top of page

MTAWALA MPYA ASIYEMJUA MWENYE HAKI!

Updated: Sep 2, 2022




Kitabu cha Mwanzo kinaishia  na wana wa Israeli wakiwa Misri pasipo utumwa  (kwa maana utumwa ulikuwa bado hujainuka). Ikumbukwe ya kwamba, Misri ilikuwa ni sehemu yenye ustaarabu pamoja na maendeleo makubwa ukilinganisha na maeneo mengine.  Katika kipindi cha njaa ya miaka saba,Yakobo na wanawe walijikuta wakiwa ndani ya Misri na wakimwinamia Yusufu ambaye alikuwa waziri mkuu. Ndoto za Yusufu zikatimia ( Mwanzo 37:5-11).


Baada ya miaka 430 +, Yusufu alikufa na kizazi chake chote. Hapo ndipo  aliinuka,mfalme mpya asiyemjua Yusufu “ Basi akainuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu.” Kutoka 1:8


Kulikuwa na heshima iliyotolewa kwa Yusufu na ndugu zake baada yake.  Wamisri  walikuwa wakimfahamu Yusufu kwa mchango wake alioutoa kwa taifa zima lakini kitu cha ajabu kilichokuja kutokea kwa mfalme mpya aliyetawala Hapo baadae ni kutomjua Yusufu yaani kutothamini kazi na mchango wa Yusufu.  


Huyu mtawala asiyejali,wala asiyeona umuhimu wa Yusufu alikusudia kuleta mabaya kwa Waebrania. Utawala wake ndio ulikuwa mwanzo wa uchungu na utumwa kwa watoto wa Mungu.  Haukuwa mpango wa Mungu kumwinua mwuaji bali Mungu aliruhusu mtawala mbaya kuinuka ili ajidhihilishe kwa ukuu na uweza wake kwa kuwaatoa Israeli utumwani.

  1. Mtawala mpya mwovu,ameruhusiwa kwako.

Chokochoko za mtawala mpya za kuwatumikisha Israeli, ziliwafanya Israeli kumgeukia Mungu na kumlilia ( kwa maana walifanyishwa kazi ngumu na za mateso),walikosa msaada mwingine isipokuwa Mungu . Kuna wakati hata wewe utainukiwa na mtu aliye juu yako,mwenye lengo baya na ovu  la kukuangusha,lakini ujue hapo ndipo mahali pa kupaza sauti yako kwa Bwana huku ukiamini mkono wa Bwana utakaokutoa. 


Mwenye haki anapotawala,taifa huinuka.  Kwa maana haki uinua taifa.  Yusufu ni mmoja ya mfano mzuri. Lakini kwa makusudi huyu mtawala mpya hakutaka kumjua. Kuna wakati ambayo hawatamjua huyo ambaye Leo mnamtegemea,wakati huo ukifika huyo mwenye haki anayekusaidia atakwenda zake na hakutakuwa na msaada wake tena hata ukiwaambia watu ya kwamba wewe ni mtoto wa yeye aliyekuwa mzuri /mwenye haki, mwenye nguvu n.k Haitasaidia 😢😢😢


  1. Kama Yusufu angelitawala miaka na karne nyingi,Israeli ingelikuwa chukizo kwa Bwana.  !!!


Ebu fikiria  yule unayemtegemea akawepo siku zote akikusaidia,Jean utaweza kumtegemea Mungu?  Jeshi hautabweteka kweli?  Bila shaka hutaweza hata kumwomba Mungu kwa sababu Yusufu wako unayemtegemea akulishe yupo akikusaidia, lakini akiondoka ndipo utajifunza kumtegemea Mungu.  


Na hali ndivyo ilivyokuwa kwa Israeli. Waliendelea kulishwa na Yusufu. Mtawala mpya na mwovu alipoinuka aliwachangamsha akili kwa kizazi kilichokuwepo.  Mimi najaribu kufikiria pale Waisraeli wanamwambia mtawala mpya “ sisi tu ndugu wa uzao wa Yusufu, tunaomba utufikirie japo kidogo na utupatie nafasi ya heshima kidogo. ..


halafu mtawala mpya anasema “ebu toeni upuuzi wenu! !! Yusufu ndio nani! !,mmejawa na uvivu tu, na bado,mtafanya kazi mpaka mtakoma! !!😠😠😠”. Hivyo hakuna tena kumbukumbu ya mwenye haki kwa mtawala mbaya namna hii.


Ingawa mwenye haki Yusufu, alitenda mema kuokoa taifa kwenye njaa,lakini amesahaulika.  Unajifunza nini  hapo?  Jambo kubwa la kujifunza ni kwamba, kuna “ kipindi cha kusahaulika “kipo  tu! Hata kama utatenda jema kiasi gani lakini hautakumbukwa kwa muda fulani! Sasa isikutishe jambo hili


 pale linapokutokea,bali kumbuka hata Yusufu alisahauliwa! Lakini ajapokusahau mwanadamu, Mungu hawezi kukusahau ( Isaya 49:14-15).

Ikiwa u me Barikiw,nifahamishe. Kwa huduma ya MAOMBI  piga kwa namba hizi hizi;

+255 683 877 900

What’s namba .+255 746 446 446


Na  Mch. G.Madumla 


UBARIKIWE. 

Comentarios


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page