top of page

NGUVU YA SADAKA ~04


Kwa ufupi

iv)Zaka/fungu la kumi.

Kwa mara ya kwanza Biblia inataja zaka kutolewa na Ibrahimu katika vitu vyote alivyokuwa navyo,Naye Ibrahimu anatoa zaka zake kwa Melkizedeki kuhani wa Mungu Aliye juu sana ( Mwanzo 14:20). Huu ulikuwa mwanzo wa zaka kutolewa,hata hivyo zaka iliendelea kutolewa.

Katika agano la kale;

  1. Zaka iliamriwa (Walawi 27:30-33)

  2. Fungu la kumi kwa kila kitu alichonacho mtu/alichokipata (Mwanzo 14:20,28:22)

  3. Zaka ilitumika kuwategemeza Walawi (Hesabu 18:21)

Kwa mujibu wa sheria,ili kupata sehemu ya kumi ya pato lako ilikubidi uchukue pato lako kama vile tuseme ni tshs 500,000/= uzidishe 10% utapata 50,000/=. Hii ilikuwa ndio sheria ya kupata sehemu ya kumi ya pato lako.

Agano jipya;

  1. Hufanywa bila sheria,namna roho atakavyo (Mathayo 23:23)

  2. Ji sadaka ya siri,bila majigambo wala kujiinua (Luka 18:13)

 Hali imebadilika sasa,kwa maana hatutumii tena sheria kupata fungu la kumi,isipokuwa sheria umuhimu wake ni kutupa mwaka. Kwa mfano,ikiwa unapokea Tshs 500,000/= na unahitaji kutoa fungu la kumi/zaka,kwa mujibu wa sheria Tshs 50,000/= ndio zaka yako,lakini katika agano jipya Tshs 50,000/= ni kama kianzio tu,huwezi kufungwa kwa sheria,bali Roho wa Bwana anataka umtolee kiasi gani? labda 60,000/=,au 80,000/= kama sehemu ya kumi. Hivyo hatupo tena kwenye sheria,bali tunaongozwa kwa Roho wa Bwana.

“Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.” Malaki 3:10

Maana ya zaka iliyokamili ni zaka ile itolewayo kwa mujibu wa maongozi ya Roho wa Bwana. Kile kinachogusa moyo kikitolewa kwa usahihi,itakuwa ni sadaka yako iliyokamili. Kamili ya 500,000/= sio 50,000/= bali kile roho anachokuongoza,Tshs 50,000/= inakupa mwanga wa kutoa tu. Biblia inasema Bwana atafungua baraka zake kwa yeyote mwenye kumtolea Bwana zaka iliyokamili,kwa maana “Baraka zinafuata mkondo wake wa kanuni.” Katika kila pato unalolipata,ipo sehemu ya zaka yako kwa Bwana. Na ni vyema ukamtolea Bwana mapema kwa kile unachokipata,usilimbikize zaka!

Je unaweza kulipa zaka mahali popote?

Au je badala ya kulipa zaka kanisani,unaweza kupeleka msaada kwa wahitaji kama sehemu yako ya zaka? Hayo ni miongoni mwa maswali muhimu yanayoulizwa na wengi. Lakini ukweli ni kwamba sadaka ya zaka ni aina ya sadaka iliyoelekezwa kutolewa kwenye madhabahu unapoabudu. Ikiwa kama unajisikia kutoa sehemu nyingine au kusaidia waweza kufanya hivyo,lakini kwanza uongee na mchungaji wako.

ITAENDELEA….

Kwa misaada zaidi nipigie simu zangu hizi;+255 683 877 900

Mch. Gasper Madumla

What’s app ni +255 746 446 446

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page