NGUVU YA SADAKA ~ 08
- Mch. Gasper Madumla
- Dec 13, 2017
- 2 min read

Bwana Yesu asifiwe….
Kwa ufupi…
( viii) Sadaka ya injili.
Ni sadaka ya kuitegemeza kazi nzima ya injili isonge mbele. Kwenye kila kanisa,lazima kazi ya injili (uinjilisti) iwepo. Na kazi hii inahitaji support/msaada wako wa maombi lakini na matoleo yako yatakayo wawezesha wainjilisti kutoka hata kufika maeneo ya mbali kuwashuhudia watu habari njema za wokovu.
“ Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!” Warumi 10:14-15 soma pia Isaya 52:7
Paulo anauliza swali la msingi sana katika sadaka ya injili. Kwamba wakiwepo watu wanaohitaji kutengeneza na Mungu. Sasa watawezaje kumjua Mungu wasipoongozwa? tena watamsikiaje Mungu,kama mhubiri hatakuwepo. Bila shaka watu hawawezi kujiongoza kama hayupo wa kuwaongoza. SasaPaulo analenga watu kuwaweshesha wahubiri wafike sehemu za mbali ili wakaifanye kazi ya Mungu.
Sadaka ya injili inafanya kazi kubwa ya kusapoti injili ndani na nje ya kanisa. Kwa maana injili ni lazima ihubiriwe ulimwenguni mwote. Hivyo kazi ya injili ya watu wote,na kila mmoja anapaswa ahiubiri injili kwa kile alichopewa. Kwa wale waliopewa neema ya kuwa wainjilisti kama karama waliyopewa waifanye kazi hiyo kwa nguvu zote. Lakini wengine ambao hawakupewa karama hiyo,basi waihubiri njili kwa mali na pesa zao kama sehemu ya sadaka yao ya injili.
Kwa sababu hiyo, basi sadaka ya injili ni ya lazima! Unapaswa kutoa sadaka hii mahali popote injili ya kweli inapohubiriwa pasipo kuangalia hao wanaohubiri wapo upande wako kidhebu,wala pasipo kuangalia ni wa jinsia gani,au wa kabila gani,au ni wazungu au waafrika n.k Bali so longer injili inahubiriwa unapaswa kutoa sadaka kuzidi kuisapoti injili hiyo,ili kusudi iwafikie wengi zaidi.
Leo kuhubiri injili kumekuwa na gharama kubwa,maana ukitumia vyombo vya habari kuna gharama,ukihitisha mkutano pia kuna gharama. Hivyo,utagundua kwamba suala la gharama haliepukiki. Lakini; Iwe iwevyo!injili ni lazima ihubiriwe.Ebu jiulize; Je ni mara ngapi unachangia pesa au mali yako kwa ajili ya injili? Je wewe ni mmoja unayefurahia umuonapo mtu anahubiri injili kwenye bus,stand,au sokoni? Unamsapoti vipi mtu wa namna hiyo? Au wewe ni mmoja kati ya watu wenye kuwabeza wainjilisti? Ikiwa utajijengea utaratibu mzuri wa kutoa sadaka za injili mara kwa mara utabarikiwa na wala hutakaa uombe baraka kwa Mungu,bali baraka za kufunguliwa kwa milango yako zitakujilia nakukupata. Sadaka ya injili ikitolewa vizuri,basi ujue injili itakuwa na kasi zaidi ya hapa.
ITAENDELEA….
Kwa msaada zaidi,na maombezi nipigie kwa simu+255 683 877 900
What’s app ni .+255 746 446 446
Mch.G.Madumla.
UBARIKIWE.
Comments