top of page

MWANAMKE MSHUNAMI~ 01

Bwana Yesu asifiwe…

Wanawake kutoka shunami ni wachache wanaotajwa. Kwa mfano yupo mwanamwali Abishagi Mshunami binti mzuri, kuliko wote mipakani mwote mwa Israeli kipindi cha uzee wa Daudi aliyetafutwa ili kumpa joto mzee Daudi ( 1 Wafalme 1:3,15,2:17). Lakini pia yupo mwanamke Mshunami mwingine kwenye kipindi cha Elisha,mwanamke aliyekuwa na cheo aliyekuwa akiishi pamoja na mumewe,ambaye Elisha alimfufua mwanaye. Hata hiyo jina la mwanamke huyu halifahamiki,hapo baadae alifiwa na mumewe na kuwa mjane. Katika kipindi cha njaa,Elisha alimtahadharisha kwamba akimbilie kwenye nchi ya ugenini ,( 2 Wafalme 8:1-6). Hata hivyo hatuna habari zake nyingi.

  1. Sasa,kufuatana na 2 Wafalme 4:8-37,ndipo fundisho hili limeegama.

“ Hata ikawa siku moja, Elisha alikwenda Shunemu; na huko kulikuwa na mwanamke mmoja mwenye cheo; naye akamshurutisha aje ale chakula. Ikawa kila alipopita njia ile, huingia kula chakula. Yule mwanamke akamwambia mumewe, Tazama, mimi naona ya kuwa mtu huyu apitaye kwetu mara kwa mara ni mtu mtakatifu wa Mungu. “ ( 8-9)

01. Ukarimu.

Hili ndilo jambo la kwanza la kujifunza kutoka kwa Mshunami. Alipomwona Elisha alitamani,Elisha asimame na ale ndipo aendelee na safari yake. Tendo hili la kumpa chakula mtu wa Mungu ni tendo la ukarimu,biblia inasema hapo,Elisha alipita mara kwa mara na kujikuta akisimama hapo na kula. Najiuliza ni wanawake wangapi leo ambao wanaweza wakawa na ukarimu kama wa huyu Mshunami? Ukarimu ni moyo wa kujali/kuhudumia mtu/watu pasipo malipo kwa maana unaweza ukamkirimu mtu na ukaishia kutukanwa!!!

Ndio maana ni suala la moyo. Bila shaka huyu,mwanamke alikuwa na moyo wa ukarimu kwa maana alimpokea mgeni na kumhudumia bila kushurutishwa na mumewe au yeyote. Ebu jiulize ni mara ngapi wageni wanapita kwako nje ya nyumba yako,hali wakiwa na njaa maana mwenye njaa haitaji kujitambulisha bali anaonekana tu! Mbona unawaacha?

02. Nguvu ya kutambua watumishi wa Mungu.

“…Tazama, mimi naona ya kuwa mtu huyu apitaye kwetu mara kwa mara ni mtu mtakatifu wa Mungu.” Swali la kujiuliza,kwani Elisha alikuwa akionekana vipi hata Mshunami akamtambua? Imekuwaje mumewe asimtambue Elisha kwa haraka isipokuwa mkewe ndiye aliyemtambua? Inawezekana mumewe alimtambua lakini alimpuuzia,hakuona umuhimu wowote wa kumjali. Hujawahi kumwona mtu anamwona mtumishi kaja kwake,halafu hana time naye,sana sana husema moyoni mwake“so what!!! Aseme alilolijia na aende zake!!!” lakini haikuwa hivyo kwa mwanamke Mshunami. Alimwona Elisha kuwa ni mtumishi wa Mungu, mtu mtakatifu.

Haya leo,ni mara ngapi unapishana na mtumishi wa Mungu pasipo kumtambua? Haina maana kila anayepita kwako umtambue,lakini ni vyema ukawa na macho ya kuona…

ITAENDELEA…

Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe na kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga kwa+255 683 877 900

Whatsapp +255 746 446 446

Na Mch.G.Madumla.

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page