top of page

NAMNA YA KUIJENGA NDOA YAKO IWE IMARA ( BUILDING A GREAT MARRIAGE) ~ 04 👨‍❤️‍💋‍👨

Ndoa ni tamu bhana!


Shalom…

Kwa ufupi.

04. Jitahidi kuwa msafi ndugu.

Si kila kitu mpenzi wako wa ndoa anapenda, kuna vingine ni kero kwake, kama ishu ya uchafu ni kero sana. Mfano mkeo hapendi jasho lako la kikwapa,💨💪 na amekushauri sana utumie japo pafyumu lakini wewe wapi! Hata kuelekea hauonekani. Jamani kuna watu wana harufu mbaya ya kikwapa alafu wao wenyewe hawajisikii sijui! Utakuta ndio mume wako sasa yupo na kikwapa cha ukweli! Mmhh Jambo hili ni kero kwa mke maana hapendi halufu hiyo, alafu mbaya zaidi kama wewe ndio mume ukirudigi tu unataka umkumbatie mkeo na jasho lako, harufu kama ya beberu si beberu basi tu! hata kuoga hujaoga khaaa!!!! Mbaya hiyo, ujue Mungu anaona tu huo ukorofi wako wa kunuka kikwapa! Au chukulia mume naye hapendi mdomo wako💋👄 wewe mwanamke, kwamba mumeo muda mrefu amekulalamikia kwamba mdomo wako“ unatema sana ” naye amekushauri mke wake lakini wewe mwanamke, maneno yanaingia huku na kutokea kule sikio la pili, alafu mbaya zaidi unataka kumbusu , khaaa. Basi si ukapige mswaki kwanza, kwani shilingi ngapi bhana, nunua mswaki. N. K sasa hayo ni mambo tu tunayoishi nayo huku uswahilini kwetu. Hivyo ni lazima ujue ni nini mwenzako hapendi kutoka kwako, nawe usifanye hayo asiyoyapenda mpenzio. Jilazimishe kuondoa tabia au mambo asiyoyapenda mpenzi wako.

Jamani usafi nalo ni jambo la kufundishwa kweli? Kwani wewe mwenyewe hujui sasa ni mke wa mtu au wewe hujui kama ni mume wa mtu? Sasa kulikoni!!!? Mpaka mpenzi wako aanze kukuchukulia bango! Hivi unajua ni mbaya kama nini kumsema mtu mzima eti kwa sababu ya uchafu tu. Lakini ni vyema nieleze kweli hapa hapa ili tumalizane kabisa,kwa sababu nimeliona jambo hili, na hili ni moja ya jambo la kutengeneza ndoa yako kuwa imara. Unajua ukiwa mchafu chafu hali hiyo inamfanya mwenzako kujisikia aibu hata kukutambulisha kwa rafiki zake! Jambo la usafi ni jambo la kawaida kabisa.

Utakuta siku zile za mwanzo mpenzi wako aaha alikuwa akipendeza, yaani ananukia kapafyumu fulani hivi, nguo zake safi, yaani mpaka raha – ulikuwa huwezi kusita kumtambulisha kwa rafiki zako, au kuongozana naye. Lakini sasa mwe!!! Aibu aisee,🏃🏃🏃🏃. Lakini inawezekana labda mkeo / mumeo ulikuwa ukimsapoti uvaaji, pesa na manukato n. k lakini sasa vipi? Mbona umeacha kusapoti kumpendesesha mkeo? Hata hivyo, kama huna nguo mpya na hayo mengine sasa ndio uwe mchafu. Kuna wanandoa ukiwaangalia huwapatii picha maana wapo wapo tu lakini papo hapo wapo pia wanandoa ambao ukiwangalia unawatamani jinsi wanavyopendeza kwa usafi. Ninajua jambo hili watu wa ndoa wanajitahidi sana, lakini ni tatizo kwa wengine wachache. Mpendwa wajibika na suala la usafi uboreshe ndoa yako isifike wakati hata underwear (chupi) unashindwa kufua nice aibu na utamkera mwenzako!

05. Mke sio shamba!

Hii ni kwa waume ! Sikia ;

Shamba ni kipande cha ardhi kilichotengwa kwa uzalishaji. Ndani ya shamba kunapandwa mazao mengi lakini pia kunatupwa uchafu mwingi. Ndani ya shamba maji husukumiwa huko n. k lakini shamba limenyimwa mdomo, lenyewe haliongei, wala halina ruhusa ya kukataa chochote isipokuwa ni lazima likubali tu. Shamba halina sauti, shamba linanyanyaswa kwa kweli! Shamba halina msaada bali linaamriwa kufanyiwa chochote na linatakiwa lazima litii si shamba lakini! Sasa, mke hapaswi kuwa kama shamba. Katika ndoa yako ni lazima ujue hilo, kwamba mkeo sio kama shamba. Kwa maana wapo wanaume ambao wao ndio kila kitu hata mkewe hatakiwi kuzungumza chochote bali atii yote hata ya upumbavu, eti atii tu. Mkeo hana sauti yoyote na hasikilizwi kwa lolote, hata akisema “ nimechoka leo mume wangu ” lakini wewe mume unasema “… nyamaza kimya wewe ni mwanamke tu, umeumbwa unitumikie mimi, ebu fanya hivi sasa…. ” tena hata tendo anakupa basi tu kwa sababu wewe ni mkali umemfanya mkeo ni shamba!!! Ni mbaya sana kufanya hivyo! Wakati mwingine mkeo anakuambia kweli “ninaumwa leo, sijisikii vizuri mume wangu, niombee… ” badala ya kumwombea na kumwacha apumzike, bali wewe unasema “ mwongo wewe, mimi ni mumeo, chukua nguo zangu unifulie, nena kateke maji ujaze tanki kwanza hilina uhakikishe nikuone kitandani mara moja baby nakuhitaji, wewe si unajua leo ndio mapumziko yangu? … ” khaa! Huu sasa ni utumwa jamani, kwani kupumzika kwako ndio umchoshe na kumnyanyasa mkeo? Haifai, mke sio shamba hata kidogo!

Hakikisha usimfanye mkeo kuwa kama shamba, kwa maana hapo hutaweza kuiimarisha ndoa yako. Jaribu kumsikia mkeo, huyo ndio mwanamke wa pekee duniani aliyekuwa mzuri kwako, hakuna kama huyo. Ndani ya mawazo / mtazamo wa wanaume wengi hufikiri kazi zote za nyumbani afanye mke, basi kila kitu husukumiwa mwanamke kwa sababu eti mume ni baba wa nyumba! Sio sawa kwa mkeo kufanya kila jambo, wewe pia unatakiwa kuwa sehemu ya kazi azifanyazo mkeo na hilo ndilo penzi, mapenzi ni kusaidiana kila mmoja.

Wewe ni shahidi katika hili, kwamba utakuta mwanaume karudi kutoka kazini na siku nyingine yupo tu nyumbani lakini hapo ndipo mke awaandae watoto kwenda shule, huyo huyo akachukue bili ya maziwa mtaa wa sita huku mavyombo ya kuosha yanamsubiri, kufagia dada atafanya lakini chumbani mke hu, huyo huyo usafi wa chumbani kunamsubiri, akirudi afue nguo za mumewe na nyinginezo, hapo yupo hoi, kupika kunamsubili kama yupo mdada wa kazi atamsaidia lakini mume ndio kasema nataka wewe ndio unipikie chakula chako mke wangu, akiwa hoi mume anamwitaji tena, na ole wake mke aseme amechoka, basi hapo si makelele ya mwanaume yatakavyosikika eti kwa sababu tu mkewe kasema amechoka, lakini si amechoka kweli, kwani wewe hufikirii, siku nzima mkeo anahangaika na weww umetulia tuli na “msuli wako ” umeuvaa huku ukicheki tv. Haifai hivyo, mke sio shamba jamani yeye pia ni mwanadamu awe na muda wa kupumzika. Jaribu kulifanyia kazi hili kwa ukuaji wa ndoa yako.

Haya, nipigie simu sasa kwa msaada zaidi pamoja na tuzungumze mambo ya ndoa.

Kwa mawasiliano zaidi piga Kwa +255 683 877 900

What’s app ni +255 746 446 446

ITAENDELEA.

UBARIKIWE.

Comentários


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page