top of page

HAZINA NJEMA YA WATOTO.

Updated: Sep 2, 2022


Ni kitu gani ulichomwekea watoto wako kwa maisha ya baadae? Ni nini hasa unachokipanda kwa ajili yao? Au ni nini unachomtengenezea mwanao kwa maisha yake yajayo? Bila shaka wengi huwapa elimu bora watoto wao kama hazina njema ya maisha yao. Lakini unafikiri elimu tu inatosha kuwafanya watoto kuwa bora hapo baadae? La hasha Elimu ni kitu kizuri,lakini hakiwezi kumfanya mtoto wako kuwa bora kwa maana wapo watoto waliosomeshwa hadi elimu ya juu,lakini leo wanamaisha mabaya kuliko maelezo!!!


Kumbe katika elimu ya dunia kuna kitu kinakosekana,kitu hicho ndicho kiitwacho “ hazina njema ya watoto ” si fedha wala mali,bali ni elimu ya Mungu/Maarifa ya Neno kwa watoto.

Kumbuka,kitu cha kwanza kabisa kwa upande wa Bwana alichowasisitiza Israeli walipotoka utumwani Misri,ilikuwa juu ya kuwafundisha watoto kuhusu wakovu mkuu alioufanya kuwatoa Israeli utumwani. “ Kisha itakuwa hapo mwanao atakapokuuliza keshoni, akisema, Ni nini hivi? Utamwambia, BWANA alimtoa Misri, kutoka ile nyumba ya utumwa, kwa uwezo wa mkono wake;” Kutoka 13:14


Mkazo wa Mungu, ni kukikata kizazi kipya kijue ni Mungu wa namna gani anayepaswa kuabudiwa. Ni nani atakayekiambia kizazi kipya,kama si mzazi? Habari za wokovu zilikusudiwa zipenyeshwe kutoka kwa wazazi kuwafikilia watoto wote. Nilikuwa nikijiuliza,kwa nini Bwana aliwataka wazazi wapeleke habari njema kwa watoto wao? Nikagundua kwamba, Mungu aliwataka wazazi waeleze ukuu wa Mungu wa kweli,


pia kukiandaa kizazi bora kitakachokuwa na maarifa ya kiungu. Watoto wana kawaida ya kuuliza,na kutafuta kujua mambo mengi,katika kipindi hicho,ndio kipindi cha kushiriki Neno ili wakue wakimjua Mungu

Katika andiko hilo ( Kutoka 13:14),watoto walitakiwa kujua habari za utumwa wa baba zao na kujua ni kwa namna gani waliteseka muda wa miaka 430. Kisha walitakiwa kujua Pasaka/ukombozi wa Mungu namna ulivyofanyika. Watoto wajue kwamba


“ hakuna aokoaye ila Mungu ” lakini waone pendo kuu alilonalo Mungu,hiyo ndio hazina njema kwa watoto wako pia. Je ni kweli unawafundisha wanao Neno la Mungu? Kwa kiasi gani? Je unafikiri kwa elimu wanayoipata mashuleni itawajenga kuwa watu bora hapo baadae? Lah hasha!!! Sidhani kama unatumia muda wako kukaa na watoto wako katika Neno la Mungu! Sidhani hata kidogo!!!


Ebu jiulize tena,unapowaacha watoto hao wajiendee wenyewe,unafikiri watakuwaje hapo baadae? Je hapo baadae utawaweza wewe? Au watakuweza wewe? Mimi nafikiri wao ndio watakao kuweza,kisha utakuja ule msemo “watoto wa siku hizi,wameshindikana!” Sio hivyo,ni wewe ndio labda hukujua namna ya kuwaongoza,au ulijua kisha ukaipotezea fulani hivi,na leo wanakushinda! “kuzijua siri za ufalme wa Mungu ” ndio hazina njema kwa watoto wako. Ni afadhali umnyime pesa mwanao,au gari,lakini sio maarifa ya Mungu.


Je unajua mpaka Bwana ilipofika wakati ilibidi awaambie wazazi,kwamba waende kuwafundisha watoto wao kuhusu namna ya ukombozi uliofanyika kwao. Kwa maana Bwana anawajua vyema wazazi, kwamba ni wazito na wagumu kuwafundisha watoto wao mambo ya Mungu. Na hata sasa hali iko hivyo hivyo. Kushindwa kuwalea watoto wako katika misingi ya wokovu kunawapelekea watoto hao kuwa chakula cha shetani! Tena kunawafanya watoto kuwa marafiki wa dunia ambapo watakuwa ni adui wa Mungu.


Hazina njema inatengenezwa na wazazi, haiji automatically,bali ni suala la mchakato. Unataka mwanao aweje hapo baadae? Anza kumwekea hazina ya Neno la Mungu. Kumbuka; ukimpeleka mtoto wako kwenye “mapokeo ya kidini” unampoteza huko,bali mpeleke kwenye misingi ya wokovu ili akue akimjua Mungu wa kweli. Wengi wetu tulipokuwa wadogo,tulipelekwa kwenye makanisa ya kidini,tukajifunza elimu fulani inayokinzana na Neno halisi la Mungu,


ingawa muda mwingine ni kana kwamba inafanana.

Na tukakulia huko,Sasa katika utu uzima wetu,maelimu hayo ya kale yamekuwa ukuta unaozuia wokovu wa Mungu, kwa maana wengi hukataa suala la wokovu kwa sababu hatukufundishwa hivyo.!!!


Sasa wewe,unayo nafasi kumfundisha mwanao habari sahihi za Yesu na WOKOVU mkuu alioleta. Chukua jukumu hili leo,la kumwekea hazina njema ya Neno la Mungu kwenye maisha yao,kwa kuwafundisha na kuhakikisha wanashiriki kikamilifu kwenye shule za Jumapili (Sunday school)


Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe.

Na kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga kwa+255 683 877 900


Whatsapp namba .+255 746 446 446


Mch. G.Madumla.


UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page