top of page

 MWANAMKE WA MITHALI 31. ~ 01

Na Mch Gasper Madumla.


Bwana Yesu asifiwe….

Kwa ufupi.

Huyu mwanamke ni mwanamke wa namna gani jamani! Kwa maana anavutia kwa sifa zake. Hakika mwanamke wa namna hii ni mtumishi wa Mungu. Mojawapo ya sifa nzuri aliyonayo ni sifa kuwa na “roho ya kicho kwa Bwana”  roho ya kicho ni roho ya kumcha Bwana na kupendezwa na maagizo yake Bwana ( Zab.112:1). 

“ Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili;Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa.” Mithali 31:30

Upendo wa macho hudanganya,uzuri wa mtu haupo kwenye macho  wala hauonekani kwa macho ya damu na nyama. Bali uzuri unapimwa ndani ya moyo wake. Lakini hata hivyo uzuri wa nje wa mwanamke ni ubatili. Yaani uzuri hauna maana,wala si kitu cha kuchukuliana nacho bali “ kumcha Bwana ndio kitu chenye maana” unajua ikiwa mwanamke atamcha BWANA basi ndie atakaekuwa bora machoni pa watu na mbele za Mungu. Hii ni sawa na kusema sifa nzuri ya mwanamke haipo katika uzuri aliokuwa nao bali ipo katika roho ya kicho.

Tumeona wengi wakilia kwenye ndoa zao na wakisema wake zao si wazuri,lakini ndio hao hao waliokuwa wakisema wake zao ni wazuri,sasa jiulize ni kitu gani kinachowafanya kulia sasa,maana kama wake zao ni wale wale? Hapo ndipo utakapoliamini neno hili “ Mwanamke amchaye BWANA,ndiye atakayesifiwa” sifa hii ni sifa ya mwanamke wa Mithali 31. Uzuri wa mwanamke au uchangamfu wake bila Mungu ni bure,maana uzuri sio wa milele. Mungu anamtafuta mwanamke mwabudu halisi na mwenye hofu naye,huyo atainuliwa.Leo hii tujifunze sifa moja ya mwanamke wa mithali 31,sifa yenyewe ni ile ya kiroho. 

01. Mwanamke mwenye sheria ya wema ulimini mwake;

“Hufumbua kinywa chake kwa hekima,Na sheria ya wema i katika ulimi wake.” Mithali 31:26

Biblia inasema mwanamke huyu,hufumbua kinywa chake ujuzi(busara ya kawaida) pamoja hekima ya Kiungu (skillful and godly Wisdom) na katika ulimi wake inatoka sheria ya wema wenye upole wema wa kuelekeza. Unajua ni mwanamke gani anayezungumziwa hapo? Si mwingine bali ni yule aliyelijaza neno la Bwana katika hekima yote,na ndio maana ulimini mwake sheria au maongozo ya kum- counsel mtu yanatoka.

Utagundua sifa mojawapo ya uzuri wa mwanamke ni yule aliyekuwa amesheheni uwepo wa Mungu akiwa na Neno ambapo kwa Neno aweza kutoa hekima na maarifa ya Kiungu.

Si mapenzi ya Mungu kwa mwanamke kutumia kinywa chake vibaya kwa kusengenya au katika uongo,au mambo ya umbea umbea hivi! Bali Ni mapenzi ya Mungu kumtazama mwanamke mwenye kuweza kuutawala mdomo wake. Na iko hivi; huwezi kutawala kinywa ikiwa ndani ya kinywa (moyoni)kumejaa hila. Bali ndani yako kukiwa na neno la Bwana,basi kinywa nacho kitatiishwa hata sheria ya Bwana itatoka kwako. 

“Sheria ya wema” ni yale maneno mazuri yenye maongozo,mafunzo,elimu ya namna ya ajabu. Mwanamke mwenye sheria ya wema ulimini mwake ni zaidi ya mwalimu,naye ni zaidi ya mwanamke wa kawaida. Watu wanapenda kumsikiliza maana ndani yake huyo mwanamke kuna Neno la Bwana,hivyo asemapo ni kana kwamba Yesu Kristo mwenyewe akisema. Hivi umeshawahi kukutana na mwanamke wa namna hii? Yaani huchoki kumsikiliza,!!!😀😂

Mimi sijui wewe unaishi wapi na umezungukwa na akina nani hapo unapoishi. Ila najua awapo mwanamke wa mithali 31 utaelewa haya niyasemayo. Lakini ni mbaya kama nini uwe na wanawake wasio mcha Mungu,maana ndani yao hakuna jambo jema hata moja. Mwanamke afumbuaye kinywa chake kwa hekima,neno baya halitoki kwake,lah! Likitoka mara moja hujishusha na kuomba msamaha. 

Hii ndio sifa nzuri ya kwanza ya mwanamke mzuri. Hata kama wewe ni mwanaume usiyeoa bado ni lazima uvutiwe na mwanamke wa namna hii. Au hata kama wewe ni mwanamke mwenzako,unatamani mwanamke wa namna hii awe rafiki wako,ili aweze kukupa neno la hekima,mashauri na mengineyo maana wanawake wapo na mambo mengi. Unajua,ukweli ni kwamba mwanamke mmoja akielimika ni sawa na kuielimisha jamii. Hata katika ndoa,mwanamke akiwa ni mwanamke kama huyu wa mithali basi ujue ndoa itakuwa ni ndoa imara na kamwe shetani hana nafasi ya kufanikiwa kuangusha ndoa!!!

Leo kwenye ndoa ni vilio vimezidi kuliko furaha. Unajua shida kubwa ipo wapi? Shida mojawapo kubwa ipo kwa mwanamke ambaye alitazamiwa awe mlinzi wa kiroho wa mumewe na familia kwa ujumla lakini mwanamke amejisahau au hajui wajibu wake kiroho. Mwanamke akiwa na sifa  za mwanamke wa mithali 31,shetani atatokea wapi aipige ndoa yako? Umeshawahi kutafakari hilo kwamba,ikiwa mwanamke ukisimama vyema na Mungu shetani hana nafasi kabisa!

Sasa,nini cha kufanya kwako mwanamke

Tafuta sana ukaribu na Mungu wako kwanza kwa kuokoka ikiwa kama hujaokoka bado. Lakini jaribu sana kujijenga kwenye misingi ya neno na maombi ukiomba Mungu akufanye uwe kama mwanamke wa mithali 31. Na inawezekana ukatembea na Mungu kwenye viwango vya juu hata ukaiokoa ndoa yako. Waweza kunipigia pia kwa namba zangu zilizopo hapo chini;

ITAENDELEA….

Kwa msaada zaidi,na maombezi nipigie kwa simu+255 683 877 900

Namba ya what’s app ni +255 746 446 446

Mchungaji Gasper Madumla.

UBARIKIWE.

Comentários


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page