top of page

KIJANA, USIPANGE CHUMBA KAMA HUJAJIPANGA


Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi sana.

Ukweli ni kwamba kupanga chumba au nyumba ni jambo muhimu la kuanza maisha nje ya wazazi/walezi wako. Lakini yeyote anayekwenda kupanga lazima awe ana sababu maalumu ya kupanga. Mfano wa sababu maalumu ni pale unapopanga kwa ajili ya kuanza kujitengemea na kuanzisha familia nyingine,huku ukijiandaa vizuri kujenga nyumba yako. Lakini ikiwa unakwenda kupanga chumba bila kuwa na malengo au sababu maalumu zenye maana,basi ni afadhali sana ubakie kwanza kwa wazazi itakusaidia!!!!

Wapo vijana wengi leo hawataki kukaa na wazazi wao kwa maana wanajiona kuwa wameshakuwa watu wazima lakini kwa bahati mbaya si wote wamekomaa kwa kujitegemea. Jamani kujitegemea si jambo dogo! Kujitegemea kunahitaji kujipanga !!! sasa kama utakwenda kujitegemea bila malengo,utapotea kitabia maana tumeshuhudia vijana wengi waliokwenda kujitegemea kwa kufuata “mkumbo”  walipotelea huko huko.

Angalia mfano wa kijana wa namna hii,ambaye yawezekana kabisa alipokuwa kwa wazazi wake hakuweza kunywa pombe au kwenda club kwa sababu ya kuchungwa na wazazi wake au walezi wake. Lakini kwa kuwa sasa anajitegemea anaweza kufanya lolote atakalo,kutoka na kurudi kwake muda wowote atakao. Kwa maana hayupo tena katika himaya ya wazazi/walezi.

  1. Uhuru usiokuwa na mipaka ni uharibifu

Vijana wanaokwenda kupanga bila kujipanga wanatafuta uhuru usiokuwa na mipaka,na kwa sababu hiyo,wanapotea wengi. Hujawahi kuona mabadiliko makubwa ya kitabia yakitokea kwa vijana ambao wamekimbia makwao kwa kigezo tu wanataka kuanzisha miji yao? Ndio wapo wengi. Na ndio maana ninakwambia kwamba ni heri kubaki home kwa wazee kama hujajipanga kupanga!

  1. Kutulia home nako kuna heshima zake

Kwa mabinti ambao wako chini ya wazazi/walezi mara nyingi wanaheshimiwa sana. Unajua hata wakaka wanaohitaji kuoa wanapenda mabinti ambao wapo chini ya usimamizi wa wazazi wao. Na tena pana utofauti mkubwa kati ya binti alianza kujitegemea na yule ambaye yupo kwa wazazi wao.

Utofauti huu ni mkubwa kwa maana yule anayejitegemea afungwi na yoyote,hivyo anaweza kufanya maamuzi yasiyo sawa bali yule aliye chini ya wazazi ni vigumu. Mfano ; Wakaka wanaweza “kumfukuzia”  binti anayeishi kwenye geto la kujitegemea bila hofu,wakaja mpaka getoni,lakini wakaka hawawezi kuja kwa binti aliye kwa wazazi wake mpaka chumbani!!!! Kwa sababu ya kuogopa wazee

Kumbuka;

Sisemi usiende kujitegemea kwa kupanga,lah hasha! Kupanga ni muhimu kama moja ya hatua muhimu ya kuanza kujitegemea kwa maana katika kupanga utajifunza maisha. Ila kama hujajipanga usiende kupanga!

Kwa msaada zaidi pamoja na maombezi, usisite kunipigia simu. +255 683 877 900

What’s app +255 746 446 446

Na mch G. Madumla

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page