top of page

MATENDO YA MITUME ~ 02.

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi,

03. Safari za Paulo.

a) Safari ya kwanza ya umisheni wa Paulo / Paul’s first missionary journey

Kanisa la Antiokia lilipokutanika kwa ajili ya kumfanyia Bwana ibada,ndipo Roho mtakatifu aliposema, “ “...Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia. Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao“ Matendo 13:2b-3. Kisha Roho mtakatifu akawapeleka na huko walikuwa na mtumishi wao Yohana (Marko) na hapo ndipo safari ya umishionary wa Paulo ukaanza. Hivyo, washonary waliohusika ni Barnaba,Paulo na Yohana Marko. Safari ilihusu maeneo yafuatayo;

  1. Mji wa Seleukia ( Kutoka huko wakasafiri katika Salami,pamoja na Kipro,) – 13 4-5. Na huko ndipo liwali mmoja aliokoka na kutoka huko ndiko jina la Paulo lilipoanza kutumika rasmi ( kwa maana alikuwa akiitwa Sauli) 13:9.

  2. Perge ( Marko akawaacha waendelee,yeye akarudi Yerusalemu) – 13:13

  3. Paulo akahubiri huko Antiokia – 13:14-41

  4. Huko Ikonio – 13:51

  5. Listra ( Paulo akapigwa mawe) – 14:8-19

  6. Derbe ( huu ndio mji wa mwisho wa Paulo kuutembelea katika safari yake ya kwanza) 14:20

  7. Kurejea Antiokia – 14:21-26.

Kumbuka;

Katika safari ya kwanza ya Paulo, haikuwa ya kawaida kwa maana alikutana na pingamizi nyingi kama vile kupigwa kwa mawe,ili kusudi adui asitishe safari hizo za umisheni. Katika mji wa Derbe,injili ilihubiriwa sana,na mafundisho mengi. Kazi ya injili haikufanywa na mtu mmoja tu,bali ilifanywa kwa pamoja lakini kiongozi mkuu alikuwa ni Roho mtakatifu. Katika muktasari ; safari hii ya kwanza ilijumuisha sura ya 13:3-4 hadi 14:21-26. Ni kana kwamba ilikuwa safari fupi hivi,lakini ukweli ni kwamba haikuwa safari fupi kwa maana miji yote ya safari hii ya kwanza haikuwa na makanisa ya awali,isipokuwa ndio kwanza walianza kulisikia Neno la Kristo.

b) Safari ya pili ya umisheni wa Paulo / Paul’s second missionary journey.

Katika mwisho wa safari ya kwanza, kulitokea hali ya sintofahamu kutoka kwa Wayahudi walioshuka na kufundisha watu wanaoamini kwamba hawawezi kuokoka ikiwa kama wasipotahiliwa kama desturi za Musa. Swali lilikuwa ni zito,hata kupelekwa Yerusalemu kwa mitume ili kupata ufafanuzi zaidi. Katika safari hii,tunaona kwanza hali ya kutokukubaliana kati ya Paulo na mtendakazi mwenzake Barnaba.( 15:41). Maeneo yaliyohusika na safari ya pili ya Paulo, ni kama ifuatavyo;

  1. Shamu na Kilikia – 15:41

  2. Listra ( Timotheo akaungana na kundi la umisheni) 16:1-3

  3. Frigia na Galatia -16:6

  4. Paulo akitokewa na maono huko Troa – 16:9

  5. Huko Filipi / phillipi ( Mwanamke mmoja aitwaye Lidia pamoja na mkuu wa gereza waokoka) 16:13-34

  6. Kanisa la Wathesalonike likaanzishwa – 17:4

  7. Waberoya,watu waungwana wakutana na Paulo 17:11-12.

  8. Mji uliojaa sanamu uitwao Athene 17:16-33

  9. Korintho / kunzishwa kwa kanisa huko 18:1-18

  10. Kuzuru Efeso kwa kitabo kidogo 18:19-20

  11. Kurejea tena Antiokia 18:22

Kumbuka;

Akiwa huko Thesalonike,kwenye sinagogi la Wayahudi. Paulo alichukua takribani sabato tatu akihojiana na kwa maandiko dhidi ya Wayahudi. Hata hivyo mateso yao yalimsukumia Paulo hata Beroya ambapo huko Beroya alokutana na wanafunzi walioamini Neno. Watu hawa walikuwa ni waajabu kwa maana waliketi kwenye neno na kulichunguza.

c) Safari ya tatu ya umisheni wa Paulo / Paul’s third missionary journey.

Safari hii hujulikana kuwa ni safari ya mwisho ya Paulo. Lakini haina maana kwamba umisheni wake pamoja na watenda kazi wenzake waliishia hapo,kwa sababu kuna umisheni kama ule uliofanyika Yerusalemu,Kaiseria,na hata huko Rumi. Safari hii inajumuisha kazi zifuatazo ( kwa ufupi)

  1. Galatia na frigia ( Akiwahimarisha wanafunzi) – 18:23

  2. Efeso ( Alikutana na wanafunzi wa zamani wa Yohana mbatizaji ambao walijua ubatizo wa Yohana tu. Lakini pia alikaa huko miaka 2 na nusu,akipiga kazi ya injili kwa viwango vya juu – 19 yote

  3. Makedonia na Uyunani 20:1-2

  4. Safari ya siku tano,wakakaa wiki moja huko Troa – 20:6

  5. Sherehe ya wazee wa kanisa ya kumwaga Paulo kwenye kanisa la Efeso -20:17-35

  6. Huko Tiro 21:1-4

  7. Na kumalizia safari katika nyumba ya Filipo muhubiri wa injili huko Kaisaria – 21:8

ITAENDELEA…

Ikiwa umebarikiwa nifahamishe tumtukuze Mungu pamoja. Kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga kwa +255 683 877 900

Na.Mch. G.Madumla

Whatsapp namba +255 746 446 446

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page