top of page

MOYO WA UTAYARI.~ 01

Bwana Yesu asifiwe….

Kwa kifupi,

Mungu hatafuti mtu mkamilifu wa kufanya naye kazi,bali mtu mwenye moyo wa utayari katika upungufu wake alionao ili Mungu amtumie na kumkamilisha. Fikiria kwamba una watoto watatu wanaocheza pamoja na marafiki zao, Lakini muda huo huo nawe unamwitaji mtoto mmoja umtume dukani,hivyo unaita “wee fulani… Ebu njoo mara moja…” lakini kumbe unayemwita amejificha kwa makusudi kwamba usimtume,amenogewa na michezo. Halafu bahati mbaya watoto wako wengine wanajificha pia,halafu gafla kanatokea katoto kengine ka watu ambacho na chenyewe kalikuwa kakicheza na wanao,hiko ndio kinakuja kwako ili umtume,kwa maana kanajua baada ya kutumwa,kataendelea kucheza tena.

Katika mfano huo,unaonesha tofauti kubwa iliyopo kati ya mtoto huyu mdogo na wale watoto wengine, kwamba mtoto mdogo huyu,ana “utayari” wa kutumwa / kutumika. Kwa maana pale wengine walipokataa kutumwa,wakajificha,lakini huyu alikubali kwa haraka tena akiwa ni mtoto asiye wako. Vivyo hivyo ndivyo ilivyo hata katika wokovu na utumishi,wapo wanaofanana na wale watoto waliojificha kukwepa kutumwa,lakini wapo pia wachache wanaokubali kutumika bila kuangalia watafaidika nini.

Utayari ni “moyo” kwa maana kati ya wengi walioitwa,wachache hupenda kwa moyo kujitoa. Usishangae kuona wengine wanakimbia kutumwa na Bwana, kwa maana kuwa na utayari ni jambo la ndani. Biblia inatueleze vyema juu ya moyo wa namna katika habari za Daudi. “ Na alipokwisha kumwondoa huyo, akamwinua Daudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia, akisema, Nimemwona Daudi, mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayefanya mapenzi yangu yote.” Matendo 13:22.Mtu anayeupendeza moyo wa Mungu, ni yule tu aliye na utayari wa kuyafanya atakayo Mungu.

  1. Kuwa na moyo wa utayari ni kukubali kulipa gharama.

Miaka kadhaa nyuma kabla sijaokoka nilikuwa na utayari wa kutumika madhabahuni,na kweli nilikuwa nikitumika,ingawa nilikuwa katika misimamo ya kidini ( sikumjua Bwana kihivyo). Lakini ndani yangu nalijitoa zaidi. Haikuwa rahisi,bali ni gharama nililipa kushinda kanisani kipindi ambacho wengine wapo majumbani kwao,mimi nilikuwa kanisani. Ule moyo wa utayari ulikuwa ndani yangu,na kwa sababu hiyo; Bwana aliniokoa kwa kunipa neema ya wokovu, nikaokoka. Hata sasa,ninatamani kuyafanya mapenzi ya Bwana yote,lakini kitakachonisaidia ni“ moyo wa utayari” tu. Unaweza ukajiuliza kwamba, kwa nini wakati mwingine Mungu amekuwa akiwatumia wale wadogo na kuwaacha wakubwa katika uzao,kama vile mzao wa kwanza ukaachwa,kisha mzao wa pili ukatumika kama lango la baraka. Moja ya sababu kubwa ni kwamba, uzao wa kwanza mara nyingi wamejikuta wakitaka kutumikiwa na sio kutumika. Sasa moyo wa kutumikiwa haiwezi kumpandisha mtu,isipokuwa ule wa kutumikia. Uzao wa pili kwa sababu wenyewe unahesabika ni mdogo,basi mara nyingi uzao huu umejikuta ukitumwa,ukidharahuliwa,n.k na hapo ndipo moyo wa utayari ukijengeka. Ukumbuke kwamba, Moyo wa utayari ni moyo wa Yesu,ni tabia yake maana amesema “Yeye hakuja kutumikiwa,bali kutumika…”

Ebu,fikiria tena mahali unapoabudu wewe,je utayari wako wa kutumika upo wapi? Ndani yako kunawaka ufanye nini? Je unaridhika na mambo yanavyokwenda? Upo na utayari wa kiasi gani? Au je unasubiri mpaka mchungaji wako ahamasishe juu ya jambo fulani ndipo ufanye? Utagundua kwamba, kuna hali ya kusukumwa ndio ufanye kitu fulani,kitu ambacho Bwana hakitaki kabisa! Wale wenye moyo wa utayari kamwe hawasubiri kusukumwa ndio wafanye.

  1. Je moyo wa utayari unapatikanaje?

“maombi” ni kitu cha muhimu sana,unachohitaji kukifanya. Bwana ndiye awezeshaye moyo huu ndani yetu,hivyo waweza kumwomba leo, ( Zab.84 yote,Wafilipi 3:8). Kati ya maombi muhimu kwako,ni kuomba Bwana akupe moyo wa utayari katika utumishi wako….

ITAENDELEA…

Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe. Na kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga kwa+255 683 877 900

Whatsapp namba .+255 746 446 446

Mch. G.Madumla.

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page