top of page

NI AIBU!!! REUBENI KULALA NA SULIA WA BABA’KE.

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi.

Neno “ sulia” lina maana ya “awala,” kiswahili cha mtaani tunasema “nyumba ndogo” kiingeleza wanasema “concubine ” . Hivyo sulia ni mke mdogo asiye halali kwenye ndoa. Ilikuwa ni jambo la kawaida hapo zamani hizo kwa Wayahudi kuwa na masulia. Kumbuka ya kwamba,masulia walikuwa pia ni watumwa fulani,hivyo walichukuliwa na kujikuta wakiingiliwa na wanaume wa kiyahudi.

Angalia mfano wa Hajiri. Hajiri alikuwa ni mgeni ( Mmisri),alikuwa ni sulia lake Ibrahimu. Na huyu mwanamke ndiye sulia la kwanza kutajwa kwenye biblia. Ibrahimu aliingia kwake naye akapata mtoto wa kiume “ Ishimaeli ” . Haukuwa utaratibu sahihi wa kiungu,bali Bwana aliwaacha na kujifanya kama azioni zam hizo za ujinga ( Matendo 17:30)

Na sasa tunamshangaa Reubeni kulala la sulia la baba yake,Yakobo. Biblia inasema“Ikawa Israeli alipokuwa akikaa katika nchi ile, Reubeni akaenda akalala na Bilha, suria wa babaye; Israeli akasikia habari...” Mwanzo 35:22.

Unajua ninajaribu kumtazama Reubeni kama lango kwenye familia ya Yakobo. Kwa maana alikuwa ni mzaliwa wa kwanza, mtoto wa kwanza kuzaliwa akiwa na wadogo zake 11 ( ukimwondoa Dina). Ninapomwangalia Reubeni kama lango nategemea kuona msimamo wa kuiongoza familia vyema,lakini bahati mbaya Reubeni akajisahau.

Tunaposema “Reubeni kutembea na sulia la baba yake ” ni sawa na kusema “Reubeni katembea na mama ake mdogo,au katembea na mama yake” si jambo lililozoeleka,wala si jambo lingetegemewa kutokea. Hili lilikuwa ni jambo la kushangaza na kuleta “laana ” kwa Reubeni. Reubeni aliufunua utupu wa mama yake mdogo,ni mbaya!!! Lakini kwa nini hata kitendo kama hiki kutukia kwa Reubeni mtoto wa Yakobo? Bila shaka Reubeni alidiliki kufanya uhuni huu kwa sababu,kulikuwa hakuna hofu ya Mungu ndani yake,Reubeni hakuwa mtu wa haki,hivyo hakimsumbua kulala na mke wa baba yake. Lakini hii ni too much bhana!!! Dah!

Unajua ukikosa hofu ya Mungu, unaweza kufanya madudu yasiyotegemewa kufanyika kwako. Wewe mwenyewe ni shahidi tu,jiangalie pale ulipokuwa huna hofu na Mungu, kisha angalia yale uliyokuwa ukiyafanya… Ni hatariiii.!!! Lakini pia,bila shaka kulikuwa na ukaribu sana kati ya Bilha Sulia na Reubeni hata wakajikuta wakiangukia zinaa.

Ebu fikiria pia hili,kisha jichukue wewe mwenyewe jiweke karibu sana kimazoea na mtu fulani awe mdada au mkaka ambaye ni ndugu wa damu kabisa. Kisha mkawa mnakaa nyumba moja,na chukulia mmezoeana sana kiasi kwamba unamfurahia na kuzungumza naye mara kwa mara muda ambao mnabakiaga wawili tu kwenye jumba kubwa namna hiyo.

Unafikiri mwisho wake ni nini? Bila shaka mnaweza mkaangukia uzinzi,kwa sababu hapaswi kuwa na ukaribu uliopitiliza na mtu mwenye jinsia tofauti. Hiki ndicho tunachokiona kwa Reubeni kulala na Bilha sulia la Yakobo. Ingawa biblia haituambii ukaribu au mazoea yaliyopo kati ya Reubeni na Bilha, lakini inawezekana watu hawa walikuwa na ukaribu sana.

Lakini kwa nini habari hii,imendikwa kwenye biblia?

Imeandikwa si kwa kusudi la wewe ukafanye kama alivyofanya Reubeni, hapana. Bali ni kwa kusudi kukufundisha usije ukajisahau na kufanya yale aliyofanya Reubeni. Uzuri Biblia takatifu imetufunulia mabaya na mema waliyoyafanya watu kwa lengo kujifunza ili kwamba sisi wa kizazi cha “doti kom” tusije tukaangamia.

Je hivi ni kweli unaweza kulala na mlezi wako?

Inawezekana kabisa wewe kutembea na ndugu,mlezi,au hata mzazi wako. Kwani tumesikia mangapi mpaka sasa kwa habari ya mambo haya? Ni mengi tumesikia watu wakifanya mapenzi na ndugu,walezi wao wa karibu. Sababu shetani pia yupo katika eneo hili. Lakini ujue endapo utakuwa mbali na wokovu unaweza ukatembea au kulala na mtu ambaye hata watu wakiambiwa watashangaa. Dawa ya mapenzi ya namna hii ni Yesu tu,na kutulia hapo kwenye wokovu ili hofu ya Mungu ijengeke kikamilifu,na hapo kamwe huwezi kufanya uchafu wa namna hii.

Matokeo yake ni nini? Reubeni alipata nini alipotembea na sulia la baba yake?

• laani ilikuwa juu yake.( Mwanzo 49:3)

Laana haikumwacha Reubeni,kwa kosa la kukinajisi kitanda cha baba yake Yakobo. Reubeni aliishi maisha ya laana badala ya baraka kwa maana katika haki Reubeni ndiye aliyekusudiwa kutawala,kuongoza kama lango la wengine wote. Sasa,tazama mbaraka wake wote ulihama na kwenda kwa nyumba ya Efraimu ( Yusufu na ndiye baba wa Efraimu). Kumbe! Ukiwa mzaliwa wa kwanza na ukikolofisha,baraka zako zinaweza kwenda na kuhamia kwa mtoto mwingine atakayejijenga na hofu ya Mungu.

Ikiwa fundisho hili limekubariki,basi ningependa kusikia kutoka kwako kwa kuniandikia msg au kunipigia kwa namba zangu zilizopo hapo juu. Pia kwa msaada zaidi pamoja na maombezi,waweza kunipigia sasa.

Kwa mawasiliano pamoja na maombi piga kwa +255 683 877 900

Na mch. Gasper Madumla.

What’s app ni +255 746 446 446

UBARIKIWE.

Comentarios


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page