top of page

NENO NA ANDIKO TOFAUTI YAKE IPO WAPI?

Updated: Sep 30, 2022


Maneno haya mawili “neno” na “andiko” katika lugha ya kiyunani hujulikana kama rhema(neno) na andiko(logos). Ni vigumu kuyaelezea tofauti yake na pia ni vigumu kuyatofautisha kila moja ingawa yanatofautiana. Tofauti yake imejificha sana,lakini nataka niyajengee swali la namna hii;


Je kuna tofauti kati ya neno na andiko?


Tulikuwa katika moja ya bible study yetu pale kanisani kwetu BBFC(Beroya bible fellowship church)na wakati mtenda kazi mmoja akitafakari (kwa maana sisi ni waberoya) alielezea maneno haya mawili akionesha kwamba yanatofauti kila moja,ndiposa mtu mmoja akamuuliza kwamba “ Je maneno hayo mawili kati ya andiko na neno,kuna tofauti? Akiwa na maana kwamba biblia yote ni neno la Mungu nalo ni maandiko,sasa kuna tofauti gani hapo?..”


Ukweli ni kwamba ilituchukua wiki tatu za kutafakari ili kuona utofauti uliopo kati ya andiko na neno hatimaye tukapata majibu. Leo nataka nikupe majibu yangu katika tofauti iliyopo hapi. Sasa ni vyema tukajua nini haswa maana ya biblia kama msingi(key study) wetu. 

Biblia ni sauti ya Mungu iliyohifadhiwa katika maandishi. Sauti ya Mungu huwakilisha “neno” la Mungu. Pia tunaposema “…iliyohifadhiwa katika maandishi” tafsiri ya“ maandishi” huwakilisha “ maandiko/andiko”. Hiyo ni tafsiri sanifu ya biblia,yenye kuonesha tofauti fulani kati ya neno na andiko ingawa bado tofauti hiyo imejificha. Tujifunze zaidi;


Biblia nzima ni maandiko matakatifu ya Mungu yenye uweza wa ajabu. Maandiko haya yanaeleza habari sahihi za ukombozi kupitia Kristo Yesu. Hivyo ni maandiko matakatifu yanayoelezea ukombozi kupitia “neno” au kupitia Kristo Yesu. Yesu ndie neno naye ni njia,kweli na uzima(Yoh.14:6) Kivipi?


Imeandikwa;“Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu;…” Yoh.1:1,14a. Katika mistari hii,tunajifunza kwamba neno ni nafsi hai tena halisi ya Mungu. Maana huyo neno ( ambaye ni Mungu) akauvaa mwili,na akakaa kwetu/akazaliwa kama mwanadamu ambaye ndie Yesu. Biblia tena inamtaja kuwa alikuwa mwanadamu asilimia na Mungu asilimia. Moja kati ya mistari inayomtaja Yesu kuwa ni mwanadamu aliyekuja kutukomboa ingawa alikuwa Mungu sawa na Baba ni 1 Timotheo 2:5-6


Hivyo neno ndiye Yesu aliyekuja kutuokoa sisi sote. Sasa biblia inaandika habari zake,ni sawa na kusema biblia ina maandiko matakatifu kuhusu neno ambaye ndiye Kristo Yesu. Ni sawa na mtu aliyekwenda kununua dawa kwenye duka la dawa akiwa ameandikiwa jina la dawa kwenye kalatasi,kisha akafika hapo dukani na kumpa muuzaji kile kikalatasi muuzaji kisha muuzaji akasoma kile kikalatasi na kisha akampatia ile dawa aliyoandikwa kwenye hiyo kalatasi. 


Mfano huj ni mfano mzuri wa kuonesha kwamba ndani ya kalatasi kuna dawa iliyoandikwa lakini kuna dawa yenyewe sawa sawa na kile kilichoandikwa. Hii ikiwa na maana andiko ni neno la Mungu kabisa lakini ndani ya hilo neno la Mungu kuna sauti iliyo hai,sauti hiyo ni pumzi ya Mungu iletayo uzima na ndio neno ( rhema). Yesu anasema; “ Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.” Yoh.6:63  Neno la Mungu ni roho tena ni uzima.Paulo anatutazamisha katika mtazamo mpya kuhusu neno na andiko, 


Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.” 2 Wakorintho 3:6


Andiko linaelezwa kwamba linaua . Paulo hana maana maandiko matakatifu yanaua,bali andiko lisilobeba sauti ya Mungu linaua. Mfano mwepesi andiko linasema “Usimwache mwanamke mchawi kuishi.” ( Kutoka 22:18). Sasa andiko hili likibaki kuwa andaiko mtu anatekeleza mauaji kimwili kabisa kwa mwanamke/mwanaume mchawi. Ni mara ngapi tumeshuhudia mchawi akiuliwa kimwili kabisa kwa sababu mkristo mmoja aliyebeba andiko hili na kusema kwamba“hata biblia imetuagiza mchawi tuwauwe wafe wote” Je ni kweli neno linasema hivyo katika andiko hili?


Sasa hapo ndipo utaona kwamba Roho hutusaidia kuisikia sauti ya Mungu katika andiko. Hapo;hatuna maana maandiko matakatifu hayana nguvu hapana. Maandiko ni neno la Mungu lakini yakisomwa pasipo Roho hubakia maandiko bali Roho akiwepo ndipo katika andiko kuna suti ya Mungu. Mungu anazungumza hata sasa katika maandiko matakatifu,na ndio maana katika maandiko mengine mtu hupata kuisikia sauti ya Mungu katika maonyo,kufundisha,kuongoza au kuadabisha ( 2 Timotheo 3:16)


Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.” Matendo 17:11 


Mstari huu,umeandika mambo mawili neno(rhema) na maandiko( logos).  Waberoya walilipokea neno(rhema),alafu wakayachunguza maandiko(logos). Mtu mmoja akisema neno na maandiko ni sawa kwa mantiki ya kuwa ni kitu kimoja kilichotoka kwa Bwana lakini mtu huyo ni lazima afahamu kwamba sauti ya Mungu ni neno ambalo linaweza likawa limeandikwa lakini sauti hiyo inasema,ni hai hata sasa na inasema katika kile kilichoandikwa. Waberoya walipokea neno sauti ya Mungu kwa vinywa vya akina Paulo,na pia wakaenda kufanya utafiti katika maandiko yaliyoandikwa waone kama ni sawa.


Hivyo ndani ya andiko (logos) kuna sauti ya Mungu(rhema). Andiko likisomwa kama andiko ni sawa na kusoma vitabu vingine ambavyo ni vya kawaida. Na ndio maana andiko lenye sauti ya Mungu linaponya. Tunamuhitaji Roho atuongoze tunaposoma maandiko tusisome kama gazeti,bali tusome tukihitaji kusikia neno linasemaje katika andiko?


Kwa msaada zaidi pamoja na maombi tafadhali usisite kunipigia kwa simu +255 683 877 900.


What’s app number ni +255 746 446 446

Mch.Gasper Madumla.

UBARIKIWE.

Comentarios


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page