top of page

CHOMBO CHA BWANA.

Updated: Aug 26, 2022


Je! Mtu huyu, Konia, ni chombo kilichodharauliwa, na kuvunjika? Ni chombo kisichopendeza? Mbona wametupwa, yeye na wazao wake, na kutupwa katika nchi wasiyoijua? ” Yeremia 22:28


Kwa ufupi,


“chombo” ni kifaa kilichotengenezwa kwa ajili ya kazi fulani. (Kumbuka; Hakuna chombo kilichotengenezwa bila kusudi/ kazi maalumu). Hivyo kwa kila kazi ya ufundi kuna chombo chake maalumu. Mafundi wanaelewa sana kuhusu umuhimu wa kila chombo kilichomzunguka


Ebu jaribu kupata picha ya fundi seremala afanyapo kazi zake. Kama akitaka kukata mbao,basi atatafuta chombo maalumu cha kukatia mbao. Msumeno ndio hasa chombo maalumu cha kukata mbao. Itakuwa ni ajabu kama fundi seremala atachukua kisu kwa kukata mbao. Sasa,hapo shida sio kisu bali shida kisu kimetumika nje ya kusudi. 

Kama ilivyo fundi mwenye kufanya vyombo mbali mbali ndivyo nasi tulivyo kwamba ni vyombo tofauti tofauti. Biblia inamtaja “Konia” kuwa chombo. ( Kumbuka; Konia alitawala muda wa miezi mitatu tu baadae akachukuliwa kwenda Babeli). Lakini kwa bahati mbaya “Konia” amekuwa chombo kilichodharauliwa na kutupwa.


Kumbuka ;


Kama “Konia” ni chombo kilichotupwa,basi ujue kuna sababu ya kutupwa kwa maana ukiona mtu amekitupa chombo,ni lazima atakuwa na sababu. Moja ya sababu kubwa inayopelekea chombo kutupwa ni “kupoteza thamani yake “. Na kama chombo kimepoteza thamani yake,basi hakifai tena. Konia na uzao wake ni vyombo vilivyopoteza thamani hata vikatupwa katika nchi ya ugeni. Konia kama chombo kilichoacha kusudi lake,kilipoteza thamani. Hata kupelekea kutupwa.


Kumbuka;


Dhambi ndio kitu pekee kinacho haribu chombo hata kupelekea kutupwa. Lakini kwa upendo wa Mungu, chombo chake kinapoharipiwa Yeye hukifanya tena kama apendavyo yeye mwenyewe. Lakini ikiwa chombo hicho kikikataa matengenezo,basi ni lazima kitupwe.

Ikiwa umebarikiwa na ujumbe huu, nifahamishe tumtukuze Mungu pamoja.


Na kwa msaada zaidi piga +255 683 877 900.


What’s app +255 746 446 446.


Na Mch. Gasper Madumla.


UBARIKIWE.

Comentários


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page