MFARISAYO NIKODEMO MKUU WA WAYAHUDI.
- Mch. Gasper Madumla
- Mar 13, 2018
- 2 min read

Picha from google mfano tu wa farisayo
Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi.
Kuna mengi ya kujifunza tunapomuangalia huyu mkuu wa Wayahudi aitwae Nikodemo. Natamani leo hii uweze kuona kama nionavyo mimi katika yale ninayojifunza. Kwanza kabisa Nikodemo alikuwa ni kiongozi wa dini, Mfarisayo; mtu aliyemuendea Yesu usiku kwa hofu kwa kuwa aliwaogopa Wayahudi maana kama angelimuendea mchana angelionekana,na hata hivyo alikuwa na mazungumzo marefu sana na Bwana Yesu. (Nikodemo asingeliweza kumuendea Yesu wakati wa mchana,kwa kuwa mchana Yesu alikuwa akisongwa na umati mkubwa wa watu,Nikodemo akahofia kuonekana)- Yohana 3:1-21.
Kumbuka mtu huyu alikuwa ni mwalimu wa sheria aliyebobea toka ujana wake. Katika mazungumzo yake anaanza na kusema
“ Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye.” Yohana 3:1
Neno “ Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu;” linatupa uhakika kwamba Nikodemo alimtambua Yesu kwenye nafasi yake kwamba“ Yesu ni mwalimu”. Nikodemo ameanza vizuri kutambua uwepo wa Yesu,lakini Nikodemo anatupa picha kwamba hata Mafarisayo walikuwa wakimtambua Yesu kuwa ametoka kwa Mungu. Ndio maana unaona neno “ Rabi,twajua…” Hivyo Mafarisayo wanamjua Yesu ni nani haswa,maana kupitia huyu mwakilishi wao asemapo “, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; “
Lakini,baada ya kusema hayo,tunaona Yesu akajibu, akamwambia, “ Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.” Nikodemo ambaye ni mwalimu wa miaka mingi Israeli,anapewa majibu hayo. Kwa lugha nyepesi Yesu anamwambia yeye ( Nikodemo) asipozaliwa mara ya pili,hawezi kuuona ufalme wa Mungu. Hapo ndipo Nikodemo alipoanza kuchanganyikiwa kwenye akili zake,maana Nikodemo alijua ufalme wa Mungu atauona kwa kuwa.anafundisha sana,kwa kuwa ni mtu mkubwa katika jamii,kwa kuwa anaijua dini na taratibu zote!!!lakini loh! Yote hayo hayakumsaidia.
Kumbe nje ya wokovu ni kazi bure hata kama u mwalimu kwenye dini au uwe na nafasi kwenye jamii. Nikodemo labda alitegemea,atasifiwa kwa sababu ni mwalimu wa siku nyingi lakini hali haikuwa hivyo. Sijui alijisikiaje alivyoelezwa ukweli huo. Ebu fikiria ungelikuwa wewe ndio Nikodemo,U mwalimu wa siku nyingi,unajitahidi sana katika dini yako,alafu unakutana na Yesu anakuambia “huwezi kuuona ufalme wa Mungu,ujapojitahidi kama hujazaliwa mara ya pili.” Nafikiri labda ungelimuuliza Bwana,“mbona ninaishika sana dini yangu?”
Watu wengine husema kwamba Nikodemo alikuwa akijua suala la kuzaliwa kwa mara ya pili,maana alimuuliza kwamba mtu awezaji kuingia tena tumboni mwa mamae na akazaliwa tena? Kwa maneno hayo,naye ni mwalimu wa Israeli hayafanani na yeye. Yaani mwalimu wa Israeli anayefundisha siku nyingi anawezaje hakawa na swali kama hilo? Hivyo inawezekana akawa anajua lakini akawa akijifanya hajui. Lakini ukiangalia kwa undani mazungumzo yao,utagundua kwamba Nikodemo hakuwa na ufahamu wa mambo ya kiroho aliyozungumza Yesu ingawa alikuwa akijua mambo ya dini katika sheria. Na kwa sababu hiyo,Kuna kitu kinachoitwa“ proud” yani kuona upo sahihi sana kwa sababu ya mapokeo ya kidini na sio wokovu kujishusha. Na ndivyo Nikodemo alivyokuwa,naye akaondoka bila kuokoka.
mtazamo wangu naona jasho lilimtoka Nikodemo kwa sababu kwanza hakuwa akiwaza kama angelipata majibu ya namna hiyo maana hata hivyo kibaya zaidi hatuoni kama Nikodemo alimpokea Yesu,na hilo ndilo baya zaidi. Leo usifanane na Nikodemo,bali weka imani yako kwa Yesu Kristo awe Bwana na mwokozi wa maisha yako
Hivyo kama Nikodemo angelimsikia Yesu,kisha angelitaka afikie kile alichokua akikisema Bwana. Then,angelitamani sasa afikishe habari hiyo kwa wenzake mafarisayo. Ingelikuwa njema sana.
Kwa huduma ya maombezi,nipigie sasa kwa namba hizi;+255 683 877 900
Namba ya What’sapp ni .+255 746 446 446
Mch. Gasper Madumla.
UBARIKIWE.
Comments