MWONGOZO WA UINJILISTI WA NYUMBA KWA NYUMBA.
- Mch. Gasper Madumla
- Oct 28, 2016
- 5 min read

Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi;
01.Uinjilisti wa nyumba kwa nyumba,nini maana yake?
Uinjilisti ni uinjilisti,lakini tunapozungumzia “..wa nyumba kwa nyumba” Tunamaana ya kumtangaza/kumhubiri Yesu nyumba moja hadi nyingine,mtaa kwa mtaa pasipo kuangalia imani ya wenyeji/wakazi wa nyumba wala pasipo kuangalia itikadi za chama,kabila,rangi n.k. Na kwa sababu ni kazi ya kujitoa hasa,wengi wamejikuta wakiisukumia mbali. Lakini ndio kazi kubwa ya injili kuliko kazi nyingine ya injili kwa sababu kupitia uinjilisti wa nyumba kwa nyumba kuna kuzaa matunda ya kudumu kuliko uinjilisti au semina ya aina yoyote.
Yesu naye alipita pita kuhubiri,na aliingia kwenye nyumba za wenye dhambi kwa lengo la kupa habari njema. Tazama pale alipoingia kwa Zakayo yule mtoza ushuru mwenye dhambi (Luka 19:5-6),Naye akawafundisha neno la ufalme wa Mungu. Soma pia Mathayo 8:14. -Na mfano mwingine kwa Stephano Matendo 8:27-35, Luka 4:38-39 N.K)
Kwa nini injili?
Ni agizo kuu ( Mathayo 28:19)
Kuwafanya watu kuwa wanafunzi.
Kushiriki pendo la Mungu kwa waliopotea
Kulitambulisha kanisa,ili watu wakapate mahali sahihi pa kuabudu.
Kuleta faraja ndani ya mioyo iliyoumizwa. N.K
Hivi unajua huko kwenye majumba ya watu kuna mambo mengi,kwa maana wapo wakristo ambao wameacha ukristo kwa sababu walijeruhiwa na watumishi wao waliokuwa wakiwaamini kama watumishi wa Mungu. Pia wapo wakristo walioacha ukristo kwa sababu wamekamatwa na dhambi,pia wapo watu ambao ni wagonjwa waliolazwa majumbani ambao wanatamani hata kusikia neno la Mungu kutoka kwako. Lakini pia wapo watu wa kawaida ambao huwezi kuwapata kwenye mikutno ya injili,wala huwezi kuwapata kwa njia ya radio,wala kwa njia ya kanisani isipokuwa unaweza kuwapata kwa kuwafuata majumbani kwao tu. Na ndio maana unjilisti wa aina hii ni muhimu sana
Namna ya kuinjilisha / kulishuhudia neno.
Hakuna mpangilio rasmi isipokuwa kuongozwa na Roho mtakatifu ndio mpangilio rasmi. Na ndio maana hata kabla ya kwenda kwenye nyumba za watu yakupasa uombe sana,ili Bwana awe pamoja nawe.Yaani ujipange ukimtegemea Mungu tu,usitegemee akili zako wala fahamu zako,bali umtegemee Mungu tu. Hivyo ni lazima uwe msomaji mzuri wa neno la Mungu,ujipange pamoja na maombi kwako yasikauke. Yafuatayo ni mambo ya kawaida kama mwongozo wa kawaida kabisa utakao kusaidia pamoja na Roho mtakatifu;
Salimia na kujitambulisha – Usiseme “Bwana Yesu asifiwe…” Ingawa ndio salamu yako. Kwa sababu kwanza hujui ni mtu gani unayeongea naye,kwa maana wengine wakisikia salamu ya namna hiyo wanakimbia na utawakosa. Bali msalimie kikawaida kabisa,kama mtu mzima mwambie “shikamoo…” Kisha endelea kujitambulisha wewe ni nani,unatokea wapi,umekuja kufanya nini hapo..n.k”
Omba kidogo – Ikiwa umepata nafasi,basi umshukuru Mungu kwa kidogo. (Maombi yatawaliwe na hekima ya Bwana,yasiwe marefu sana wala yasiwe mafupi sana.)
Moja kwa moja anza na ujumbe wa neno la Mungu.
Kisha mpe nafasi naye aseme kitu chochote labda alichoelewa,kisha omba nafasi ya kuomba naye. Ili uumpe nafasi ya kumpokea Yesu. Lah akikataa basi omba naye dakika chache. ( Kakati ujumbe wako,ujifunze kumtia moyo )
Msaidie katika swali,au hoja,au mashaka aliyokuwa nayo-ikiwa kama atakuuliza. Nawe mjibu kwa ufupi kwa kuchagua maneno ya kujibu.
Mwalike katika ibada zenu na kumpa kipeperushi chenye kuonesha ratiba za ibada zenu.
Mpe kitabu cha hongera kwa kuokoka ikiwa kama kipo.
Urudipo kanisani,chukua hatua ya kumuombea tena huko huko aliko.
Mambo muhimu ya kuzingatia katika injili;
Zima simu zako / weka vibration. (Kumpa nafasi Roho mtakatifu)
Kuwa smart. ( Kumbuka,usmart ukizidi sana nayo ni shida,hiyo kuwa mtu wa kawaida nadhifu)
Ikiwa kama mpo wawili au zaidi,basi mnie mamoja na awe muongeaji mmoja kwa niaba ya wengine. Ikiwa mwingine anahitaji kunena basi mwingine na anyamaze ili muweze kusikilizana.
Msilinene vibaya kanisa,wala msinene vibaya mchungaji wenu kusudi watu wa nyumba wasije wakasikia wakawadharau au kuwakataa ninyi pale mnenapo.
Acha mizaha./Kazi ya injili haitaji mizaha!
Ulenge kwenye kusudi isiwe unafika nyumba fulani basi badala ya kushuhudia unataka maji ya kunywa,au chakula,au unabweteka kwa mazingira( labda mazingira ni mazuri kisha waanza kumuomba mwenyeji akuwashie TV kidogo umalizie mpira unaoendelea katika TV N.K)
Usipendelee katika injili yako,bali sema kweli ya Mungu (Sio unamwangalia mtu kisha unamtengenezea somo lake kwa sababu ya namna anavyoonekana)
Usioneshe utofauti wa imani yako (Labda kujiinua,na kujiona wewe ni bora sana)
Hakikisha; – Unawafuatilia wale wote uliowatembelea ( Wale waliokoka na hata wale wasiokoka.
Changamoto ;
Hakuna kazi iliyokosa changamoto,hata kazi ya injili ya nyumba kwa nyumba ina changamoto zake. Mara nyingi changamoto za injili ya mtaani zinafanana. Baadhi ninaziona kuwa ni changamoto;
I).Changamoto eneo la wainjilisti.
Hofu hata kushindwa kujieleza vizuri. ( Mara nyingi ukianza vibaya katika kujieleza basi kunakufanya kupoteza lengo kamili la ushuhudiaji.)
Neno hafifu- Wapo wainjilisti wanaokwenda nyumbani kwa mtu kuwafundisha neno na kwa sababu ya maarifa machache ya Mungu waliyonayo hujikuta wakifundishwa wao na mwenye nyumba yaani wanahubiriwa wao badala ya kuhubili.
Maombi kukosekana – Mshuhudiaji lazima awe mwombaji.
Kukosa upendo baina ya washuhudiaji. ( Ikiwa washuhudiaji wa siku wakikosa upendo basi hawawezi kutembea pamoja kwa maana watu wawili hawawezi kutembea pamoja wasipopatana Amosi 3:3-“ Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana? ” )
II.Changamoto kwenye nyumba za watu/site.
Zifuatazo ninazitazama kuwa ni chamnamoto ambazo mwinjilisti anaweza kukutna nazo;
Upinzani mkali wa kidini katika huko nyumbani.
Kukataliwa pamoja na injili.
Kushindwa kupokelewa vizuri au kutopokelewa kabisa.
Kutakwa kimapenzi pale unapokuwa jinsia tofauti. Kama mwinjlisti ni binti anamhubiria mkaka,mkaka anaweza akamtazama kwa lengo la kumtaka. Au hata kama mwinjilisti ni mkaka anaweza akategwa.
Mashambulizi ya kiroho / nguvu za giza kujaribu kurudisha mashambulizi.
Kukatishwa tamaa kwa namna nyingi – Unaweza ukawa unamfundisha neno mtu halafu huyo mtu akawa anachati kwenye simu yake au akawa anaangalia TV wala hakujali kabisa! (Bali usichoke) N.K
Kuulizwa maswali ya kijinga jinga kwa nia ya kukejeri n.k
Ni nini mwinjilisti anapaswa kujua katika maandalizi yake?
“ Maswali chochezi ” Lazima mwinjilisti ajue majibu ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara na watu. Mfano watu wasiookoka huuliza “kuokoka ni nini? ,kwani mtu aliye hai anaweza kuokoka na bado anaishi?…” Yapo maswali mengi sana ambayo ni yale yale ya siku zote yamekuwa yakiulizwa ulizwa. Hivyo akama mwinjilisti unapaswa kuwa na majibu yake kabala hujaenda huko mtaani. Miongoni mwa maswali ambayo kila mwinjilisti anapaswa kuyafanyia kazi na kujua majibu yake ni ;(Maswali haya ni miongoni ya maswali yanayoulizwa sana)
Je Yesu ni Mungu? Imeandikwa wapi?
Kuokoka ni nini maana yake?
Dini ipi ni ya kweli? Kwa nini umnaabudu Jumapili?
Hoja juu ya ubatizo wa maji mengi.
Hakuna mambo ya kunena kwa lugha,imeandikwa wapi?
Hoja juu ya udhihirisho wa Roho mtakatifu. Kwanza ni nani huyo Roho mtakatifu?
Wagalatia ni akina nani? Je sio wakristo msio na akili?
Sanamu ni nini? nani anaabudu sanamu?
Nguruwe ni najisi?
Je ni kweli mwanamke anaruhusiwa kufundisha? Mbona biblia imekataa? wewe vipi?
Suala la kuwa mtoto wa Mungu na kuwa mwana wa Mungu.
Maswala ya ndoa na mahusiano.
Dhambi ni nini? (Maswala ya makosa na msamaha)
Je idara ya uinjilisti inahitaji kuwa na uongozi?
Jibu ni ndio. Idara iliyo kamili inahitaji kuwa na uongozi kamili. Kwa kuwa tunazungumzia kazi ya injili tunahitaji pia kuwa na viongozi watakaoongoza wengine; Katika idara hii;hatuitaji kuwa na safu ndefu ya viongozi,bali viongozi wachache wanatosha;
Mwenyekiti
Katibu
Mwekahazina
Wajumbe wawili ( Kama muhimu,wanaweza kuwepo)
Mwenyekiti.
>Kuratibu vikao vyote vya idara ,pia kupanga eneo la injili.Kusimamia utekelezaji wa kuzifuata roho za watu zilizookolewa kipindi cha ushuhudiaji..Kupokea taarifa muhimu kutoka kwa mchungaji na kuziwasilisha kwenye idara.Kubeba nembo na taswira halisi ya kanisa.
Katibu.>Kuandaa vikao mbali mbali vya uinjilisti kwa idhini ya mwenyekiti.Kutunza kumbukumbu za watu waliookoka pamoja na mawasiliano yao ya simu.Kuandaa minutes,agenda na kusoma katika vikao.
Mwekahazina.>Kutunza pesa za uinjilisti katika mpangilio mzuri.Kutunza mapato na matumizi ya kifedha katika idara ya ushuhudiaji.Kutoa taarifa za mapato na matumizi.Kutoa pesa ya kutengeneza vipeperushi,au vijitabu vya hongera ya kuokoka.Kuwasilisha katika uongozi makusanyo yote ya sadaka yatakayopatikana wakati wa kushuhudia.
Wajumbe watatu.>Watafanya kazi yoyote watakayopangiwa na viongozi wao. (Pia kiongozi wa nidhamu anaweza akawepo hapa)
Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe. Kwa msaada zaidi,pamoja na MAOMBI ; piga sasa ; +255 683 877 900.
Whats app namba ; +255 746 446 446
Na Mch.G.Madumla.
UBARIKIWE.
Comments