MFANO WA DEPOSIT SLIP KATIKA IMANI.
- Mch. Gasper Madumla
- Feb 12, 2019
- 2 min read

Shalom…
Kwa ufupi.
Unapoenda bank na kuweka pesa zako kwenye akaunti,kuna form fulani ya kibenki ya kuweka pesa zako,ile form inaitwa “ deposit slip ” Hivyo deposit slip ni form maalumu ya kuweka pesa kwenye akaunti yako. Ukijaza form hiyo na ukaweka pesa kwenye akaunti yako, uwe na uhakika pesa yako iko kwenye akaunti.
Ninakumbuka miaka michache nilikuwa katika ofisi fulani kwenye kitengo cha uhasibu. Nilikuwa mara kwa mara ninaweka na kutoa pesa kutoka akaunti yetu. Leo,ninaikumbuka ile form ya kuwekea pesa / deposit slip. Nami ninaingalia kwa mtazamo wa kiimani kidogo.
Ukiwa na pesa yako na umefika bank na umekusudia kuiweka kwenye akaunti yako. Basi utapewa form ya kujaza/deposit slip; nawe utajaza vizuri na ukimaliza unazipeleka pesa zako kwenye dirisha moja wapo la cashier / teller, kisha yule cashier atakupa karatasi / fomu ya kuonesha umeweka pesa yako kwa usahihi kwenye akaunti yako.
Ukitoka hapo pamoja na pay in slip,/deposit slip yenye muhuri wa bank hapo utakapoiangalia hiyo deposit slip / pay in utaziona pesa zako, ingawa pesa zako zipo bank kwa sababu deposit slip inakupa uhakika wa pesa zako zimekwisha ingia kwenye akaunti salama.
Akitokea mtu akakuwekea pesa kwenye akaunti yako, akaweka cash na kisha akaja akakuonesha deposit slip basi hapo moja kwa moja kiroho chako kwatu 😁😁😁. Unaamini pesa zipo kwenye akaunti kwa sababu umeona cash deposit slip.
Sasa, imani inafanana na cash deposit slip. Uombapo, lazima uamini na kuwa na uhakika kwamba umekwishapata. Bila hofu ona kwamba kile ulichoomba kimepatikana tayari, na kipo kwenye akaunti yako ( Mathayo 21:21-22). Mwenye Imani inafanana anafanana na yule anayekwenda kuweka pesa kwenye akaunti, mwombaji huweka maombi yake kwenye akaunti, na bila shaka anapaswa kuamini kile alichokiweka kwamba kipo. Hivyo anapoangalia akaunti yake anapaswa aone majibu ya kile alichokiweka.
Ikiwa kanuni hii ni ya kawaida kabisa, kwa nini mtu wa Bwana imani yako isiwe kama cash deposit slip? Yaani pasipo shaka unajua kama uliomba mke/mume au chochote ukafanya, basi imani yako iwe kama cash deposit slip. Unajua cash deposit slip haidanganyi, hata kama mtu atakataa kwamba hakuna pesa lakini ukweli ni kwamba pesa ipo, haidanganyi hiyo form kwa maana tayari imepokelewa. Fikiria maombi unayoyaomba, ukaamini kwamba Mungu kayapokea na tayari ameyapiga muhuri wa mbinguni, ni nani awezaye kukataa?
Fikiri mwenye deposit slip akaichana, je pesa yake haitaonekana kwenye akaunti yake? Jibu ni jepesi tu, deposit slip inakuonesha tu kwamba kiasi fulani kimeingia bank kwa hiyo ukiamua kuichana au usiichane, haizuii uwepo wa pesa zako kwenye akaunti yako bank. Pesa zipo pale pale. Imani uliyonayo ikibezwa, ukasemwa hata hivyo havizuii kile ambacho Bwana alichokitenda kwako. Chochote ufanyacho kwa Bwana, ona kama deposit slip kwamba umekwishapokea tayari na hakuna wa kukunyanganya maana ni chako.
Ikiwa kama umebarikiwa nifahamishe, pia Kwa maombi na msaada zaidi , piga +255 683 877 900.
What’sapp namba +255 746 446 446
Mch. G. Madumla.
UBARIKIWE.
Comments