top of page

MATESO YA MWENYE HAKI

Updated: Sep 5, 2022

Na MchG.Madumla.



baba yangu wa kiroho anasimulia kwa ufupi akiwa anafundisha ibadani siku moja. Anasema alizaliwa kijijini eneo fulani lenye milima milima na akasomea huko kwa shida fulani hivi kwa kuwa kipindi kile hakikuwa na maendeleo kama ya leo,hivyo elimu ya Tanzania kwa sehemu kubwa ilikuwa ni elimu ya shida sana. Lakini yeye,alipokuwa mwanafunzi alisoma kwa bidii akitaraji kuwa mfanyabiashara hapo baadae.


Hivyo hakukatishwa tamaa na changamoto alizokutana nazo maana alijua kwamba ni za muda tu,na hata hivyo ndoto yake itatimia. Na kweli akafanikiwa kufaulu na kupata nafasi ya masomo ya juu katika shule ya Minaki iliyopo pugu Dar. Alipata mateso ya kimaangaiko,lakini kwa kuwa alitarajia kuitimiza ndoto yake hivyo mateso hayo yalikuwa ni mtaji kwa maisha yake.


Ndipo iliponilazimu kuliangalia jambo hili kwa upana zaidi; kwa maana ukiwaangalia washindanao,hujizuia yote na kukubali kuteseka kwa kitambo tu ili waweze kushinda machezo. Biblia inatueleza;


“Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika. ” 1 Wakorintho 9:25


Mfano; tazama jinsi mwana michezo ya ndondi. Watu ambao hujizuia kwa mambo mengi ili miili yao iwe shupavu,wanapangiwa hata vyakula na vinywaji vya kunywa. Lakini si hao tu ebu waangalie wanariadha vile vile,ebu waangalie tena watu ambao wanahitaji kupunguza mafuta katika miili yao jinsi ambavyo wanavyojitutumua kwenye mazoezi na papo hapo huteseka kwa kujinyima baadhi ya vyakula. Tena mazoezi yao,wengine ulipa pesa jimu kukimbia wanakimbia,kuchoka na wanachoka,! Alafu na pesa wanalipa yaani sio bure! Lakini yote haya ni kwa sababu wanatarajia kupata afya njema.


Angalia mfano wa mama mjamzito anavyopata shida mara aende kliniki,wakati mwingi anahisi kuchoka,kichefuchefu n.k lakini katika mateso yote hayo, anatarajia kupata mtoto na ndipo fulaha yake ipo hapo. Kisha akishapata mtoto mara husaau yote hayo.

Sasa haya yote ni mateso ambayo ni mtaji kwako kwa hapo baadae. Mateso haya niliyokuelezea ni kusudi mtu apokee taji yenye kuharibika,lakini tunapozungumzia mateso ya mwenye haki ni yale mateso yanayookufanya mwisho upokee taji isiyoharibika.


Lakini ni lazima ukumbuke kwamba kusudi ili uweze kupokea taji isiyoharibika yakupasa uvumilie/uwe mtu wa kuvumilia katika hayo yote unayoyapitia. Kwa maana atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokoka ( Marko 13:13)


Bilia inaeleza kwamba ikiwa unamfuata Yesu kikamilivu basi utachukiwa na watu,na utapelekwa katika masinagogi. Lakini utavikwa taji usipozimia moyo yaani utamuona Bwana usipokata tamaa/ukiwa na uvumilivu. Leo hii kuna mateso mengi lakini kumbuka neno lisemavyo ;


“Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini BWANA humponya nayo yote.” Zab.34:19


Mimi sijui mateso yako yapo eneo gani? Inawezekana kabisa mateso yako ikawa hali yako ya kiafya. Kwamba umeokoka vizuri lakini bado unaona magonjwa hayatoki kwako. Sikia leo neno la Mungu,Mungu hajakuacha bali tambua kwamba hayo yote ni sehemu tu ya mtaji kwako kwa maisha ya baadae,kwa kuwa lipo tumaini kwake Bwana.


Bwana atakuponya nayo yote,lakini usijiukumu kwa lolote,wewe muachie Bwana aendelee na kazi yake huku ukiyatazama kama mtaji katika maisha yako. Unajua yapo mateso mengi upitiayo,na katika hayo yote haina maana kwamba Mungu hajakusikia pale ulipoomba bali kuna namna Mungu anafanya ili umjue zaidi na usipotelee dhambini.


Ukifanikiwa kuvumilia katika hayo yote unayopitia ukiwa ndaninya Yesu na Yesu ndani yako basi utakuwa mwenye heri yaani ; “ Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.” Yakobo 1:12


Ujue kwamba ikiwa utayatazamia maisha ya baadae utapata kuwa na tumani katik hayo unayopitia. Ebu angalia mfano mdogo tu kwa wafanyakazi. Utakuta mtu ameajiriwa kazi fulani,hivyo uamka asubuhi sana au wakati mwingine ni usiku usiku, kama saa tisa na nusu au kumi hivi na anafanya bidii awahi ofisini kisha afanye kazi kwa bidii “ akitajaria kupata malipo mwisho wa mwezi”.


Ebu jiulize,Vipi kama kusingelikuwa na msharaha,Je mtu angeliweza kudamka asubuhi namna hiyo? Au je angefanya kazi? Jibu ni jepesi kabisa kwamba asingefanya kazi kabisa!!!

Kama mfanyakazi wa kawaida hufanya kazi zake kwa mateso mengi akitarajia kulipwa mshahara,Je si zaidi sana kwako amvaye umeokoka na unapitia mateso fulani kwamba utavikwa taji isiyoharibika?


Hivyo basi usife moyo katika hilo jaribu,au hilo unalopitia wewe jua kwamba Mungu ni mwaminifu. Tena usiache kuomba hata kidogo kumbuka neno hili; “ Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.” 1 Wakorintho 10:13


Endelea kuwa mwenye haki/kuwa na mausiano mema na Bwana Mungu wako,kwa maana hayo mateso ni mtaji wa maisha yako ya baadae.


Hakuna jambo lisilo na mwisho,hata hivyo yote hayo yana mwisho lakini upo mwanzo mzuri kwako. Utavikwa taji uzipozimia moyo.


Kwa msaada zaidi na maombezi piga sasa kwa +255 683 877 900


Mch.Gasper Madumla.


What’s app ni +255 746 446 446


UBARIKIWE

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page