MIJI MITATU AMBAYO YESU ALIFANYA MIUJIZA MINGI.
- Mch. Gasper Madumla
- Feb 22, 2019
- 2 min read

Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi.
“ Ndipo akaanza kuikemea miji ile ambamo ndani yake ilifanyika miujiza yake iliyo mingi, kwa sababu haikutubu.” Mathayo 11:20
Ilifika wakati Yesu aliikemea miji mitatu ambayo kwa kweli kazi ya Mungu ilidhihilishwa kwao,kwa kuwa na shingo ngumu,hawakuweza kutubu. Watu wa miji hiyo hawakumwamini kuwa ndiye masihi wa Bwana, ingawa walisikia na kuona mengi yaliyotendeka. “ Ole” ilikuwa ikiwahusu watu wote wa miji hii mitatu.
Ninapojifunza jambo hili,ninaogopa kidogo kwa maana hata leo,ukiangalia baadhi ya miji tena miji mikuu,kazi ya Mungu imedhihilishwa,lakini bado wakazi wa miji wamemkataa Yesu,wala hawamwamini! Hakika ole hii aisemayo Yesu haiwezi kutuacha salama. Sajajua wewe upo katika mji gani,lakini mimi nipo Dar es salaam mji ambao kazi ya Yesu imefanyika na hata sasa inafanyika katika ukubwa,kwa maana makanisa ni mengi,vituo vya injili ni vingi,lakini cha ajabu wakazi wengine walio wengi wamemkataa Yesu!!! Miji ambayo Yesu alifanya miujiza mingi ni kama ifuatavyo;
01. Kapernaumu. ( Mathayo 11:23)
Huu ulikuwa mji mkubwa na wenye maana katika kipindi cha Yesu. Ulikuwa katika pwani ya ziwa Galilaya. Kwa kuwa Yesu alifanya huduma yake kubwa kwenye mji huu,hata ukaitwa mji wa Yesu ( Mathayo 9:1). Bila shaka ulikuwa mji wenye makao ya makuu ya huduma yake. Na ukumbuke kwamba, Kapernaumu ndipo Mathayo mtoza ushuru alitokea hapo kwa maana kwa umaarifu na ukubwa wake ulisababisha kuwepo kwa watoza ushuru . Ijapokuwa miujiza mingi ya Yesu ilifanyika lakini watu hawakuweza kugeuka na kumwamini Yesu.
02. Bethsaida ( Mathayo 11:20-21)
Ulikuwa mji muhimu kwa wavuvi kaskazini ma Galilaya. Watu kama Petro na ndugu yake Andrea walitokea hapa,ambapo baadae wakawa mitume wa Yesu,hata Filipo pia ni mwenyeji wa Bethania. Yesu alifanya miujiza mingi hapa,kama vile aliwapa watu kula kama 5000,aliponya pia na baadhi ya miujiza. Hata hivyo wenyeweji wake hawakumwamini hata kutubu, walistahili
03. Korazini ( Luka 10:13)
Ni sehemu ya ziwa Galilaya, haikuwa mbali na Kapernaumu na Bethsaida kwa maana ni kama maili mbili hivi kutoka Kapernaumu. Ole ilikuwa pia kwa Korazini kwa maana walishuhudia miujiza / kazi kubwa ya Bwana lakini hawakuamini wala kutubu ( Luka 10:13).
Hivyo miji hii mitatu Kapernaumu, Bethsaida na Korazini ilikuwa ipo karibu karibu,ilikaa mfano wa pembe tatu. Ambapo Korazini ilikuwa juu kushoto Kapernaumu na kulia Bethsaida miji hii ilikuwa kaskazini mwa ziwa Galilaya. Hata hivyo watu wake walikuwa wagumu,hawakutubu ni afadhali miujiza hiyo ingelifanyika huko Tiro na Sidoni ( miji ya maana na maarufu ya Foinike), wangelitubu tangu hapo na kuvaa magunia. Lakini Ole ni kwa Kapernaumu, Bethsaida na Korazini miji mbayo iliyaona mengi/ miujiza mingi ya Yesu Kristo.
Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe. Kwa MAOMBI pia piga kwa +255 683 877 900
Whatsapp namba .+255 746 446 446
Na Mch.G.Madumla.
UBARIKIWE.
Comments