top of page

MKE WA UZINZI !

Updated: Aug 29, 2022




Hosea nabii wa Bwana amekuwa nabii wa kipekee aliyepewa agizo au Neno kutoka kwa Bwana kwamba anapaswa kwenda “ kuoa” Binti Gomeri anayefahamika kuwa ni mke wa uzinzi.

Ndoa yake Hosea ilikuwa inatoa maelezo kuhusu Israeli namna walivyokuwa ni wazinzi wa kiroho yaani Israeli ilipoteza uaminifu wake mbele za Bwana ingawa waliokolewa na kutolewa Misri kwa mkono wa Bwana ulio hodari.


Pamoja na kwamba kitabu cha Hosea kiliachilia maonyo makali kwa Israeli, Lakini maelekezo ya kuoa “kahaba” hayakuwa mepesi kwa maana si kitu kidogo kufunga ndoa na kahaba. Kwa maana hatumwoni  Hosea akilalamika katika kumwoa  binti mzinzi,bila shaka alijua kuwa maagizo hayo ni ya Bwana. 


Kikawaida kabisa usiombee kuishi na mume au mke mzinzi. Maumivu ya mke au mume yanauma sana. “jamani moyo unauma unapoona uzinzi wa mpenzi wako” nakwambia usiombee!!! 


Na ilikuwa ni mpango wa Mungu kueleza namna ambavyo “ maumivu yanayoletwa na uzinzi ” ili kusudi tuelewe kwamba sisi hatuna tofauti na mke au bibi harusi ambao tupo katika agano na Mungu.

Fahamu kwamba jina la Hosea lina maana ya “ wokovu ” au “ Mungu anaokoa” na kwa sababu ya jina hilo linaelezea kusudi la Mungu kwa taifa lake. Israeli watoto wa Mungu walivurugwa kwa dhambi zao za kumwacha Mungu.


Hivyo wakawa wazinzi wa kiroho yaani walikosa uaminifu wao. Kwa maana uzinzi wa kiroho ni hali ya kwenda kinyume na uaminifu wako katika agano uliloingia. Israeli nao walikuwa na agano kama taifa teule watu wa milki ya Mungu. 

Nafikiri ndoa ya Hosea haikuwa simulizi tu bali ilikuwa ndoa halisi isipokuwa kwa taratibu za kale wanawake waliokuwa wakiolewa walikuwa ni mabikira ( wanawake wasiojua mume) .

  • Hivyo inawezekana kabisa Gomeri alikuwa mzinzi baada ya kuolewa na Hosea kitu ambacho kinaleta maumivu makali kwa maana kama alikuwa mzinzi kabla ya kuolewa maumivu yake yangelikuwa machache. Kwa maana Neno “ mke wa uzinzi ” ulikuwa ni unabii wa hapo baadae 


Hivyo,Mungu alitaka kuonesha namna ambavyo Israeli ilipokuwa waaminifu na baadae kurudi nyuma kiimani na kupoteza uaminifu wao wakiwa bado ndani ya agano. 

Kwa sababu hiyo, kumbe mke au mume uliye naye aweza kubadilika na kuwa mtu mwingine labda akawa mwaminifu au akawa mzinzi kama alivyo Gomeri. Kilichoandikwa katika kitabu cha Hosea kimeandikwa ili kufundisha kwamba kunaweza kukawa na mabadiliko yoyote katika ndoa yako ingawa kipindi cha Hosea ujumbe ulilenga moja kwa moja kwa Israeli kukosa uaminifu wao.


Lengo maalumu la unabii wa Hosea ni kuwafanya Israeli kutambua nafasi yao ya kwanza waliyoipoteza kwa kupoteza uaminifu lakini kiini pia ni warejee kwa Bwana kwa njia toba. Lakini ukumbuke kitendo cha kuishi na “ mzinzi ” tena bila hata kumfukuza ni kitendo cha “upendo” . Na hivi Mungu alitaka kuonesha upendo wake kwa mtu ambaye amekosa uaminifu  lakini yeye Mungu bado anampenda akimsubiri atubu ( 1 Petro 3:9)

Mke wa uzinzi, Gomeri alikuwa na muda na wanaume wengine na hatimaye akamwacha mumewe Hosea na ndivyo Israeli walikuwa na muda na miungu mingine huku wamemwacha Mungu wa kweli.


Hii ni sawa na kusema mtu anapokuwa mzinzi katika ndoa yake basi hawezi kuwa na muda na mwana ndoa wake isipokuwa yule anayetoka naye,na huyo anaye toka naye ni kitambo tu,si halisi !!!


Mke wa uzinzi anaweza kubadilika?


Kwa mujibu wa Hosea nabii wa Bwana kuao Binti wa uzinzi kama kielelezo cha Israeli kukosa uaminifu wao kwa Mungu ambapo baadae walisisitizwa warejee upya. Basi ni dhahiri mke wa uzinzi anaweza kugeuzwa,na kuwa mtu mwaminifu.


Kitu kikubwa usichoke kumpenda pamoja na kwamba ni mzinzi lakini aweza kugeuzwa na kuwa mtu bora kwako.

Ikiwa kama umebarikiwa,au unahitaji msaada zaidi piga sasa Kwa +255 683 877 900


What’s app number +255 746 446 446


Na Mch. Gasper Madumla


UBARIKIWE

Comentarios


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page