top of page

MTAZAMO WA KIBIBLIA KUHUSU MATESO NA BARAKA / SUFFERING & BLESSING.

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa kifupi.

Biblical view of suffering and blessing

Biblia imeeleza kwa undani kuhusu masumbufu / mateso na baraka ( suffering and blessing). Ingawa hakuna mkristo anayependa mateso,bali sote tunapenda baraka na tumesahau kuwa mateso ni sehemu ya ukristo wetu. U mkristo ? Basi huna ujanja wa aina yoyote ya kukwepa kuteseka kwa kwa kuwa Kristo naye aliteseka. Mateso ni kikombe cha kila mtu hata kama umekomaa zaidi kiroho lakini ni lazima ukinywee kikombe hiki. Maana ikiwa akina Paulo walipitishwa wewe u nani?

  1. Mateso,masumbufu / suffering.

Masumbufu ni nini ? ( What is the suffering? )

Masumbufu au mateso /suffering ni kitu au jambo lolote linalokuumiza au kukutesa. ( it is anything that hurts or irritates ). ; Ingawa masumbufu yanachosha sana lakini ni sehemu ya utumishi pia. Mateso au masumbufu yanaweza yakawa ya kiroho au kimwili. Katika biblia tunapozungumzia “suffering “hatuwezi kuacha kuwazungumzia watu kama Ayubu,Paulo,mitume,Yesu. Lakini leo kwa ufupi sana ebu jifunze kitu kwa ;

• Ayubu ( Ayubu 1 &2 )

Biblia inamwelezea Ayubu kuwa ni mtu aliyekuwa mkamilifu na mwelekevu,aliyemcha Mungu na kuepukana na uovu. Hii ni sawa na kusema Ayubu alikuwa amekaza sana kwa Mungu kiasi kwamba hata Mungu alikuwa akijivunia. Leo Mungu anapokuangalia,Je anajivunia kwako? Mimi sijui,ila jiulize. Ayubu aliteseka sana sio kwa sababu alitenda dhambi bali Mungu aliruhusu mateso. Je kwa nini Mungu aruhusu mateso kwa Ayubu?

Mungu alitaka kumwakikishia shetani kwamba Ayubu ni mkamilifu sana,Mungu anajua Ayubu hawezi kumwacha Mungu hata kama atapatwa na nini. Hivyo Mungu hakumjaribu Ayubu bali aliyekuwa akijaribiwa ni shetani. Umepata kitu hapo? Mambo machache unayoweza kujifunza kwake;

  1. Ayubu aliendelea kumwabudu Mungu kipindi cha mateso. ( Ayubu 1:20-21)

  2. Ayubu ingawa aliteseka lakini hakufanya dhambi ( Ayubu 1:22,2:10)

  3. Ayubu hajui chanzo cha mateso yake,Kumbe kulikuwa na mazungumzo kati ya Mungu na shetani.

  4. Je unapopitia mateso, utaendelea kumwabudu Mungu? Au utamwacha?

Nini chanzo cha mateso ? / what are the causes of suffering?

01. Dhambi – Hiki ni chanzo kikubwa kinachotutesa leo. Wengi huteseka kwa magonjwa hata vifo kwa sababu ya dhambi.( Isaya 59:2)

02. Kuipigania imani / because of faith. – wengine huteswa mpaka kufa kwa sababu ya wokovu. Tazama baadhi ya wakristo wanaoishi kwenye nchi za kiarabu namna wanavyoteseka. ( 2 Timotheo 3:12)

03. Ujinga wa kutojua kweli. – Usipoijua kweli ya Mungu,shetani au dunia au watu watakutesa maana utapewa kila kitu ule na utakula,utarushwa huku na huko. Hakuna kitu kibaya kama ujinga. Utavuna ulichopanda ( Wagalatia 6:7-9)

04. Nidhamu ya Mungu / God’s discipline ( Waebrania 12:6,1 Korintho 11:29-32)

  1. Baraka / blessing.

Neno “ baraka ” linahusisha hasa kibali cha Mungu au kukirimiwa kibali cha Mungu. The word of “blessing ” refers to God’s favor or being granted God’s favor. Baraka au neno kubarikiwa limejitokeza zaidi ya mara 600 katika agano la kale na zaidi ya mara 100 kwenye agano jipya. Hata hivyo mkazo mkubwa wa baraka kwenye agano jipya ni baraka katika mtazamo wa kiroho ( spiritual blessing)

Tunapozungumzia baraka lazima tumzungumzie Ibrahimu ambaye ahadi ya baraka zetu zimetajwa kwake ( Wagalatia 3:14). Hii ni kuonesha kwamba suala la baraka ni suala la kiroho. Baraka ambazo Mungu alimwahidi Ibrahimu zimetimilizwa kupitia Yesu Kristo. Na hapo ndipo tunabarikiwa kwa baraka zote za rohoni katika ulimwengu wa roho ndani yake Kristo ( Waefeso 1:3 )

Kumbuka ; kwenye agano jipya baraka za rohoni hutokana na Mungu kwa wale tu walio ndani ya Yesu.( Warumi 4:7-8 ). Lakini hata hivyo,zipo pia na baraka za kiuchumi ( financial blessing) – Wafilipi 4:19.

  1. Je ni kweli wamataifa nao wamebarikiwa?

Swali hili ni tata, kwa maana inategemea muulizaji analenga baraka za namna gani. Lakini ebu labda ujiulize hivyo. Ili kupata ukweli wa kujibu swali namna hii,itakulazimu kurudi nyuma kwanza na kuangalia biblia inasema nini kuhusu kubarikiwa kwa wamataifa.

Awali yoyote neno “ Wamataifa ” lilikuwa na maana ya watu wasiotoka Yuda,au wasio-wa Yuda ( Wayahudi ). Watu hawa walikuwa wemechaguliwa na Mungu kama mfano wa taifa tu. Hivyo dhama ya “ Wamataifa ” ikaja kuashilia watu wa kutoka mataifa mengine na kwa sababu mataifa hayo waliabudu miungu,walikuwa hawana Mungu. Hivyo “ Wamataifa ” likabadilika maana kuashiria watu wasiomjua Mungu au watu wasiokoka. Na ndio maana hiyo hiyo leo hutumika pale tunaposema “ Wamataifa “

Sasa,kwa kuwa Ibrahimu amehusika katika baraka zetu. Ni vyema ukajifunza hili; Mungu alimbariki Isaaka mtoto wa Ibrahimu kama mtoto wa ahadi lakini pia alimbariki Ishamaeli mtoto wa Ibrahimu asiyekuwa wa ahadi na Mungu akasema “Na kwa habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha, nami nitamwongeza sana sana. Atazaa maseyidi kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kuu. “ Mwanzo 17:20

Sote tunafahamu kabisa Ishmaeli kama chanzo cha Wamataifa maana hata hivyo alifukuzwa naye akaenda na kutoka huko kukawa na taifa kubwa tu. Lakini Ishmaeli kama kiongozi alibarikiwa na Mungu mwenyewe.

Hivyo Wamataifa na wao wamepokea sehemu ya baraka kama baraka za kawaida kabisa ambapo tunasema wamepewa “mafanikio ya nje ” wengi huyaona mafanikio yao kama baraka lakini ukweli ni kwamba wanatembea kwa neema na nje ya baraka za Mungu. Sasa,usishtuke kuona watu wa dini wanamiliki mali na fedha. Kwa maana hayo ni mambo ya kawaida kabisa kwa maana la msingi ni baraka za rohoni.

  1. Kubarikiwa ni kukutana na Yesu.

Kila aliyempokea Yesu,hakika.

amebarikiwa kwa baraka zote za rohoni hata kama anaishi kwenye nyumba ya udongo au amepanga kwa sababu baraka ni zaidi ya nyumba na zaidi ya mali tena ni zaidi ya fedha bali baraka halisi ni amani ya moyoni ambayo huletwa na Bwana unapompokea. Watu walio mbali na Yesu hawana amani / furaha hii,na haipatikaniki kwa lolote bali ni kuokoka tu. Sasa hapo utagundua kitu kwamba yeye aliyeokoka ana kitu cha kipekee ambacho asiyeokoka hana. Na hicho ni kibali cha Mungu ( it’s God’s favor) .

Je unaweza kuomba baraka?

Ndio,unaweza kuomba kwa Mungu kubarikiwa kwa maana ni ahadi kwako. Ebu soma neno la;“ Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.” Wafilipi 4:19

Natamani leo tuwasiliane pamoja na maombi. Lakini ikiwa umebarikiwa na fundisho hili nifahamishe pia. Kwa maombezi pia nipigie kwa namba hizi hizi + 255 683 877 900 

WhatsApp ni .+255 746 446 446

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page