top of page

NGUVU YA SADAKA ~ 07


Bwana Yesu asifiwe…

 Kwa ufupi.

(vii) Dhabihu ya nabii.

Ni sadaka ya kumtegemeza mtumishi wa Mungu. Si wengi wanaowategemeza watumishi wa Mungu kwa fedha zao au mali walizonazo kwa sababu hawajui nini maana ya mtumishi wa Mungu. Watu wengi waliotoka kwenye dini zao,hawafahamu umuhimu wa kuwasaidia watumishi wa Mungu kwa maana walikuwa hawafanyi hivyo kule walikotoka. Ebu fikiri mtu aliyekuwa kwenye dini fulani ambapo watumishi wa Mungu wanasaidiwa na misaada kutoka nje au kutoka kwenye shirika fulani,sasa katika mazingira kama hayo; mtu anamwona mtumishi kavaa,kala,n.k akijua kwamba shirika linamsaidia. Mtu huyo akipata neema ya wokovu na kuja kwenye kanisa la kiroho hufikiria hali ile ile ya kwanza kwamba mchungaji atajua atavaa nini,atakula nini,atasomeshaje watoto wake! Ndani yake hakuna moyo wa kutoa kwa mchungaji wake kwa sababu ya mapokeo aliyoyapokea kwenye dini yake ya kwanza.

Katika huduma ya Yesu kulikuwa na wanawake waliomtegemeza kwa mali zao ( Luka 8:2-3). Kile walichokuwa wakitoa kwa Yesu kilikuwa ni sadaka ya nabii. Ulikuwa ni mfano tu,kutuelekeza nini cha kufanya kwa wachungaji wetu tulionao leo. Wachungaji na watumishi wa Mungu wengine wanahitaji sadaka ya namna hii ili mambo mengine yasonge mbele vizuri.Kwa maana kama waamini hawatawategemeza wachungaji wao,hatari moja itakayokuja ni kwamba mchungaji itambidi atafute namna mbadala ya kujitafutia pesa,na kuliacha agizo la Bwana aliloitiwa. Hapo ni hatari,kwa maana anaweza kutunga somo la kuwalazimisha watu watoe kinyume na utaratibu/maandiko. Au akawa nusu kanisani na nusu kazini,hata hakakosa muda wa kujiandaa na mambo ya ibada kwa maana hawezi kutumikia mabwana wawili!

Mambo madogo madogo kama hayo,si yakufundishwa kufanya bali uonapo penye uhitaji kwa nabii wako wewe fanya kama kwa Bwana pasipo kuangalia wengine. Ukiamua kutoa sadaka kwa nabii wako,unaweza hata sasa. Wala huhitaji kuwa na pesa nyingi ndipo ufanye. Unaweza kumtegemeza mchungaji wako kuanzia leo ukatoa sadaka zako za kinabii kwa siri nami nataka nikuambie,Hapo utamuona Bwana Mungu akifungua mambo yako mengi. Jaribu katika hili,kisha uone baraka za Bwana.

Ni vyema kuanzia leo ukajiwekea kautaratibu fulani hivi,kwa kutoa sadaka kwa Mungu kwa kuwabariki wachungaji wako. Kuangalia nini haswa anachokiihitaji ambacho kipo kwenye uwezo wako,na ukawa unapanda kwake kama sehemu ya sadaka yako ya kinabii. Hivi unajua ni rahisi sana kama utaamua kufanya hivyo. 

ITAENDELEA….

Kwa msaada zaidi,na maombezi nipigie kwa simu+255 655 111 149/683 877 900/762 414 446.

What’s app ni +255 655 111 149.

Mch.G.Madumla.

UBARIKIWE.

Comentarios


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page