNGU hujifunua hata sasa kwa watu wake kwa njia mbali mbali kama apendavyo;
01.KWA NJIA YA MIUJIZA.
Mungu Yeye ni mtenda miujiza ya kweli,ndiye aliye mkuu peke yake (Zab.86:10). Miujiza ya Mungu ipo kwa sababu ya kumtukuza Yeye peke yake na si mwingine (Hesabu:1422). Na ikumbukwe ya kwamba Yeye ndiye atendaye miujiza yote ya kweli. Miujiza ipo kwa sababu zifuatazo;
(a) Kudhihilisha nguvu iliyopo ndani yake.
(b) Kuwafanya watu waziamini nguvu zake ( Yoh.2:23 )
(c) Miiujiza ya Mungu ipo ili pia iweke tofauti kati ya miujiza yake na miujiza ya shetani.
Biblia imejawa na miujiza ya Mungu,kuanzia agano la kale hadi agano jipya. Labda tuiangalie baadhi tu ya miujiza ya Bwana katika biblia;
~ Kuzaliwa kwa Isaka katika tumbo la Sara (Mwanzo 21:1-3),kuzaliwa kwa Yakobo na nduguye Esau katika tumbo la Rebeka(Mwanzo 25:21-26) na kuzaliwa kwa Yusufu katika tumbo la Raheli (Mwanzo 30:22-24). Hii ilikuwa ni miujiza ya Bwana maana hawa wote walizaliwa katika matumbo ya mama zao yaliyokuwa yamefungwa.
~Kichaka kilichowaka moto ( Kutoka 3:1-4)
~Miujiza mbele ya farao na mapigo ya Misri (Kutoka 4-13)
~Kuvuka bahari ya shamu (Kutoka 14)
~Kuvuka mto Yordani (Yoshua 3)
~Kuvunjika na kudondoka ngome ya Yeriko ( Yoshua 6 )
~Miujiza kwa mtu wa Mungu Eliya (1 Wafalme 17-18,2Fal 1)
~Isaya ( 2 Wafalme 20),Elisha (2 Wafalme 2;13),Tazama miujiza ya Yesu.
02.KWA NJIA YA HUKUMU.
Hii ni njia ambayo Mungu hujidhihilisha kuadabisha watu katika haki. Tazama Mungu alivyojidhihilisha katika hukumu hapa; ( Farao Kutoka 4-12),(Nebukadreza Dan 4:28-37),( Belshaza Dani 5),(Anania na Safira Matendo 5:1-11),( Kwa Herode Matendo 12:22-23),( Watumishi wote wa uovu Ufunuo 20:10,14-15)
03.KWA NJIA YA NDOTO NA MAONO.
~Ndoto na maono mengine huleta mafunuo ya Mungu na mipango yake aliyoipanga. Vitabu vifuatavyo vina ndoto na maono mengi yanayomfunua MUNGU.; Vitabu kama;Ezekieli,Danieli,Zekaria,Amosi,Nahumu,Matendo na,Ufunuo.
(A)Kwa njia ya ndoto,MUNGU huzungumza.
Mara nyingi tunasoma BWANA MUNGU akijifunua kwa watu wake kwa njia ya ndoto,katika kufikisha ujumbe uliokusudiwa. Soma habari za ;
~ Abimeleki Mwanzo 20:3-7
~Yakobo Mwanzo 28:12;31:10
~Labani. Mwanzo 31:24
~Yusufu Mwanzo 37:5-9
~Suleimani 1Wafalme 3:5-15
~Nabukadreza Danieli 2:1,31;4:5,8
~Danieli Danieli 7:1-28,
~Yusufu Mathayo 1:20-21,2:13,19-20
~Mamajusi Mathayo 2:11-12
~Mke wa Pilato Mathayo 27:19
(B)Kwa njia ya maono,MUNGU pia husema;
~Ibrahimu Mwanzo 15:1
~Yakobo Mwanzo 46:2
~Isaya, Isaya 6:1-8
~Ezekieli, Ezekieli 1:8
~Anania na Safira Matendo 9:10-11
~Yohana kitabu cha Ufunuo
03. KATIKA NENO LAKE.
~Neno la Mungu katika biblia linamdhihilisha Mungu alivyo,sababu neno la Mungu ni Mungu mwenyewe akizungumza na wote wenye mwili.
▪Hizo ni baadhi ya njia ambazo Mungu hujifunua kwetu. Lakini kumbuka pia,njia za Mungu hazichunguziki kwa maana anaweza kujifunua kwa namna yoyote ile isiyojuzu mwanadamu kuijua ( Njia ambayo mwanadamu hawezi kuzijua kabisa )
~Kwa huduma ya maombi,tafadhali piga sasa kwa namba yangu hii;+255 683 877 900
What’s app number +255 746 446 446
Na Mchungaji Gasper Madumla.
UBARIKIWE.
Comments