top of page

MPENDE JIRANI YAKO – 01.


Camera360_2014_10_8_071136_jpg

Mch. Gasper Madumla.


Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi,

Mtiahani mkubwa upo katika “kupenda” na hasa kumpenda jirani. Na mtiahani huu kamwe huwezi kufauru ikiwa kama humpendi Mungu kwanza,kwa maana kumpenda jirani yako ni matokeo ya kumpenda Mungu. Katika “kupenda” kuna gharama kubwa hata kupoteza uhai kwa ajili ya kupenda. Leo tunapotafakari kuhusu “kumpenda jirani yako” ni vyema tukajiuliza swali hili “jirani yako ni nani?”.

Jirani yako ni yeyote aliyekaribu nawe. Sasa,upo na nani aliyekaribu yako?. Lakini biblia inapanua wigo mkubwa wa maana hii ya jirani katika kisa alichosimulia Yesu katika Luka 10:25-37. Yesua kifumbua jibu la jirani yako ni nani,kwa maana katika kisa hiki anaeleza kuwa Jirani yako ni zaidi ya yule aliyekaribu nawe bali jirani yako ni yeyote awezaye “ kukujali na kukusaidia ” bila kujali umbali uliyenaye. Kwa maana yule aliyemwonea huruma yule ndugu aliyejeruhiwa,huyo ndiye hasa jirani. Sasa ukiangalia katika hali ya kawaida kuhusu jirani kwa mfano huo,utagundua kwamba jirani alitakiwa kuwa Kuhani na Mlawi ambao wanaukaribu na myahudi aliyeangukia kwa wanyanganyi,lakini hali haikuwa hivyo,bali Msamalia aliyekuwa mbali kimahusiano ndiye aliyekuwa ni jirani ya Myahudi. Hii yote ni kuonesha jirani ni yule mwenye kutoa msaada kwako.

Pamoja na hilo,Neno linakutaka yule aliyekaribu na wewe,umpende,na yule aliye mbali naye umpende. Jirani yako umpende ili kusudi kwa pendo hilo,upate kumtangaza Yesu Kristo. Ni agizo kabisa la kumpenda jirani yako sawa sawa na yale aliyoyanena Yesu katika Yoh.13:34. Lakini Neno halikuishia hapo,linaendelea kusema “umpende na adui/anaeyekuudhi” – Mathayo 5:43-48. Ukitafakari kuhusu hili,utagundua kwamba Yesu alikuwa anajua mioyo yetu kwamba ni mioyo isiyokuwa na pendo. Tunashida sana katika eneo hili,na ndio maana akasema “mpendane” (Yoh13:34),kama tusingelikuwa na shida ya kushindwa kupenda basi asingelisema hivyo. Leo imekuwa ni shida katika eneo hili kwa maana hatupendani kabisa,picha hii inatuonesha jinsi gani hatumpendi Mungu pia.

  1. Je inawezekana kumpenda jirani yako,?

Ndio inawezekana kumpenda huyo jirani yako,tena hata kumpenda anayekuudhi na kumwombea mema tu. Inawezekana kumhurumia anayekutesa,na kuamua kumpenda katikati ya mateso ya kila siku,jifunze kwa Yesu ambaye katika hali ya mateso yetu,hali ya kufarakana naye na kumkataa tena mbaya zaidi na kumnenea kwa mabaya,lakini bado Pendo lake kwako na kwangu halikupungua hata sasa,anatupenda upeo. Yeye ni Mungu,lakini pendo hilo amekwisha limimina kwako. Kumbuka ; hata wewe waweza kumpenda jirani yako,anza mazoezi ya taratibu taratibu ya kumpenda na kumwombea na hatimaye kupitia wewe huyo jirani aje kumjua Yesu,na aokoke.

ITAENDELEA…

Ikiwa kama umebarikiwa,nifahamishe tumtukuze Mungu pamoja. Kwa msaada zaidi na MAOMBI piga sasa kwa + 255 683 877 900

What’s app namba +255 746 446 446

Na. Mch.G. Madumla.

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page