top of page

DAMU KWENYE KIZINGITI CHA JUU. – 01


Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi,

“Damu na kizingiti cha juu” ni ujumbe wa ukombozi uliofanyika kwa damu ya Mwana-kondoo wa Mungu,Yaani Kristo (1 Wakorintho 5:7). Lakini leo tunaangazia haswa ufunuo wa kutia damu kwenye miimo miwili  na katika kizingiti cha juu katika nyumba za Waisraeli. Kwa nini waliambiwa wapake damu juu ya milango yao,na isiwe mahali pengine popote pale? Ni kweli ilikuwa ni kwa sababu wahepukane na pigo,walindwe,lakini kwa nini iwe juu ya kizingiti cha mlango? si wangeliweza kupaka hata ukutani,maana bado damu ingelikuwa ni damu ile ile.

Biblia inasemaje?“ Nao watatwaa baadhi ya damu yake na kuitia katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu, katika zile nyumba watakazomla.” Kutoka 12:7,soma pia Kutoka 12:22. Kwa mujibu wa maelekezo hayo ya Mungu kwa kinywa cha Musa na Haruni,yafuatayo ni mtaji wa kujifunza;

  1. Ulinzi.

Biblia inasema Bwana atakapopita juu /(passover),ya nyumba watakamokuwemo watu wake wa Israeli,hapo hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwa Waisraeli na kuwaharibu kwa sababu ya uwepo wa Damu ya Mwana-kondoo iliyopakwa kizingitini (Kutoka 12:23).Hii ina maana kuwa, Damu iliyopakwa imefanyika ulinzi dhidi ya mwenye kuharibu,(Kupaka damu kwenye nyumba ni kitendo cha kufunika nyumba dhidi ya uharibifu).Mlinzi mzuri ni yule anayewekwa mlangoni mwa jengo au nyumba kwa maana hapo ndipo mwivi huingia.Kwenye malngo watu huweka ulinzi wa mageti makubwa,kamera,mbwa,walinzi,n.k Kwa lengo la kulinda kile kilicho ndani.Na lazima kile kinacholindwa kiwe na thamani,( kwa maana huwezi kulinda kisicho na thamani). Hivyo damu ya Mwana-kondoo imepakwa “mlangoni” Kuwakilisha “ulinzi”

  1. Utambulisho

Katika andiko hilo (Kutoka 12:7),Biblia inawataka watu wa Mungu wapake damu “juu ya kizingiti cha milango” . Bila shaka damu waliyopaka ilikuwa inaonekana wazi sana,kwa maana ukisogeoa kwenye nyumba ya mwisraeli huna sababu ya kuuliza uliza,hii ni nyumba ya nani?,bali utatambua tu ni nyumba ya mwisraeli kwa sababu damu inamtambulisha aliyopo ndani ya nyumba. Damu ya Mwana-kondoo iliwatambulisha mbali na Wamisri,na wao Wisraeli walijijua utofauti waliokuwa nao. Utambulisho huo huo ndio unaofanyika hata sasa! Lakini kitu cha ajabu leo kuna shida sana!!!! Kwa maana leo imefika wakati imekuwa ni vigumu kumtambua mtu aliyeokoka na yule asiyeokoka,kwa sababu kama kuvaa wanafanana,kama kucheza miziki wanafanana,kuongea wanafanana! Ni ajabu sana leo na wokovu tulionao!!! Lakini,Lengo la Damu ya Mwana-Kondoo ilikuwa ni kuwatofautisha watu wa Mungu na wa mataifa.!

  1. Utii.

BWANA alikuwa akiwafundisha utii watu wake. Wale tu waliotembea kwenye maelekezo yake,waliokoka siku ile na wasiotii waliangamia moja kwa moja. Maelekezo yaliwataka wapake Damu kwenye sehemu za juu za vizingiti vya milango ya nyumba zao,lakini sehemu nyingine zozote zile kwenye nyumba wasipake! Katika hali ya kawaida kabisa,asiyetii hivyo ni lazima atakwenda kupaka hadi chooni,atapaka uwani,kinyume na maelekezo. Wasiotii kuangamia ni sehemu yao hata kama damu ilikuwepo lakini,kama hasingelitii mtu angeliangamia. Leo,hata kama upo na Yesu,lakini kama hutafuata kile unachoelekezwa naye,utapotea tu. Lakini pia,Bwana aliwaagiza wasitoke ndani (wabakie ndani kila mmoja),Ilikuwa kama mmoja angelitoka nje basi angelipigwa kama mmoja wapo wa Mmisri, kwa sababu ya kutokutii kwake.

  1. Imani.

Fikiria wewe ndio mmoja kati ya Waisraeli,kisha jiweke kwenye tukio hilo. Na gafla unaambiwa leo usiku BWANA atapita atawapiga jirani zetu Wamisri halafu baada ya hapo unaambiwa kwamba,ili usipatwe na pigo hilo,paka damu ya Mwana-Kondoo tu,kisha tulia ndani. Wakati huo nyumba yako unapoiangalia unagundua kunasehemu haijazibwa vizuri,ukuta wake haupo imara. Hivi ungeliweza kuamini kirahisi rahisi,?Au ungeanza kufanya ukarabati wa kujenga uzio,au kujenga na uzio? Bila shaka haikuwa ni rahisi,kama wasingelikuwa na imani. Mungu alikuwa akiwafundisha kwamba;Ni Damu tu ya Mwana-Kondoo ndio ulinzi pekee. Hata sasa huna haja ya kujenga ukuta kwa ulinzi wa Roho yako,bali kwa damu pekee yatosha kukulinda. Lakini Je unaamini hayo? Suala lipo hasa kwenye kuamini!!! Kumbuka unapoiamini Damu ya Yesu,hiyo tu yatosha kulinda mali zako,biashara zako,familia yako,huduma yako,watu wako n.k

ITAENDELEA…

Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe na kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga kwa+255 683 877 900

Whatsapp +255 746 446 446

Na Mch.G.Madumla.

UBARIKIWE.

Komentarze


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page