top of page

MWANA-KONDOO ASIYEKUWA NA ILA

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi,

Kitabu cha Kutoka 12 yote inazungumzia mambo makubwa mawili,“Pasaka/ukombozi na mikate isiyochachwa ( The Passover and the Festival of Unleavened Bread) ” . Moja kati ya maelekezo muhimu waliyopewa Waisraeli walipokuwa wakijiandaa kutoka utumwani Misri,ilikuwa ni kumchinja pasaka/Mwana-Kondoo mume wa mwaka mmoja “asiyekuwa na ila” – Kutoka 12:5. Neno “ila” ni “dosari / upungufu“,Hivyo;Bwana aliwataka Israeli wamtoe Mwana-Kondoo asiyekuwa kilema,au ulemavu wowote ule,na kwa sababu hiyo,aliwapa muda wa kutosha wa kukagua Kondoo,ili pasiwe na makosa yeyote ya kuchanganya katika utoaji.

  1. Ufunuo uliopo hapo;

Mwana-Kondoo alipitishwa kwa makuhani,kuthibitisha kama kweli ana dosari au la. Na ikiwa atagundulika na dosari/ila yoyote ile ( dosari kama ulemavu au labda akiwa na ugonjwa) basi huyo hatafaa kutumika. Zoezi hili la ukaguzi lilikuwa likifanywa kwa umakini sana,kwa ngazi moja hadi nyingine. Hawakupaswa kumchukua Mwana-Kondoo mweye umri mdogo sana kama wa miezi,wala huyo Mwana-Kondoo asiwe mzee sana,bali awe mwenye umri mzuri wa kati kati,(Ili kusudi awe wa thamani sana)

Mwana-Kondoo huyo alikuwa ni kivuli cha Kristo ( 1Wakorintho5:7). Kwa maana, Kristo Yesu, ndiye haswa aliyeandikiwa. Yeye ndiye Mwana-Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu ( Yoh.1:29). Kristo Yesu alipokamatwa ili asurubiwe,kwa mujibu wa injili zote. Alipelekwa makuhani tofauti tofauti. Kwa mujibu wa kitabu cha Mathayo,alipokamatwa kwanza alipelekwa kwa kuhani mkuu,Kayafa na hapo jopo la waandishi na wazee walikuwa wamekusanyika hapo ( Mathayo 26:57). Lakini hata hivyo, Kayafa hakuona hatia/dosari lolote lile kwa Yesu ijapokuwa kulikuwa na watu waliojipanga kusema uongo juu yake.

Kuhani mkuu alimkagua Yesu na kuona kwamba hakuna dosari yoyote kwake,kisha akampeleka kwa Liwali mmoja aitwae Pilato ( Mathayo 27:2), Yesu akiwa kwa Pilato kwa maneno mengi ya uongo aliyosemewa juu yake,mkewe Pilato akateswa sana katika ndoto juu ya Yesu, haki ilionekana kwake Yesu wala dosari/ila haikuoneka ( Mathayo 27:19). Hata hivyo Pilato naye akamkagua,na mwishoe naye,hakuona “ila au dosari ” yoyote kwa maana Kristo, ndiye Mwana-Kondoo asiyekua na ila.

Kama ilivyo kule kwa Mwana-Kondoo kipindi cha pasaka ya kwanza,asiyekuwa na ila,jinsi alivyokaguliwa na makuhani ili kuwa sadaka ya ukombozi kwa Israeli,ndivyo ilivyo kwa Yesu hana ila,mpatanishi kwa njia ya damu yake ( Warumi 3:23-25). Hivyo; makuhani wote walimpitisha Yesu / Mwana-Kondoo kutafuta ila yoyote, hawakuona,naye Yesu damu yake ikamwagika kwa ajili ya wengi.Kumbuka tena,Mwana-Kondoo aliyechinjwa alikuwa mume wa mwaka mmoja, si mzee. Yesu naye miaka 33 aliyotumia katika mwili,hakuwa mzee bali ni kijana na mtu wa makamu,kuonesha damu yake inathamani sana.

Mwana-Kondoo asiyekuwa na ila,alikuwa akizungumziwa Kristo hasa,Yeye aliyekukomboa kwa kumwamini tu kwa kuthibitisha ukiri wako kwake. Ni vyema kufahamu kuwa Kristo alichubuliwa,alijeruhiwa kwa ajili yako ( Isaya 53:5),pasipo kosa wala dhambi ya aina yoyote ile kwa sababu Yeye ni Mwana-Kondoo asiye na ila. Huu ni upendo wa namna gani,mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya mwingine! Ni vyema, ukajingamanisha na Kristo leo,kwa kumpokea kwa imani tu,tunapoomba kwa pamoja.

Ikiwa umebarikiwa na ujumbe huu,basi nifahamishe tupate kumtukuza Mungu pamoja. Lakini inawezekana labda unahitaji MAOMBI kwa maana nawe unapitia changamoto hii,Basi kwa yote nipigie sasa kwa + 255 683 877 900

What’s app namba ni+255 746 446 446  (Jiunge pia na kundi la UJUMBE WA LEO kwa kutuma neno NIUNGE katika what’s app kwa namba hiyo hiyo)

Na Mch.G.Madumla.

UBARIKIWE.

Comentarios


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page