top of page

MOYO WA UKAIDI.


Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi;

Moyo wa ukaidi /a sinful heart.

Moyo wa ukaidi ni ule moyo usiotaka kuenenda kwenye utaratibu wa kiungu. Pale unapomwona mtu anayeelekezwa kwamba atembee katika njia impasayo,lakini akikataa,basi ujue huyo ana moyo wa ukaidi,na matokeo yake hakika ataangamia,kwa maana aonywaye mara nyingi akishupaza shingo,atavunjika ghafula wala hapati dawa – Mithali 29:1. Kwa mujibu wa Biblia,tumchukue Kaini kama key study yetu,mtu mwenye moyo wa ukaidi tangu hapo mwanzo. Lakini alionyo vyema kwamba aache ukaidi wake ili asije akaangamia dhambini, lakini kwa ugumu wa moyo wake alikataa maonyo/maelekezo na hatimaye alipotelea pabaya! Baada ya ibada ya matoleo ilipoisha naye sadaka yake haikupokelewa,Bwana alimwambia Kaini,kwamba;

”  Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.” Mwanzo 4:7 Kumbe nafasi ya kutengeneza na Bwana ilikuwa imeachiliwa kwa Kaini,Mungu alimwonya mapema kwamba yampasa aishinde dhambi na tena kama angelitenda vyema katika utaratibu ule aliouweka Mungu,basi angelikubalika na Bwana. Hata hivyo kwa ugumu wa moyo wake,alikataa maonyo hayo. Moyo wake wa dhambi ulimwangamiza. Kaini ni mfano wa mtu mwenye moyo wa ukaidi

  1. Nini chanzo cha moyo huu?

Kila jambo lina chanzo chake,ikiwa chanzo cha roho ya kicho ni Bwana,basi ni dhahili kuwa chanzo cha moyo wa ukaidi ni roho ya shetani kwa maana Bwana Mungu hakuweka roho mbaya ndani yako wala ndani yangu. Hivyo chanzo cha moyo wa dhambi,ukaidi kimetokana na anguko la mwanadamu,ibilisi ndiye hasa mwenye roho ya namna hiyo. Lakini ukitafakari habari ya Kaini kaka wa maovu,utagundua kwamba mbali na kuwepo kwa msukumo wa ibilisi kwake,lakini yeye mwenyewe Kaini aliamua kuishi kwa kufuata utaratibu wake na kukutaa utaratibu wa Mungu,

hali hii inatufundisha na kutuonesha kwamba wapo watu wenye kufanana na Kaini,watu ambao ingawa wamepewa utaratibu wote ufaao lakini wamekataa wao wenyewe kufuata utaratibu huo. Na bahati mbaya sana leo,tunao akina Kaini wengi kwenye nyumba za ibada,watu ambao wameonywa mara nyingi lakini hawataki wala hawapo tayari kubadilika. Je wewe ni mmoja wa akina Kaini?,Chukua hatua sasa ya kubadilika kwa maana mabadiliko halisi yapo ndani yako na yanaanza na wewe. Maombi ndio dawa ya kwanza ya kuleta moyo wa haki kwa kuuondoa moyo wa ukaidi. Waweza kunipigia tushauriane pamoja na maombi;

Ikiwa umebarikiwa nifahamishe tumtukuze Mungu pamoja. Kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga kwa +255 683 877 900

Na.Mch. G.Madumla

Whatsapp namba .+255 746 446 446

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page