MBALI NA WOKOVU,U CHAKULA CHA WACHAWI.
- Mch. Gasper Madumla
- May 19, 2015
- 1 min read

Mchungaji Gasper Mdumla.
Bwana Yesu asifiwe
Kwa ufupi,
Tunapozungumzia “Dini” tunamaa ya mpango wa mwanadamu wa kumtafuta Mungu. Mpango huu ni taratibu za kibinadamu alizojiwekea/walizoweka. Na mara nyingi mpango wa mwanadamu ni kizuizi kikubwa cha wokovu,kwa sababu kama upo kwenye dini/mpango fulani,utajikuta utakinzana na wokovu kwa kuukataa kabisa kwa maana dini hazikubaliani na wokovu. Wachawi wanajua hili,kwamba watu walio mbali na wokovu,ni watu bariki kiroho,wamepoa na hatimaye wanaweza kufanya lolote lile na wasipingwe kwa sababu watu wa dini hawana nguvu halisi za Roho mtakatifu,kwanza hata kumjua kama kuna Roho hawajui! Loh !!!Hii ni atali sana,Ndio maana Paulo aliwauliza wanafunzi fulani kule Efeso /wanafunzi wa Yohana mbatizaji kwamba mlipokea Roho mtakatifu mlipoamini?,wao wakamjibu hata kusikia kwamba kuna Roho mtakatifu hawajasikia – Matendo 19:2-3
Wachawi wana nguvu kwa walio mbali na Bwana,ni kama vile watu hao wanakuwa ni chakula kwao kwa maana chochote watakacho kufanya wanafanya tu! shetani haogopi jinala lako la kiristo,au familia uliyotoka,au kanisa unaloabudu bali uogopa hali ya uhusiano wako na Mungu. Ukitaka kuwa shinda roho za wachawi,mpe Yesu maisha yako sasa,kisha chukua hatua ya kukua kiroho kwa Neno na maombi. Ni simpo tu!
Angalia maisha ya Paulo,utagundua kwamba hakutishwa na akina Elima wachawi wabobevu katika uchawi wao ( Matendo 13:6-12). Paulo Aliwashinda kabisa wachawi wote,kwa maana Roho wa Mungu alikuwa ndani yake. Wachawi walipomuona Paulo,hawakuangalia jina lake Paulo wala ukoo wake,bali waliangalia Paulo amebeba nini moyoni mwake na hapo ndipo ushindi unapoonekana. Ukiwa na Yesu moyoni,hakuna cha uchawi wala uganga utakaokula maisha yako,tambua hilo.
Ikiwa kama umebarikiwa,nifahamishe tumtukuze Mungu pamoja. Kwa msaada zaidi na MAOMBI piga sasa kwa + 255 683 877 900
What’s app namba +255 746 446 446
Na. Mch.G. Madumla.
UBARIKIWE.
Comments