top of page

MWOTA NDOTO.


Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi sana …

Siku zote mwota ndoto hapendwi, tangu enzi za mwota ndoto Yusufu hata leo hali imekuwa vile vile. Ukitafuta sababu zinazofanya kumchukia yeye mwenye ndoto, kwa kweli hutaziona bali utakachokiona ni kwa sababu ya ndoto zake tu ndio zimesababisha chuki kubwa ya namna hii. Ebu jifunze kwa Yusufu, kijana aliyependwa na baba yake Yakobo (Mwanzo 37;3).

Ingawa Yakobo alimpenda sana mwanae Yusufu kiasi kwamba kukawa na chuki kwa watoto wake wengine lakini bado inaonekana Yusufu alikuwa akitenda mema ya kumpendeza babae, hii inakufundisha kwamba kama utatenda mema utapata tu kibali kwa baba yako. Jukumu la Yakobo lilikuwa ni kuwapenda sawa watoto wake wote 12 lakini haikuwa hivyo kwa sababu wale watoto 11 ( ukimwondoa Yusufu) walikuwa watenda mabaya mfano tu angalia mtoto mkubwa Reubeni ambaye alilala na mke wa babaye ( ni sawa na kusema alitembea na mama yake).

Sasa je hili si baya? Lakini ndugu zake na wenyewe waliendelea kutenda mabaya kitu ambacho kikamfanya baba yao Yakobo kuendelea kumpenda mwanae mdogo Yusufu ( maana hata hivyo hapo kwanza Yakobo alimpenda mkewe Raheli aliyemzalia Yusufu kulikuko wengine, hata watoto wake Yakobo akawapenda). Lakini hata sasa kama kuna mtoto mmoja ambaye ni msikivu mtenda mema kwa maagizo uyaagizayo, Je hutatokea kumpenda kuliko ndugu zake?

Ndoto za Yusufu (Mwanzo 37:5-11).

Huu ulikuwa ni mwanzo tu, kwa kijana mdogo kama Yusufu kuota ndoto kubwa namna ile, hajawai kurekodiwa mahali popote kwenye biblia kwa kijana mdogo kuwa na ndoto kubwa kama za Yusufu. Hii inatuonesha wazi kuwa Mungu yupo na anaweza akasema na mtu yoyote yule. Mungu anampango hata katika maisha yako, wewe pia unazo ndoto.

Yusufu mwenye umri wa miaka 17 tu akapata kuota mambo makubwa ya miaka mingi ijayo, hata yeye hakuwa akijua nini hasa maana ya zile ndoto zake. Hii ni sawa kabisa kwako, pale unapoota jambo fulani kubwa na kukosa kujua maana yake! Ndio, inafanana kabisa!!!

Ebu jiulize katika ndoto unazoziota hivi karibuni, Je unazijua maana yake? Na ikiwa la, je hufanani na Yusufu ambaye kwa kweli naye hakujua afanye nini. Bila shaka Mungu alikuwa akisema na Yusufu kwamba yeye Yusufu si mtu wa kawaida kwa maana ndugu zake watakuwa chini yake pasipo kujali wao ni wakubwa lakini yeye ni mdogo.

Hata kwako, unaweza ukawa juu ya ndugu zako wakubwa katika kile ulichonacho kwenye ndoto. Eneo zima la ndoto ni eneo pana sana kwa maana ni mambo yaliyobeba mafumbo / mambo yaliyojificha sana.

Hivyo kuna ndoto ambazo Mungu anasema na wewe kwa niaba ya kwenda kuwaambia watu, na kuna ndoto ambazo Mungu anasema na wewe tu pasipo kumshirikisha mtu yeyote kwa muda mrefu sana. Ndoto za Yusufu zilikuwa ni za kwake kwake tu, kumwonesha yeye atainamiwa na ndugu zake.

Lakini hata hivyo, inaonekana ni Mungu huyo huyo ndiye aliyemtaharakisha Yusufu kuzisema ndoto zake kwa ndugu zake wanaomchukia na ni Mungu huyo huyo ndiye aliyewafanya ndugu zake kutafsiri ndoto hizo kwa usahihi wake ili kusudi mambo yote yatimie.

Unajua ni rahisi kuota lakini si rahisi kutafsiri, na ndio maana wengi huota lakini hawajui tafsiri yake,kazi ya kutafsiri ndoto ni kazi ya Roho mtakatifu. Lakini cha ajabu ndugu zake Yusufu ambao wenye mioyo ya uchungu, hasira, na hila ndio walitafsiri ndoto hizo tena kwa usahihi wake. Je huyo si Mungu aliyekamata vivywa vyao na kutafsiri katika usahihi wake? Ndio ni Mungu.

Je tunaweza kumlaumu Yusufu kwa kuzifunua ndoto zake kwa ndugu zake?

Hapana, hatuwezi kumlaumu kwa kuwa inaonekana kulikuwa na msukumo wa kiungu katika hili. Lakini si vyema kuwa msemaji juu ya ndoto zako kwa watu wasio sahihi kwako kwa maana wanaweza kukuchelewesha kufikia ndoto hizo. Kumbuka ; Roho mtakatifu ndiye rafiki yako wa karibu anayepaswa kushirikishwa yote oli akusaidie hata kukuongoza ni nani wa kumwambia na ni nani usimwambie, kwa maana kuisema ndoto yako si kigezo cha kuifanya itimie. Hivyo hakikisha ni nani unayemshirikisha ndoto zako.

Adui wa kwanza ni mtu wako wa karibu, ebu fikiria kwa ndugu zake Yusufu, ni ndugu wa damu moja lakini ndio hao hao waliokuwa maadui wakubwa. Kilichowafanya kumchukia Yusufu mdogo wao si kingine ni ndoto tu ( Mwanzo 37 :19). Hii inaonesha dhahiri kabisa kwamba hata wewe adui yako wa kwanza ni ndugu zako, watu wa karibu, rafiki zako wa karibu n. k

ambao kama wataizisikia ndoto zako za kuinuliwa kwako, basi ujue hawatakupenda na utashangaa kuona watu mliokuwa mkishibana ndio wa kwanza kukuchukia. Sasa yakitokea hayo, ujue ni ndoto zako tu ndicho kinachowasumbua hao. Hivyo si vyema uwaambie kila kitu ili kupunguza maadui, mengine waambie unapopata kibali cha Bwana na mengine makubwa usiwaambie wasije wakakuua au kukuchelewesha kufikia ndoto zako.

Je una ndoto?

Bila shaka jibu ni ndio. Lakini jambo muhimu kujua sasa ni kwamba ndoto hizo ni ndoto tu, bado hazijawa na uhalisia, na hapo unamwitaji Mungu sana akusaidie. Unahitaji utulivu mkubwa kwa kufunga kinywa isipokuwa pale tu inapobidi. Mchungaji ni kiongozi wa kiroho anapaswa kushirikishwa ndoto zako kusudi akusaidie katika uwanja wa maombi pamoja na ushauri na si vinginevyo.

Hata katika hili ni lazima ujue ni mchungaji yupi unaweza kumweleza ndoto zako, kwa maana wengine wanaweza wasikusaidie. Usiogope kuchukiwa sasa kwa sababu ya ndoto ulizonazo, kwa maana watu wanaokuchukia sasa ndio hao hao watakaokupenda pale watakapokuona upo juu.

Watu watakukatisha tamaa kwa maneno mengi, lakini wewe mwangalie Bwana tu, na simama katika neno lake, nami nakwambia ijapochelewa ndoto yako lakini isubiri, na itakuwa hivyo. Kumbe, uvumilivu unahitajika sana katika eneo la ndoto zako… Anyway , Niishie hapa bhana,. 😁😁😁

Kwa msaada zaidi pamoja na maombezi, ushauri + 255 683 877 900

Na mch Gasper Madumla.

What’s app ni +255 746 446 446

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page