top of page

KWA NINI UNATAFUTA KUJIUA? – 02 ( tamati)

Bwana Yesu asifiwe…

…hata hivyo watu wengi leo wanajiua kwa mambo mengi sana. Kuna watu wanashangaza kwa yale wanayoyafanya. Kwa maana kuna watu ambao wakiwa msibani wanalia vibaya sana kana kwamba wanatamani wafe wao. Hujawahi kuona mtu msibani akilia hivi “…hiii,hiii,hii…kwa nini umeondoka mapema jamaniiii,…hiii,hiii…bora ningekufa mimi,…boraaaa,nife mimi…” Sasa cha ajabu fikiri ndio kama vile Mungu angelisema ;

“…Nimesikia mtu hapa anataka afe yeye badala ya huyu aliyekufa,ni nani huyo asimame…” alafu uone kama huyo aliyekuwa akilia hivyo kama atasimama au ataendelea kulia kwa maneno yake. Umeona hapo,! Yaani mtu wa namna hii alikuwa akitamka maneno ya kifo/ mauti pasipo kuwa makini,wala hajui ni nini anachotamka! Lakini ndivyo leo wengi wanajiua kwa maneno ya vinywa vyao! Jiulize wewe mwenyewe ni mara ngapi umejitamkia mabaya kwamba bora ufe kama ndio maisha yenyewe ndio hivyo!

Mtu mmoja nilimsikia akisema “ …bora nizaliwe paka ulaya,au bora nizaliwe mbwa ulaya,maana huku kwetu njaa kali..” Nikajiuliza huyu mtu ana akili sawa sawa kweli? Anajua alisemalo kweli? Hivi unajua gharama ya kuzaliwa mwanadamu? Kama hujui kwa nini utamani uwe paka au mbwa wa ulaya? Nani kakwambia kwamba ulaya maisha mtelezo? Nenda kawaulize wakazi wa huko watakuambia jinsi maisha yalivyo,nakwambia wakati mwingine maisha ni magumu kuliko ya huko kwenye nchi yako!

Hivyo ni lazima uchunge kinywa chako. Kinywa kinaweza kuua au kuleta uzima,inategemea unakitumiaje.

  1. Kwa nini inafika wakati mtu anajiua?

Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskariote, naye ni mmoja wa wale Thenashara.Akaondoka, akaenda akasema na wakuu wa makuhani na majemadari, jinsi atakavyoweza kumtia mikononi mwao. Wakafurahi, wakapatana naye kumpa fedha.Akakubali, akatafuta nafasi ya kumsaliti kwao pasipokuwapo mkutano.“ Luka 22:1-6

Maandiko yanatupa sababu ya kwa nini Yuda aliweza kumsaliti Yesu. Biblia inasema “shetani alimwingia” ,hiyo ni sababu tosha ya Yuda kumsaliti Yesu na baada ya hapo,ni shetani huyo huyo,aliyempelekesha Yuda kwenda kujiua. Kumbe mtu anapofikia maamuzi ya kujiua basi ujue ndani yake kunamsukumo mkubwa wa shetani. Si rahisi kwa mtu yoyote kujiua kama shetani hajausika kwa maana yeye shetani ndiye muuaji ( Yoh.10:10). Hata kama kutakuwa na sababu nyingine iwayo yote,lakini ujue katika sababu yoyote ni shetani ndiye mwenye kuikuza na kukuleta kwenye kifo.

Nilikuwa ninashangaa namna ambavyo vijana wadogo kwenye baadhi ya nchi zilizoendelea wakijiua kwa sababu ya kile wanachodai eti ni “msongo wa mawazo” hapo nikagundua ni mapepo/ shetani tu ndiye sababu ya wao kujiua. Ukitafuta sababu za watu waliojiua utazikuta nyingi tena nyingi sana, kwa maana wengine watakuambia “ mapenzi ndio yanaua,” wengine watakuambia “ wivu,hasira,chuki” n.k . lakini hayo yote ni shetani tu!

Jifunze kwa Yuda aliyesaliti na baadae akajiua. Bila shaka Yuda hakuona thamani ya kuishi tena ikiwa kama ametenda kosa la namna hile. Bila shaka alikuwa akijiuliza kwamba “hivi,nitaonekanaje? Itakuwaje sasa?” ndivyo hata leo nawe umekuwa ukijiuliza uliza kwa kile ulichokosa “hivi itakuaje sasa?” Ukumbuke dawa sio kujiua,kwa maana hata mtu akijiua bado kosa litabakia pale pale na mbaya zaidi na motoni atakwenda.

  1. Katika kosa kama hilo,ipo njia.

Laiti kama ingelikuwa inawezekana ukamuuliza marehemu aliyejiua kwamba “nini kilikupelekea,hata ukachukua uamuzi huu wa kujimaliza?” bila shaka angeliweza kukujibu hivi “ …nilikosa msaada,sikuona njia yoyote…” na huo ndio ukweli wenyewe. Ukiona mpaka mtu nachukua hatua ya kujiua kwa namna yoyote ile basi ujue alikosa msaada,alifikiri mpaka mwisho kisha shetani akamwonesha njia ya kutatua tatizo hilo,ni kujimaliza ili awe salama!!!

Lakini tambua ya kwamba njia ipo kwake Mungu leo. Huna sababu ya kufanya maamuzi ya kutoa uhai wako,kwa sababu njia ipo ya utatuzi. Hata kama shida kubwa namna gani,kwa Mungu hiyo ni ndogo sana. Hivi unajua Yeye Mungu aweza kushughulikia hilo tatizo nawe ukabaki ukishangaa!!!

  1. Moto wa milele ni wa kila anajiua!

Ni lazima ujue kwamba ikiwa mtu akifanya maamuzi ya kuutoa uhai wake,hawezi kuingia kwenye ufalme wa mbinguni bali ataingia motoni. Na moto wa huko,ni halisi sio maneno ya nadharia tu. Ni vyema ujue ikiwa unakubali kuchomeka milele pasipo msaada wowote,ni hatari kwenda huko,usiombee!!!

Ikiwa moyoni mwako unahisi uchungu kiasi cha kutamani kufa,tafadhali naomba unipigie simu sasa hivi,hata kama upo mbali kiasi gani naomba tuwasiliane sasa,maana huyo ni shetani anayetaka akutie kwenye maamuzi mabaya.

Piga sasa kwa + 255 683 877 900  What’s app ni +255 746 446 446

 ( pamoja na ushauri,na ikiwa umebarikiwa pia na ujumbe huu,nijurishe tafadhari)

Mch.G.Madumla.

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page