MWONGOZO,IDARA YA VIJANA.
- Mch. Gasper Madumla
- Oct 16, 2016
- 6 min read

“Mwongozo” ni taratibu zinazoongoza kikundi fulani cha watu. Kwa lugha nyingine mwongozo huitwa “ katiba ” yenye kanuni zilizopitishwa na wajumbe wa kamati kuu. Hivyo katika kila kikundi,au idara ni vyema pawe na utaratibu wa namna gani idara au kikundi au chama kitaenda kwa kufuata “katiba/mwongozo ”
Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi,
Kikundi pekee chenye idadi kubwa ya watu/wanachama katika makanisa mengi ulimwenguni ni kikundi/ idara / chama cha vijina. Kwa kuwa wao ndio kundi la walio wengi,basi ni lazima kundi hilo liongozwe na katiba/mwongozo ulioenda shule/ katiba nzuri. Najaribu kuliandikia kundi hili rasimu ya mwongozo ambao nafikiri unaweza ukawafaa kwa sehemu fulani ;
01. Kijana na kanisa;
“…Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu. ” 1 Yoh.2:14
Biblia inamtazama kijana kama mtu mwenye nguvu lakini pia mwenye kuweza kulihifadhi Neno la Mungu ndani yake. Hivyo biblia haijakosea kumwona kijana kama mtu mwenye nguvu,kwa maana tangu mwanzo Mungu aliwatumia sana vijana katika nyanja tofauti tofauti.
Kijana kama Yusufu mwenye umri wa miaka 17 tu (Mwanzo 37:2),Kijana kama Yeremia ( Yer. 1:6-7),Kijana kama Timotheo,Yosia,Daniaeli na wenzake,n.k wote hawa walikuwa ni vijana ambao Mungu aliwatumia.(Hata mama yake Yesu Mariamu alikuwa ni kijana Mungu alipoanza kumtumia,hata Yesu mwenyewe alikuwa ni kijana.)
Katika zama za leo kumekuwa na utata kuhusu kijana ni mtu gani? Utata huu umeingia hasa katika makanisa mengi,na kupelekea kushindwa kumwelekeza kijana akae katika idara ipi hasa,maana utakuta mtu ni kijana kwa umri lakini ameoa au kuolewa,Sasa hapo ajui akae katika idara ya wamama / wababa au aendelee kukaa katika idara ya vijana?!
Na kwa sababu hiyo tumeshuhudia vijana wengi wapo katika idara ya wababa kwa waliooa au wapo katika idara ya wamama kwa walioolewa,na wengine wameamua kubaki kule kule kwa vijana. Ukiona hali ya namna hii,ujue ni “suala la mwongozo “ limekosekana hapo, hivyo Kila mmoja anafanya atakachoona sawa kwake!!!
Kwa mujibu wa serikali,yenyewe Haina migogoro au utata wa namna hii,Kwa maana serikali inamtambua kijana kwa kumpima “umri” wake hata kama kijana yupo katika ndoa. Na umri wa serikali wa kijana ni kati ya miaka 15-40-45 . Hivyo kikanisa tunaangalia si umri tu bali hali yake ya familia ( amezaa,au ana watoto,ameoa / kuolewa?). Pamoja na hayo ni vyema umri nao ukaangaliwa pale inapobidi.j
Matokeo ya vijana wakisimama vyema ndani ya kanisa;
Kukua na kuongezeka kwa kanisa
Kuimarika kwa ulinzi wa kiroho na kimwili ndani ya kanisa
Kukuza uchumi wa kanisa
Kumsaidia mbeba maono na kuhakikisha maono ya kanisa yanasonga mbele
N.k
Mambo ya kuzingatia kwa vijana.
Yapo mambo mengi ya kuzingatia katika idara ya vijana na hasa kwa kijana mmoja mmoja. Lakini katika hayo yote lililo kuu ni ;
01. Usafi wa roho na mwili
Kawaida vijana “wana mvuto “ kiroho hata kimwili. Hivyo ndio kundi pekee ambalo linawindwa sana na shetani kwa maana ndio kanisa linategemea nguvu kazi kubwa kwa vijana. Neno “Usafi wa kiroho na kimwili “ linalenga kuhusu “kujitunza pamoja na suala la uaminifu” kwa maana katika mvuto aliokuwa nao kijana,ni vigumu kujilinda pia ni vigumu kujitunza ingawa vyote viwili vinawezekana. Hiyo ndio vita ya kwanza ya vijana,( kutunza ujana wao dhidi ya anasa za dunia hii). Njia pekee ya kuutunza ujana,ni kukubali kuwa mwanafunzi katika kanisa moja.
Maono na malengo ya vijana.
Kuwa mwanafunzi (beaing disciple )
Kuwafanya watu wengine kuwa wanafunzi ( To make more disciples ) Mathayo 28:19
Kuwa na umoja katika chama cha vijana.
Muundo wa uongozi kwa vijana:
Kamati kuu.
Kamati mbali mbali.
(i) Kamati kuu:
Muundo wenye kueleweka na unaotumika sana katika kamati kuu ni kama ifuatavyo;
Mwenyekiti
Makamu mwenyekiti
Katibu
Makamu katibu
Mtunza pesa.
N.B – Mchungaji wa vijana ( au yeye aliyeteuliwa na uongozi)ndie mwangalizi mkuu wa idara,yeye aweza kushauri jambo katika nafasi yoyote.
ii).Kamati mbali mbali. – Inapendeza kusiwe na kamati nyingi kwa maana kutakuwa na mwingiliano wa kazi. Kamati zifuatazo,ni kamati pendekezi zenye umuhimu kusaidia kamati kuu;
Kamati ya maadili/Nidhamu na mahusiano.( ina Mwkt,&Katibu,au mwkt peke yake.)
Kamati ya mipango.( Ina Mwkt,Katibu na mjumbe 1)
Namna viongozi wapatikanavyo:
Kwa kupigiwa kura / election.
Kwa kuteuliwa / apointing
Sifa za viongozi;
Si lazima sana kwa kila kiongozi awe na sifa hizi zote kwa sababu hatutafuti mtu mkamilifu bali Bwana amkamilishe ( kwa maana Bwana anamwita mtu jinsi alivyo) lakini ni lazima kijana awe huru mbali na dhambi (We are not looking for a perfect one but one who is free of pettern of sin). Hakuna mtu atakaye kamilika kwa sifa zote,bali katika kuchagua angalia zile sifa muhimu tu,nayo yatosha. (Kabla ya kuchagua au kuteua pitia sifa hizi zifuatazo)
Safi kimwili na kiroho.
Asiyelaumika / above reproach
Mwenye kiasi na busara.
Mwenye utaratibu.
Mwenye kukaribisha/mwenye ukarimu.
Ajue kuelekeza vijana,afundishe panapobidi./mwenye neno la kushirikisha vijana.
Ajue kuelekeza vijana,afundishe panapobidi./mwenye neno la kushirikisha vijana.
Kuambatana na viongozi wenzake.
Si mkolofi./asiwe mwenye hasira za haraka.
Mpole.
Mpatanishi,si mchochezi/wala asiwe mtu wa vikundi vikundi kiasi kwamba akawa na makundi yake binafsi.
Asiwe mwenye kupenda fedha na mapato ya aibu.
Ameshuhudiwa mema na vijana wenzake.
Mstahivu / mvumilivu.
Mwenye kauli moja / Asiwe na kauli mbili mbili.
Mwaminifu.
Mwenye nidhamu kwa wenzake na vijana wote.
Muwajibikaji kwenye shughuli mbali mbali za vijana na kanisa.
Awe mberoya halisi.
Mtunza siri.
Mcheshi kidogo.
Asiruke mamlaka aliyopewa. (Mfano: Akiwa na jambo asilipeleke moja kwa moja kwa mchungaji au kwa Apostle bila kulijadili na viongozi wake. Ni makosa makubwa sana kupeleka kila jambo kwa wachungaji bila kulijadili. Isipokuwa kama kutakuwa na ulazima,aweza kulipeleka jambo kwa mchungaji)
Kazi za viongozi.
01.Mwenyekiti wa vijana;
Msemaji mkuu wa umoja wa vijana.
Ni mwenyekiti wa vikao vyote vinavyomuhusu.
Kusimamia utekelezaji wa kila agenda kwa muda unaeleweka.
Kupokea oda/taharifa muhimu kutoka kwa mchungaji/apostle.
Kusimamia usafi wa kanisa ( Mfano; kufua majoho ya ubatizo pale yanapotumiwa ikiwa kama hayatapelekwa drycleaner,kuondoa chupa za maji zilizotumika ikiwa zitakuwa zimetupwa mahali pengine nje ya dustbin)
Kubeba nembo na taswira ya kanisa lake,ndani na nje ya kanisa. N.K
Makamu mwenyekiti.
Kukaimu nafasi ya mwenyekiti katika hudhuru wa mwenyekiti.
Kusimamia kazi zote ziende sawa sawa kama agizo la mwenyekiti wake.
Aweza kuendesha kikao kwa kibali cha mwenyekiti wake.
Kubeba nembo na taswira ya kanisa lake,ndani na nje ya kanisa. N.K
Katibu.
Muandaaji wa vikao mbali mbali (awe mbunifu) kwa idhini ya mwenyekiti.
Kujali/kukontroo muda katika vikao vyote.
Kutunza kumbu kumbu vizuri.
Kuandaa minutes,agenda na kusoma katika vikao.
Kuandika mipango mifupi na mipango mirefu ya umoja wa vijana kwa mwaka huu na mwaka mmoja ujao. ( To have short and long plan for the BBFC youth) kwa kushirikisha viongozi wenzake.( Mipango yote itaanzia kutoka katika kamati ya mipango na maendeleo,kisha itawasilishwa kwa katibu)
Awe ndie mratibu wa kutoa taharifa kwa hidhini ya mwenyekiti.
Katibu msaidizi.
Kushirikiana na katibu kuandaa vikao vyote kwa mujibu wa mwenyekiti.
Awe mbunifu-Kupanga njia mbadala wa kuwasilisha agenda.
Kukaimu nafasi ya katibu katika kutokuwepo kwa katibu.
Mwekahazina.
Kupokea ada na michango yote ya umoja ( kama itakuwepo)
Kutunza mali na fedha zote za umoja.
Kutunza kumbu kumbu ya mapato na matumizi ya umoja wa vijana.
Kubuni njia za kuingiza pesa katika mfuko wa umoja wa vijana.
Kufanya malipo na manunuzi halali.
Kukusanya risiti zote za manunuzi na kuzihifadhi.
Kutoa taharifa za mapato na matumizi mara kwa mara kwa viongozi na wajumbe wote.
Kamati ya nidhamu na mahusiano.
01. Mwenyekiti wa nidhamu.
Kuongoza vikao vyote vya kamati ya nidhamu.
Ndie msemaji mkuu wa kamati ya nidhamu.
Kurejeza kijna aliyeanguka kinidhamu kwa upendo,kumuonya.
Kutoa taharifa mara kwa mara kwa viongozi wa kamati kuu kuhusu hali ya kinidhamu ya vijana. Taharifa zifike pia kwa mchungaji,ili mchungaji aweze kujua hali ilivyo na kuwaadabisha wale wote wasiotaka kwenda sawa.
Kuhakikisha vijana wanakuwa na mahusiano mazuri- mahusiano ya ndani na nje ya umoja.
02.Katibu.
Kuandaa vikao mbali mbali na agenda kuhusu hali ya kinidhamu sawa sawa na makubaliano ya mwkt.
Kuandika kila taharifa ya kijana atakaye hojiwa na mwenyekiti wa nidhamu.
Kusoma taharifa zote za vikao.
03.Wajumbe wawili.
Kutekeleza yale yote walioshirikishwa katika vikao vya kinidhamu.
Kamati ya mipango.
Majukumu au kazi kubwa ya kamati hii ni kubuni njia za maendeleo ya umoja wa vijana ( njia sahihi sawa sawa na imani tuliyokuwa nayo) Watakuwa na kazi kama ifuatavyo:
Mwkt wa kamati.
Ndie msemaji mkuu wa kamati. Awe mbunifu.
Kupanga mipango mifupi na mirefu na kuwasilisha kwa uongozi.
Kusimamia mipango yote inapewa kipaumbele katika kamati kuu.
Katibu.
Kuratibu shughuli za mipango ya kimaendeleo.
Kutunza kumbu kumbu za mipango ya kimaendeleo ya umoja.
Kuandika mawazo yote ya mipango mifupi na mirefu ya mwaka sawa sawa na maamuzi ya kikao husika.
Mjumbe.(aweza kuwa mmoja au zaidi ya mmoja kulingana na matakwa ya kikao)
Kushirikiana kimawazo na katika msaada wowote sawa sawa na mahitaji husika ya kikao.
Kumbuka:-Katika kamati zote ni lazima viongozi wafanye mambo yafuatayo,Kudumisha upendo katika umoja wa vijana,Kusimamia na kushiriki ibada zote za kanisa bila kukosa,pia kujitoa kushiriki maombi.(Ikiwa kama kiongozi kiongozi anahudhuru,basi ahakikishe anatoa taharifa kwa mwkt na uongozi mzima wajulishwe kutokuwepo kwake.)
Kujiunga na umoja/Idara ya vijana;
Mshirika yoyote wa kanisani ambaye ni kajana anaruhusiwa kujiunga. Kama kukiwa na ada ya kujiunga,haitakuwa sawa kwa maana wengine wanaweza kukosa ada hiyo na ukawa umewafukuza. Hivyo pasiwepo na kigezo/masharti magumu ya kujiunga bali milango iwe wazi kwa vijana wote,wajiunge na idara ya vijana.
Sifa za kijana anayepaswa kujiunga na umoja huu:
Awe tayari /bila kulazimishwa.
Awe mshirika wa kanisa/ lah akiwa si mshirika bado mnaweza kumchukua kwa maana huo ndio mwanzo wa yeye kuwa mshirika.
Ni vyema asitumikie idara mbili tofauti ( Mfano haipendezi sana awe upande wa idara mbili,labda awe idara ya wamama kisha papo hapo yupo kwa vijana)
Awe mtunza siri za umoja wa vijana.
Kujitoa /kuacha idara.
Kijana yeyote anaweza kuamua kuahama,kanisa,kuacha kuwa mwanachama,bila kumlazimisha. Isipokuwa afuatiliwe.
Kumbuka ; Majukumu ya vijana wote; Moja ya jukumu kubwa la vijana wote ni kumpenda Mungu. Na mengine yatafuata katika hili.
Ikiwa kama umejifunza kitu, nifahamishe. Kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga kwa+255 683 877 900
What’sapp namba +255 746 446 446
Mch. G. Madumla.
UBARIKIWE.
Comments