top of page

METHUSELA MTU ALIYEISHI MIAKA MINGI KULIKO WOTE.


Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi;

Ni mtoto wa Henoko kwenye kizazi cha Sethi,mtu wa ajabu kuwahi kuishi kwa miaka mingi kuliko wanadamu wote kwa maana miaka yake ilikuwa ni miaka 969 (Mwanzo 5:25-27).Wengi walikuja na wengi waliondoka katika miaka yake Methusela. Ni baba pia wa Lameki aliyemzaa Nuhu mtu aliyekwenda na Mungu. Hatujui nini ilikuwa siri ya kuishi kwa muda mrefu namna hii,bila shaka kuna siri katika maisha ya Methusela. Hata Adamu na Sara hawakupewa miaka mingi kama ya Methusela. Ukiwaona watu wanatangaza mtu mwenye umri mkubwa katika siku za leo watakuwa wanazungumzia umri wa miaka 100 +,lakini sio 900+,Methusela alikuwa na siri ya kuishi miaka mingi kuliko wanadamu wote walioandikwa.

  1. Alifanya nini cha ajabu?

Biblia haitaji chochote alichokifanya mtu huyu isipokuwa aliishi,akawa na uzazi kisha akafa. Inawezekana kulikuwa hakuna chochote alichokifanya kile cha ajabu! Lakini uzuri wake ni kwamba alikuwa kwenye mlolongo wa kizazi kilichopitisha neema ya Bwana kwa maana alimzaa Lameki,Na Lameki akamzaa Nuhu,na Nuhu kukatokea Shemu,Hamu na Yafeti,na kwa Shemu kwake kukazaliwa Ibrahimu na hapo ukoo wa Yesu ukaanza. Ikiwa hakuna chochote alichokifanya huyu ndugu,si jambo la kujifunza kutoka kwake.

 Wengi tunamlaumu Methusela kwa maana hatuoni kitu alichokifanya kwa miaka yote hiyo aliyopewa na Bwana zaidi ya kuzaa tu. Je leo hii,hawapo akina Methusela? watu waliopewa miaka mingi,lakini hawakufanya lolote zaidi ya kuzaa kisha wakafa! Hii in changamoto kwako,kwa umri uliopewa na Bwana,ni vyema uwe na alama ya kitu ulichokifanya utakachokumbukwa na watu kwamba watu wajifunze kwako.

Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe. Kwa msaada zaidi na MAOMBI piga ;+255 683 877 900.

Whatsapp namba+255 746 446 446 .

Na Mch. G. Madumla.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page