top of page

NGUVU YA SADAKA ~ 03

Bwana Yesu asifiwe….

Kwa ufupi;

iii) Sadaka ya mbegu.

Hebu chunguza kwanza picha hiyo nzuri ya mizabibu. Utagundua aina tatu za rangi katika hiyo mizabibu (Nyekundu/damu ya mzee,nyeusi na rangi kama ya pinki). Picha hii inatupa kuelewa kwamba kuna mbegu tofauti tofauti za kupanda kulingana na msimu wa majira na nyakati. Kila mbegu hutegemea msimu ili ikue ipasavyo,na mpandaji anapaswa kujua majiara sahihi ya kupanda kutegemea na aina ya mbegu aliyonayo.

Mbegu ni nafaka inayopandwa kwa ajili ya kuzaa. Hivyo kusudi kubwa la nafaka inayopandwa ni kuleta mazao mema. Na kwa sababu ili mbegu ipandwe hata izae inahitaji hatua chache muhimu Sana. Hatua mojawapo iliyo muhimu Sana ni kuoza/kufa hiyo mbegu baada ya kufikiwa chini. Bwana Yesu anaelezea hili katika Yoh. 12:24;

“ Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.” Kumbe ili mbegu iweze kuzaa inahitaji ife kwanza. (Ingawa mfano huo Yesu aliutoa akiwa na maana nyingine,kwamba ikiwa tunahitaji kumzalia Mungu matunda mema/kuokoka vilivyo Basi ni lazima tuuzike utu wa kale na kuzaliwa upya)

Hivyo mbegu inapandwa na mkulima akitarajia kupata mazao hapo baadae. Na kila apandae vivyo hivyo utazamia faida ya kupata mazao yaliyo mema. Katika taratibu za upandaji,huwa mara nyingi upandaji unafanywa kwa misimu,hii ikiwa na maana upandaji haufanywi kiolela olela tu! Mkulima mzuri anajua majira yaliyo sahihi ya kupanda,na anajua apande nini kwa sawa sawa na msimu uliopo. Hivyo kuna mkulima apandaye mwanzoni mwa mwaka,mwingine katikati ya mwaka, mwingine mwisho wa mwaka. Lakini kwa kusudi la kupata mazao yaliyo mema sana,inamlazimu mkulima kupanda mbegu zake mwanzoni mwa mwaka.

Mbegu ni sadaka inayopandwa haswa mwanzoni mwa mwaka. Mbegu haitupwi Wala kutolewa kwa sababu ikitupwa haitakuwa na kuzaa (kumbuka kwamba haitaoza ikiwa Kama itatupwa) . Hivyo sadaka ya mbegu “ inapandwa katika udongo mzuri” kusudi ilete mazao mengi. Zipo taratibu nzuri za kupanda mbegu yako. Taratibu hizi zinalinganishwa na taratibu za kupanda mbegu ile ya kawaida.

Je ni taratibu zipi zilizo nzuri za upandaji mbegu yako?

  1. Kujua majira sahihi ya kupanda. (Kumwuuliza Roho mtakatifu)

  2. Kuandaa mbegu yako/zako zilizo nzuri kwa upandaji.(Kitu gani unaguswa kutoa?,hiyo sadaka yako ikoje?)

  3. Andaa shamba lako vizuri.(Ingia kwenye maombi kabla ya kutoa)

  4. Hakikisha unitilia Maji na samadi.(Neno likuelekeze vyema,na uombe tena)

  5. Hakikisha unazui wadudu wasije na kuaribu mzao wako/ Ilinde mbegu yako kwa kuzui wadudu waaribifu.(Ngoa kila pando la adui,pingamizi,na namna yoyote ya kuzuia ukuaji wa mbegu yako)

  6. Kuwa na matarajio ya kuvuna mazao mema. (Weka imani yako kwa Bwana) N.K

Mbegu inatoka wapi?

Mbegu inatoka katika kila Pato lako halali. Hivyo katika kila Pato lako halali kuna mambo matatu yanayopatikana,nayo ni ;

“ Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu;mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu.” 2 Wakorintho 9:10-11

  1. mbegu

  2. Chakula ( mkate)

  3. Akiba/ zidisho

Kumbe kila mmoja anayo mbegu. Kumbuka hilo usisahau kwamba katika kipato chako kuna mambo hayo matatu. Hivyo huna udhuru kusema kwamba huna mbegu hali una kipato fulani.

Mbegu inapandwa wapi? Kwa mtu yeyote ?

Ni vyema ukajua shamba la kupanda mbegu yako. Kumbuka kanuni ya upandaji ni kwamba huwezi kupanda sehemu yoyote,Bali kanuni inakuelekeza upande katika ardhi yenye rutuba. Mbegu inapandwa kwenye madhabahu maalumu ambapo unakula chakula chako cha kiroho,au kwenye madhabahu alipo kuhani afundishaye kwa usahihi na kwenye uwezo wa kuiatamia mbegu yako ili kusudi ilete mazao mengi hapo baadae.Watu wengi wamepanda mbegu kwenye shamba wasilolijua,hapakuwa na maandalizi mazuri ya upandaji kiroho. Hivyo hawakufanikiwa kuvuna yale waliyoyatarajia,kwa maana ni lazima uwe makini katika upandaji wa mbegu kama sadaka.

Kumbuka,utoaji wa sadaka hii ya mbegu sio namna ya kumhonga Mungu au kumtega Mungu ili afanye kitu fulani kwako. Kwa maana wapo watu ambao wanaelewa hivi,kwamba ili mambo yao basi ni lazima wapande pesa au mali fulani kwa Mungu halafu husubiria kulipwa na Mungu (kwa maana walitoa hapo mwanzo).Sadaka ya mbegu ni tendo la rohoni la kumtolea Mungu kilicho chema katika msimu fulani maalumu uliojipangia au uliopangwa na kanisa lako.

Angalizo;

Mungu alazimishwi kujibu maombi yako kwa kigezo cha kupanda. Kwa maana biblia haisemi kwamba utamlazimisha Mungu akupe mavuno/majibu kwa sababu umepanda kitu fulani. Bali sadaka ya mbegu ipandwe kwa imani tena kwa moyo wote.

ITAENDELEA…

Kwa msaada zaidi  + 255 683 877 900

Mch.G.Madumla

What’s app ni +255 746 446 446

UBARIKIWE.

Comentarios


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page