NGUVU YA SADAKA ~09 (Tamati)
- Mch. Gasper Madumla
- Dec 19, 2017
- 2 min read

Bwana Yesu asifiwe. …
Kwa ufupi.
(ix) Sadaka kwa wahitaji – ( Luka 19:8,Warumi 15:25-27)
Wahitaji ni watu ambao wamepungukiwa au kukosa kabisa mahitaji muhimu kama vile chakula,mavazi na malazi,au wale waliokuwa hawawezi (wagonjwa) wanaohitaji msaada wa kutibiwa. Kundi lote la watu namna hiyo,huitwa ni “wahitaji” ambao hawanabudi kusaidiwa.Biblia inataja kwamba maskini wapo siku zote na hawatakoma (Kumb.15:11,Mathayo 26:11)
Hii ina maana watu hao wanahitaji msaada kutoka kwako,sio tu msaada wa kuwaombea bali msaada wa kifedha na mali ili uwawezeshe zaidi kuishi. Kuna kusudi la kuwa na maskini,kwa maana Mungu angeliweza kutufanya sote tuwe matajiri na wala pasiwepo na wahitaji,lakini ile namna ya kuwa na wahitaji inaonesha ni jambo la kimungu ili wewe na mimi tukawasaidie kwa “sadaka zetu”
`` Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.” Mathayo 25:39-40
Maneno hayo ni Yesu mwenyewe anasema hivyo,na anakuambia wewe na mimi. Kama ukisoma habari nzima kuanzia mstari wa 34 utagundua kwamba Yesu akihubiri juu ya namna ya kuwasaidia wale wasiojiweza,na vile uwasaidiavyo basi ni sawa na kumuhudumia Yesu vivyo hivyo. Kumbe,kuwa mkristo pasipo kuwa mtoaji wa sadaka kwa wahitaji bado hujawahi mkristo sawa sawa! Thamani yako ya wokovu ipo katika utoaji.Kumbuka kile kilichoandikwa kwenye Yakobo 1:27,kwamba imani iliyo sawa mbele za Mungu ni ile ya kuwasaidia wajane na yatima katika dhiki zao.
Je nitaanzaje kuwasaidia wasiojiweza? / Nifanyeje basi?
01. Omba toba. Kwa sababu haukufanya vizuri hapo mwanzo. Sio dhambi,lakini ni makosa ya kutowasaidia watu wengine hali unao uwezo huo.
02. Kwa mujibu wa neno la Mungu katika Wakolosai 3:17, neno linakutaka kwa kila jambo au tendo uanze na Bwana. Hivyo,ni vyema kabla ya kufikiria ni wapi upeleke misaada yako,basi mshirikishe Mungu katika maombi. Muulize Roho mtakatifu akuelekeze wapi na ni nini cha kusaidia. Kwa kuwa Roho mtakatifu ni Mungu mwaminifu sana,basi uwe na uhakika atakupa maelekezo na ili ujue hayo,utapata amani ndani yako ni nini cha kufanya.
03. Inenee sadaka yako katika Jina la Bwana.
Ni muhimu sana kuiombea sadaka yako kwa sababu hiyo sadaka itakapopokelewa isipokelewe kama pesa au mali ya kawaida bali yeye apokeaye apokee kama uponyaji katika dhiki yake. Wakati mwingine unapomsaidia mtu kwa mali,ile mali iguse moyo wake hata aje kwa Yesu, aokoke.
04.Jenga utaratibu wa kuwasaidia wahitaji kidogo kidogo kwa kile ulichonacho. -Huitaji kuwa na pesa au mali nyingi bali unahitaji “moyo” tu wa kutoa. Ni nini ulichonacho sasa?Je hakiwezi kumsaidia mtu mmoja aliyeshindwa kununua dawa ya tshs 1,000/=ili awe sawa? Bila shaka unaweza kuwasaidia watu wanahitaji msaada wa ukweli ukweli.
Kwa wale wahitaji waliopo pembezoni mwa barabarani huasaidie pia,lakini lazima uwe makini kwamba kila sadaka yako unayotoa ni lazima uinenee/uiombee ili kusudi kama kuna roho nyingine ya chuma ulete kutoka kwa mwombaji huyo,basi ishindwe na ikutane na Roho wa Mungu. Lakini usipite bila kumsaidia ikiwa ndani yako inajisikia amani ya kumsaidia.
Kwa msaada zaidi,+255 683 877 900
What’s app ni +255 746 446 446
Mch .G.Madumla.
UBARIKIWE.
Comments