top of page

MUNGU AKISEMA,AMETENDA.

Updated: Sep 2, 2022

Kwa ufupi,


Yeye ndio maana ni Mungu,neno lake ni amini na kweli, likiachiliwa,haliwezi kurudi bure bali ni lazima litatimiza mapenzi yake ( Isaya 55:10-11). Hii ni sawa na kusema kwamba katika kila katika Neno la Mungu, limebeba mapenzi yake na likitoka katika kinywa chake,ujue limekwisha tenda tayari. Ndio maana tunaona katika uumbaji, biblia inasema,“ Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.” Mwanzo 1:3 .


Nuru ilikuwa ndani yake,aliposema tu,mara moja bila muda/ within no time! Nuru ikawa. Hiyo ndio sifa ya Bwana MUNGU tunaemwabudu. Tofauti iliyopo kati yetu na Mungu tunayemtumikia ni kwamba, Yeye hutenda pale atamkapo,yaani utiisho wa Neno lake ni utendaji kazi wake,wakati sisi waamini tunahitaji muda wa kutendeka kwa kile tunachokitaka,kwa maana hatutendi sisi isipokuwa ni Yeye ndiye atendaye.


Yesu naye alikuwa sawa na Baba,kwa maana akisema,ametenda. Katika miujiza yake yote,pale aliposema,kilitendeka kitu saa ile ile,ebu angalia pale alipoituliza dhoruba,gafla dhoruba ilitulia saa ile ile,bahari ikatulia ikiwa shwari kuu kwa maana yeye ndio mtuliza dhoruba,kiburi cha bahari hakina nguvu kwake ( Zab.89: 9).


Kumbuka ya kwamba Yesu ingawa alikuwa ni Mungu 100 asilimia,lakini alikuwa mwana wa Mungu vile vile. Ikiwa kama alikuwa ni mwana wa Mungu, basi kile alichokitenda ndicho alichokitenda Mungu ( Yoh.5:19). Hivyo wewe pia ni mwana wa Mungu vile vile (ikiwa kama umeokoka).


Hii ina maana Neno unalolitamka linapaswa liwe na nguvu ya kusababisha athari katika ulimwengu wa roho,lakini pia; yadhihilike katika ulimwengu wa mwili.

Najifunza kitu katika hili,kwamba pale Mungu anaposema nimekubariki,basi ujue ni tayari ametenda nawe umekwisha barikiwa. Akisema nitakuokoa na mabaya ( Isaya 43:2),ujue wokovu tayari umekwishaachiliwa! Anaposema Yeye hatakuacha kabisa wala kukupungukia,ujue amini amekwisha tenda hivyo ( Waebrania 13:5c).


Hivyo kila ahadi yake,ni ametenda tayari ndani ya ahadi hiyo. Shida inakuwa kwako tu,namna ya kupokea ahadi hizo. Unajua hata “uponyaji” umekwisha achiliwa kwa damu ya Yesu pale msalabani? Pale aliposema “kwa kupigwa kwake,sisi tumepona” Isaya 53:5. Alipotamka “uponyaji” hapo ni amekwisha tenda tayari. Hivyo unapoomba,ni sawa na kuvuta uponyaji huo ulioachiliwa tayari, na ndio maana kuomba ni lazima kwa maana Yeye amekwishafanya yote kwa ajili yako,amini tu na utapokea.


Hivyo,tunajifunza kwamba; katika kila Neno la Mungu, ni tayari ametenda. Pia katika ahadi yake,tayari ametenda. Kazi iliyopo si kwake bali ni kwako namna ya kujiunganisha naye katika kile kilichotendwa tayari. Kweli ya biblia inaeeleza ukamilifu wake,Yeye BWANA ni mkamilifu sana,kuliko tunavyofikiri. Neno lake limebeba utendaji kazi tayari katika mazingira yote unayoyapitia,na ndio maana katika kila mazingira kuna Neno lake maalumu,hii yote ni kuonesha hakuna mazingira ambayo BWANA hakusema,tena hakutenda.


Jaribu kusoma kwa ukaribu sana maisha ya vijana wanne ambao ni Danieli na wenzake. Biblia inatueleza namna ambavyo Neno la wakati linavyofanya kazi. Utagundua pale ambapo Danieli alipokuwa kwenye mazingira magumu,mazingira ya kuuwawa Neno lilileta ukombozi kwake,( yani Kulikuwa tayari na uzima).


Neno la Mungu likamtoa kwenye maangamizo kwa maana, Yeye akisema, ametenda tayari! Wewe je,upo kwenye mazingira gani hivi sasa? Je unajua katika mazingira hayo hayo, Mungu hajakaa kimya?


Ndio,lipo Neno lake,na Neno lake ni utendaji kazi tayari! Unanielewa lakini? I wish/ natamani uelewe kile ninachokielewa sasa. (Maana ni vigumu sana kikielezea kwa maandishi machache.)

Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe na kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga kwa+255 683 877 900


Whatsapp +255 746 446 446


Na Mch.G.Madumla.


UBARIKIWE

Comentarios


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page