top of page

NGUVU YA SADAKA.~02

Na Mch.G.Madumla.


Kwa ufupi;

ii) Sadaka ya kawaida.

Hii ni aina ya sadaka tunayoitoa mara kwa mara tuwapo kanisani. Badala ya wanyama leo tunatoa pesa au mali zetu kwa Bwana kama nafasi ya kumtumikia Bwani. Lakini kumbuka sadaka zinapaswa zitolewa kupitia msingi mmoja wa “pendo” kwamba yeyote anayemtolea Bwana hana budi atoe kwa moyo wa kupenda (2 Wakorintho 9:7a). Na ndio maana mtu akitoa kwa kupenda kamwe hawezi kusukumwa sukumwa katika utoaji.  Ukipenda utatoa kilichonona,kama Habili alivyotoa vilivyonona kwa sababu moyo wake ulipenda.

Lakini ni vyema kufahamu kwamba,Mungu hana shida ya pesa,au mali zetu. Hii ikiwa na maana hata kama hatutamtolea Bwana,bado Yeye atabaki kuwa Mungu. Hatuwezi kumbadilisha kwa chochote.Hivyo faida ya utoaji ipo kwa mtoaji si kwa mpokeaji. Ni sisi tunaotafuta uhusiano na Mungu,naye kwa pendo kuu ametupa nafasi ya kujiungamanisha naye katika matoleo.Katika utoaji wa sadaka,Yeye Mungu huangalia moyo wako. Je unatoa kwa kupenda?Je unatoa kwa kushukuru?Au unatoa kwa sababu ya mabaki yaliyozidi,au kwa sababu mchungaji akuone!!!!  Luka 21:1-4

Yafaa kila mwamini ajue anawajibu wa kumtolea Bwana sadaka nzuri. Na kumbuka kwamba chochote kizuri kina gharama,kina maumivu pia. Mfano;ukitaka kutoa kilichonona itakulazimu kulipa gharama juu ya kile ukitoacho. Na hapo ndipo moyo wako utaambatana na unachotoa.

Sadaka katika agano la kale.

Roho mtakatifu alikuwepo kabla ya agano la kale,kwa kuwaYeye ni wa milele. Lakini alikuwa hajadhihilishwa,hivyo Mungu aliwapa Israeli taifa lake la mfano sheria mbali mbali za taratibu za ibada na utoaji. Hali akijiua mioyo ya watu wake kwamba ni mioyo migumu,hivyo akaona aweke japo kiongozi / sheria ili watu wajue nini wanapaswa kufanya na nini hawapaswi kufanya. Katika agano la kale; Sadaka zilitolewa kama ilivyoamriwa katika sheria. Kwa mujibu wa sheria/torati iliwataka makuhani kupokea sadaka za watu na kuziwasilisha kwa Mungu,lakini hata hivyo kulikuwa na watu waliokosa,walihitaji watoe sadaka. Mambo yafuatayo yaliandikwa katika utoaji wa sadaka kwenye agano la kale.

  1. Aina za sadaka ( – Wanyama tofauti Walawi 1:2-17,Na sadaka za unga Walawi 2:1-16)

  2. Sadaka ilitegemea muda (Sadaka za kila siku Kutoka 29:38 -42,Sadaka za majuma Hesabu 28:9-10,Sadaka za mwezi Hesabu 28:11-15,Sadaka za mwaka Hesabu 28:16-)

  3. Kusudi la sadaka (kama vile;utakaso Walawi 1:3-17,Kushukuru Walawi 2:1-6)

  4. Ni nani anayetoa ( Wachache hupokea kwa niaba)

Sadaka – agano jipya.

Sadaka ya kipekee ya agano jipya ni sadaka ya Mwana-kondoo,Kristo (Yoh.1:29).Kupitia sadaka hii,wakristo wote hutakiwa kujitoa kwake ili waweze kumpendeza Mungu. Sadaka muhimu katika agano jipya ni kujitoa kwa Yesu kikamilifu. Hata hivyo pesa na mali nzuri zinahitajika kuwategemeza watumishi wa Mungu (Wafilipi 4:18)

ITAENDELEA…

Ikiwa kama umebarikiwa,nifahamishe,na kwa msaada zaidi – piga sasa+ 255 683 877 900

Mch. G.Madumla

What’s app ni +255 746 446 446

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page