MUKTASARI WA VITABU 66 VYA BIBLIA ~ 01.
- Mch. Gasper Madumla
- Oct 19, 2019
- 3 min read
Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi,
Makala hii ni hazina mama ya kukufanya ujue muktasari wa kila kitabu katika biblia. Labda,makala hii ingelipaswa kuchapwa kisha kuuzwa kwa wakristo wengi zaidi ili kusudi itoe mwanga kwa wasomaji wa biblia. Lakini hata hivyo,wewe unayesoma sasa umepata neema ya kupata hazina hii bure kabisa. Lengo kuu la makala hii ni kukulahisishia kufahamu yaliyomo katika vitabu 66 vya biblia yako. Biblia ni kitabu cha ajabu kwa maana ni kitabu kilichohifadhi “sauti” ya Mungu ndani yake ( 2 Timotheo 3:16). Jambo moja la kukimbuka ni hili; “muundo wa biblia ” biblia imeundwa kwa maagano mawili yaani “agano la kale na agano jipya” na huo ndio muundo wa biblia.
Vitabu vya agano la kale ( 39)
A) Vitabu vya sheria/ Pentateuch books (5 )
Mwanzo/Gen. – Kinazungumzia mwanzo wa kila kitu,mwanzo wa ulimwengu,/ hata mwanzo wa watu waliochaguliwa na Bwana.
Kutoka/Exodus – Ukombozi,na kuanza kwa historia ya taifa la Israeli wakielekea Kanaani chini ya uongozi wake Musa.
Mambo ya Walawi / Leviticus – Kitabu cha sheria kinachotoa taratibu za utakaso,vyakula,ibada. Pia zinatolewa taratibu za sadaka.
Hesabu / Numbers – Kitabu kinachoeleza Israeli akielekea alipokusudiwa kwa miaka 40 Mungu akimfundisha kwa maajabu huko jangwani.
Kumb./Deuteronomy – Kurudiwa kwa sheria na zikatolewa kwa haraka kabla ya kuingia Kanaani.
B)Vitabu vya historia / Historical books ( 12)
Yoshua / Joshua – Kumbukumbu ya ushindi kuingia Kanaani chini ya uongozi wa Yoshua na mgawanyo wa ardhi katikati ya makabila 12
Waamuzi / Judges – Mzunguko wa dhambi na Historia ya kukombolewa kwa ardhi kupitia waamuzi 15.
Ruthu/Ruth – Habari nzuri ya Ruthu chimbuko la Daudi na ukoo wa Yesu.
1,2 Samweli – Historia ya Samweli na miaka ya mwanzo ya utawala wa kifalme Israeli chini ya utawala wa Sauli na Daudi.
1,2 Nyakati / Chronicles – Kumbukumbu kubwa ya utawala wa Daudi,Sulemani,na wafalme wa Yuda mpaka kwenye muda wa utumwa wa babeli.
Ezra – Kumbukumbu ya kurejea kwa Wayahudi kutoka utumwa ( babeli) na kujengwa tena kwa Hekalu.
Nehemia /Nehemiah – Kujengwa tena kwa ukuta wa Yerusalemu na kuanzishwa tena kwa mambo matakatifu.
Esta / Esther – Habari ya ukombozi kupitia malkia Esta wa Kiyahudi na kuanzishwa kwa sikukuu ya Purimu.
C) Vitabu vya mashairi / Poetic books.
Ayubu / Job – Mateso ya mwenye haki
Zaburi /Psalms – Mkusanyiko wa nyimbo 150 kwa ajili ya kusifu na kuabudu.
Mithali / proverbs – Hekima,haki
Mhubiri / Ecclesiastes – Maisha yasiyo na maana bila Mungu / ni ubatili bila Mungu.
Wimbo bora / Song of songs – Pendo la Kristo na Kanisa.
D) Vitabu vya manabii wakubwa / Prophetic books the major prophets
Isaya/Isaiah – Kitabu cha ukombozi/redeption,kitabu kilichojaa nabii za masihi Kristo,Ole juu ya mataifa yenye dhambi.
Yeremia / Jeremiah – Nabii aliaye,aliishi kipindi cha Yosia mpaka kipindi cha utumwa/captivity. Ujumbe ni kurudi nyuma kwa Wayahudi na urejesho wake.
Maombolezo / Lamintations – maombolezo ya Yeremia akieleza habari za huzuni juu ya pendo lake kwa Israeli.
Ezekieli – Hali ya huzuni ya watu wa Mungu na njia ya kuinuliwa kwao baadae na utukufu / a book of striking metaphors vividly portraying the sad condition of God’s people and the way to future exaltation and glory.
Daniel – Maono binafsi yahusuyo matukio ya historia ya kiungu na za kidunia / apocalyptic vision concerning events in both secular and sacred history.
E) Vitabu vya manabii wadogo / minor Prophets (12)
Hosea – uasi wa Israeli unaoelezwa kitabia kama uzinzi wa kiroho. Hosea aambiwa atwae mke wa uzinzi na watoto wa uzinzi, jinsi ajisikiavyo ndivyo uasi wa Israeli unavyomfikia Bwana.
Yoeli /Joel – Ni nabii wa Yuda. Toba ya taifa na baraka. Watu walarue mioyo yao kwa toba.
Amos -mchungaji nabii, jasiri mrekebishaji,kukataa ubinafsi na dhambi. Kitabu kinabeba maono matano
Obadia – Hatma mbaya/ adhabu ya Edomu na kukombolewa kwa mwisho kwa Israeli.
Yona – Simulizi ya huduma ya umisionary uliokataliwa. Simulizi inayoonesha huruma ya Bwana asiyekuwa mwepesi kukasirika
Mika / Micah – tabia za maadili yasiyofaa /mabaya ya Israeli na Yuda,lakini kutabili kwa kuanzisha kwa ufalme wa kimasihi ambapo haki itashinda.
Nahumu – Lengo mama ni uharibifu wa Ninawi. Yuda imepewa ahadi ya kukombolewa kutoka Ashuru.
Habakuki – Kiliandikwa kipindi cha ubabeli. Namna gani Mungu anaweza kuruhusu taifa ovu kudhalilisha Israeli.
Zefania / Zephaniah – matishio lakini yanaishia na maono ya hatma ya utukufu wa Israeli/ Somber in tone,filled with threatenings,but end in a vision of the future glory of Israel.
Hagai – Kemeo kwa watu wazembe / (wasiojali Mungu bali mambo yao ) katika kujenga nyumba ya Bwana, lakini pia aliahidi kurejea kwa utukufu wa Mungu pale nyumba ya Bwana itakapomalizika.
Zekaria / Zechariah – Kuamshwa kwa Wayahudi kujenga tena hekalu na kuna maono 8 na kuna ushindi wa ufalme wa Mungu.
Malaki / Malachi – Maandalizi ya ujio wa Masihi / a graphic picture of closing period of OLD Testament history,and showing the necessity of reforms before the coming of the Messiah.
Kutoka kwenye kumbukumbu za vitabu nisomavyo nimeona nikukusanyie hayo machache katika mpangilio niliofikiri kwamba utakufaa. Hata hivyo makala hii inaendelea. Ni vyema ukajua kwamba katika kila kitabu, Mungu alikuwa akisema na ndivyo asemavyo hata sasa kwako pia.
ITAENDELEA…
Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe tupate kumtukuza Mungu pamoja na kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI, piga kwa +255 683 877 900
Whatsapp namba +255 746 446 446
Mch.G.Madumla
UBARIKIWE.
Comments