top of page

MFALME HERODE – 1


Picha kutoka Google.


Kwa ufupi…

Bwana Yesu asifiwe…

Jina “ Herode” Herode ni jina la wafalme linalowakilisha hasa wafalme wanne waliotawala kati ya sehemu ya Yuda (Judea) chini ya utawala wa kirumi. Hivyo ni Herode ni jina la “ cheo” cha watawala katika agano jipya,kama leo tunavyotumia cheo cha watawala wetu kwa jina la “raisi”

  1. .Herode mkuu ( Herode the great)

Alikuwa ni mfalme katika Yuda,Galilaya,Iturea na Traconitis mnamo 37-4 kabla ya Kristo (BC). Habari zake tunazisoma kwenye 2:1-19 pamoja na Luka 1:15.Mara tu baada ya kifo cha Herode ,Nusu ya ufalme wake ,ikijumuisha Yuda, Ideumaea, na Samalia,ulitwaliwa na mtoto wake Archelaus,mbapo ufalme wake uliobakia uligawanywa katikati ya watoto wake wengine. Ni mtoto wa Antipater ambaye mama wa Antipater ni Doris

  1. .Herode Philipo II- Mama yake ni Cleopatra,alikuwa mfalme wa Iturea na Traconitis (4BC-AD34). Soma Luka 3:1

  2. Herode Antipas

Alikuwa mfalme katika Galilaya na Perea ( mnamo 4BC- AD39) mama yake ni Malthace. ,>Msamaria.Soma Luka 3:1,; Herode Antipas ndiye Yule Herode aliyepelekea kifo cha Yohana mbatizaji kwa kukatwa kichwa chake akiwa gerezani. Soma Mathayo 14 :1-12,Marko 6:14-29. Pia Herode Antipas anaonekana kuwa ni mfuasi wa Masadukayo Mathayo 16:6 . Pilato alimpelekea Yesu kwake ( Luka 23:7-12)- alikuwa ni mume wa pili wa Herodia

  1.  Herode Agrippa I. ( AD 37-44) – (Au Herode Agrippa mkuu).Huyu alikuwa ni mjukuu wa Herode mkuu,(Herod the great)Waweza kusoma habari zake pia katika Matendo 12: :1-25,Na ndie aliyemua Yakobo ndugu yake Yohana.“ Panapo majira yale yale Herode mfalme akanyosha mikono yake kuwatenda mabaya baadhi ya watu wa kanisa.Akamwua Yakobo, ndugu yake Yohana, kwa upanga.” Matendo 12:1-2. Ndie pia alimtupa Petro gerezani Matendo 12:1-24.( Agrippa mkuu alikuwa ni mtu aliyeshika YUDA na Samaria ambazo babu yake alikuwa ndio muanzilishi.

  2. .Herode Agrippa II.  

Alikuwa mfalme katika Yuda,na ni mtoto wa Agrippa wa kwanza,(Herode Arippa mkuu) Pia habari zake zinaonekana katika Matendo 25 :1-26,Tena katika mstari wa 13 Linalomeka hivi hilo andiko ;“ Siku kadha wa kadha zilipokwisha kupita,Agripa mfalme na Bernike wakafika Kaisaria, wakimwamkia Festo.” Paulo alikuwa akijitetea mbele zake

  1. .Herode Archelaus ( Mama yake ni Malthace) Alikuwa mfalme katika Yuda, Idumea na Samaria ( 4 BC – AD6). Ni mtoto wa Herode mkuu na Kilikuwa ni kipindi ambacho Yusufu na Mariamu walipoondoka Misri na kukaa Nazareth – Mathayo 2:19-23.

Kumbuka; Alikuwepo Aristobus ( mamaye ni Mariamne) alikufa 10 BC)- hakuna taarifa zake za kutawala. Pia Herode Philipo I. Mama yake ni Mariamne,huyu hakuongoza / hakutawala( alikuwa ni mume wa kwanza wa Herodia) Mathayo 14:3,alikufa AD34.

Hivyo ni Herode sita tu ambao ndio walitawala katika nafasi ya ufalme nao ni Herode mkuu,Herode philip II,Archelaus,Herode Antipas,Herode Agrippa I,na Herode Agrippa II. Hata hivyo katika utawala mwingine tunaona Feliki mkewe ni Drusila huyu Feliki alikuwa mtawala / A governor of Judea wa Yuda mnamo AD52-59 Matendo 24:24 Alitaraji kupokea rushwa kupotosha haki mbele ya Paulo. Ni matumaini yangu kuna kitu umejifunza siku ya leo,basi ikiwa ndivyo nipigie simu na uniambie umejifunza na tuombe pamoja kwa kujifunza mambo hayo.

ITAENDELEA

Piga sasa kwa;

+255 683 877 900 Namba ya what’s app ni .+255 746 446 446

Mchungaji Gasper Madumla.

UBARIKIWE..

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page