NGUVU YA SADAKA ~06
- Mch. Gasper Madumla
- Nov 28, 2017
- 1 min read

Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi…
(vi) Sadaka ya shukrani.
Ni sadaka unayoitoa kwa Bwana kwa sababu amekutendea mengi makubwa na ya ajabu,tena mengi ambayo hata hukuwahi kuomba,lakini kwa wema wake Bwana amekutendea.Huitaji kuangalia yote,bali anza kuangalia afya yako na kumrudishia Mungu utukufu kwa maana ni wangapi siku ya leo wanatamani wangelikuwa kama wewe kiafya lakini hawakuweza,wengine wamekufa wengine wamelazwa nakadhalika. Wewe u nani basi? Au wewe u mtakatifu sana kuliko wengine?
Lengo kuu la sadaka ili ni kumrudishia Bwana sifa na utukufu katika yote aliyokutendea Bwana Mungu na yote anayozidi kukutendea na familia yako kwa ujumla. Ukitafakari utagundua kwamba hata hapo ulipofika ni Bwana tu. Hivyo mpe Mungu utukufu kwa mali zako,kwa fedha zako pia. “ Atoaye dhabihu za kushukuru,Ndiye anayenitukuza.Naye autengenezaye mwenendo wake,Nitamwonyesha wokovu wa Mungu.” Zaburi 50:23
Tunajifunza kwa wale wakoma 10 ( Luka17:11-19). Wote waliponywa lakini ni mmoja tu ndiye aliyerudi kushukuru,tisa wote wakaondoka zao.Mfano huu wa wakoma 10,unatuonesha kwamba watu wengi hawana utaratibu wa kushukuru isipokuwa ni wachache tu wanaoweza kurudi na kumshukuru Mungu. Wewe unapaswa kuwa miongoni mwa wachache wrudio kwa Bwana kwa shukrani. Ni jambo la kuanza sasa na kuliweka kwenye maisha yako,hata ukawa na moyo wa shukrani.
Ni vyema ukamtolea Bwana kwenye madhabahu ya kanisani mwako kwa lengo la kuwafundisha wengine waanze kumshukuru Mungu. Lakini hakuna sheria ya kutoa,popote pale waweza kumshukuru Bwana Mungu wako.
ITAENDELEA….
Kwa msaada zaidi,na maombezi nipigie kwa simu+255 683 877 900
Namba ya what’s app ni +255 746 446 446
Mch.G.Madumla.
UBARIKIWE.
Comments