MUKTASARI WA VITABU 66 VYA BIBLIA ~ 02 ( tamati)
- Mch. Gasper Madumla
- Oct 22, 2019
- 3 min read
Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi,
Agano jipya ( 27)
A) Injili ( Biographical books)
Mathayo – Kwa Wayahudi, Yesu anaelezwa kuwa ni masihi mfalme. ( Mwandishi ni mmoja wa mitume 12 wa Yesu)
Marko – Mwandishi ni Yohana Marko. Anasisitiza hasa kuhusu nguvu za ajabu alizonazo Kristo dhidi ya magonjwa,mapepo/ (Christ is explained to have the supernatural power over nature, diseases and demons)
Luka – Anaeleza kuwa Yesu ni Mwana wa Adamu mwenye huruma na rehema kwa ajili ya watenda dhambi na maskini.
Yohana – anamweleza Yesu kuwa ni mwana wa Mungu na kinaeleza mafundisho ya Kristo kiundani sana/katika mafunuo/ kiroho zaidi. Maneno mawili “ imani na uzima wa milele” yakisisitizwa karibu kitabu kizima.
B) Kitabu cha histori ya matendo ya mitume. – Mwandishi ni “Luka” picha halisi ni kuanza na kukua kwa kanisa la kwanza kuanzia kupaa kwa Kristo mpaka kufungwa kwa Paulo huko Rumi.
C) Nyaraka 13 za Paulo mtume.
Warumi – Kwa wakristo huko Rumi.Injili ya Mungu iletayo Wokovu kwa watu wote,ndio mkazo mkubwa.
1 Wakorintho – Kwa kanisa la Korintho,lengo mama ni usafi wa kanisa kutoka kwenye matendo maovu pamoja na msingi wa mafundisho.
2 Wakorintho – inaangazi hasa tabia za huduma ya kitume pamoja na neema ya utume / Characteristics of an apostolic ministry and vindication of Paul’s apostleship.
Wagalatia – ulinzi wa mamlaka ya kiutume na mafundisho ya kuhesabiwa haki kwa imani na kuwaonya walimu wa uongo
Waefeso – mpango wa utukufu wa wokovu mkazo mkubwa ni kwamba vikwazo vyote kati ya Wayahudi na wamataifa vimekwisha kuvunjwa ikiwa mtu akiwa ndani ya Kristo.
Wafilipi – Wazo kuu ni furaha,Paulo anawaandikia kanisa yeye akiwa kifungoni na wadumishe upendo. Neno “furaha” limeandikwa mara kumi na sita.
Wakolosai – utukufu mkuu wa Kristo kama kichwa cha kanisa na kwa sababu hiyo wakristo hawahitajiki kurudi nyuma kwenye upagani.
1 Wathesalonike – Kwa ajili ya wongofu wapya waliokuwa katika mateso, Paulo akaandika kama moja ya kuwafariji,kuwashauri.
2 Wathesalonike – Kurudi kwa Kristo kwa maana Wathesalonike walisongwa na maswali juu ya kurudi kwa Kristo.
1 Timotheo – nyaraka ya kichungaji ,ushauri makini kwa mchungaji kijana kuhusu mwenendo na kazi ya kihuduma.
2 Timotheo – Ni nyaraka ya mwisho ya Paulo aliandika kwa ufupi kabla ya kifo chake na kumkanseli Timotheo kuhusu kijana mwema katika imani.
Tito – Ni nyaraka ya kichungaji,ni barua ya kimwongozo katika huduma. Paulo alikuwa akimpa mwongozo Tito mshirika wake katika huduma. Ni moja ya barua za kichungaji.
Filemoni – lengo mama ni “msamaha” Paulo anamtaka Filemoni ampokee Onesmoa na kumsamehe
D) Nyaraka nyingine / general letters
Waebrania – Kuwatia moyo wakristo wa kiebrania waliokosa msimamo kwamba Yesu Kristo ndio utimilifu wa agano la kale,yeye ni mkuu kuliko taratibu zote za kale. Wakristo wawe ni mashujaa wa imani. Pia kinamweleza Kristo kama mpatanishi wa neema ya Mungu.
Yakobo – ndugu yake Yesu ndiye labda ni mwandishi. Mada kuu ni matendo mema na Imani yenye kufanya kazi.
1 Petro – Maelezo ya maisha matakatifu kwa wale wanaopitia mateso.
2 Petro – Namna ya kushughulika na walimu wa uongo na waovu waliojichanganya na kanisa.
1 Yoh.- Kuwahakikishia imani waamini,na kuyakataa mafundisho ya uongo yasemayo kwamba Yesu sio mwanadamu kamili na sio Mungu kamili. Walaka ulilenga waamini wenye level / kiwango tofauti cha imani.
2 Yoh.- (kwa mwanamke mmoja aliyechaguliwa na mtoto wake) kinaeleza kuhusu Ukweli wa kiungu na uovu wa dunia hii. Yohana anaeleza pia habari ya upendo
3 Yoh. – Kwa mpendwa Gayo. Yohana anamtaka Gayo awasaidie walimu wa Neno la Mungu wanaosafiri na kumkemea Diotrefe kwa kukataa kwake kuwakaribisha.
Yuda – Kinaonya kuhusu manabii wa uongo ambao walikuwa wakifundisha kwamba kuokolewa kwa neema kunatoa kibali cha kuendelea kutenda dhambi .
C) Kitabu cha ufunuo / Prophetic book – Kuwatia moyo waaminifu katika imani wasimame imara dhidi ya mateso. Maono yanayoshughulikia matukio ya kiimani/ kiroho. Msuguano/ vita kubwa inayooneshwa ni ile ya kiroho kati ya nguvu za Mungu dhidi za shetani ambapo inaishia na ushindi wa mwanakondoo. Pia kutoa mwanga wa kurejea kwa Kristo kuwaokoa wenye haki na kuhukumu waovu ( And to compromise in the righteous and judge the wicked)
Kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga sasa kwa +255 683 877 900
Whats app +255 746 446 446
Mch.G.Madumla.
UBARIKIWE
Comments