top of page

MATENDO YA MITUME ~ 01.

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi,

Kitabu cha matendo ya mitume ni kitabu cha ajabu na cha kuvutia. Mwandishi ni “ Luka” anaitwa ni “ tabibu mpendwa“. Kwa maana Luka alikuwa ni tabibu/daktari ( Wakolosai 4:14). Injili ya Luka na matendo zote zimemwandikia Theofilo 1:1,zinaendana. Wazo kuu la matendo ya mitume ni kueleza kiundani kuhusu maendeleo ya kanisa la kwanza tokea hapo Kristo alipopaa mpaka kufungwa kwa Paulo huko Rumi.

Lakini haikuwa tu kuonesha maendeleo ya kawaida,isipokuwa namna vile Roho mtakatifu alivyohusika kuliimarisha. Lakini hata hivyo matendo ya mitume huwezi ukaisoma bila kumzungumzia mtume Paulo ambaye hakuwa katika mitume 12 wa Yesu,kupitia matendo ya mitume tunaona huduma yake katika mwanzo kabisa akianzia kuitwa kwake.

Kitabu kina mgawanyiko wa sehemu mbili.

01. Kipindi cha huduma za umisheni wa nyumbani.

Hapa tunazungumzia Yerusalemu kama kitovu kikuu cha huduma. Kazi kuu ilikuwa kwa Wayahudi,mtume Petro hasa ndiye aliyeitwa kwa waliotahiliwa. Katika kazi hii ya kwanza tunaona yafuatayo;

(a)Matukio ya awali ( maandalizi)

  1. Agizo la kuwafikia walio karibu na walio mbali ( 1:4-8)

  2. Kupaa kwa Bwana ( 1:10-11)

  3. Kushuka kwa Roho mtakatifu ( 2:1-4)

  4. Kujazwa Roho mtakatifu/ ubatizo katika Roho mtakatifu (2:4,4:31)

02. Huduma ( kazi imeanza)

  1. Huduma ya Petro – Mahubiri ya kwanza ya Petro/ kazi ya kwanza ya Petro katika siku ya pentekoste. Zao la kwanza watu 3000 wakaokoka ( 2:14-40). Mahubiri ya pili ( 3:13-26). Na zao la tatu jingine watu 5000 wakaokoka ( 4:5-12)

  2. Huduma ya Stefano – 7:1-6 ( Bwana amkusudia Sauli / Paulo aokoke)

  3. Huduma ya mwinjilisti Filipo pamoja na Petro mtume – ( 8:5-25)

  4. Huduma ya Filipo mwenyewe ( 8:26-40)

Mambo muhimu ambayo kanisa la kwanza la Bwana yaliyotokea.

  1. Ukuaji / ongezeko

  2. Kujazwa Roho mtakatifu (4:31)

  3. Umoja katika Bwana ( 4: 32-37)

  4. Kuchaguliwa / uongozi ( 6:1-6)

  5. Ghadhabu ya Bwana akifundisha kwa vitendo kwa kulinda msingi wa kanisa / kuiondoa dhambi kanisani ( 5:1-10)

  6. Maombi ndani ya kanisa (1:14)

  7. Mateso kwa waamini – ( 4:1-3,17-22;5:17-18;8:1-3,9:1 n.k)

Kwa kuyaangalia hayo machache,utagundua ndio hayo hayo yanayotokea leo kwenye kanisa la Bwana. Kwa mfano “mateso” ; katika nyakati hizi za mwisho,yapo pia mateso kwa watu wa Mungu ndani ya kanisa. Kuna watumishi wakifungwa au hata kuuwawa kwa ajilk ya Kristo. Lakini hata hivyo kanisa la leo limekosa jambo moja la msingi nalo ni “umoja“. Angalia hapo,unaona umoja ulivyochukua nafasi ndani ya kanisa, watu wote walikuwa pamoja kwa umoja. Lakini sasa kila kanisa linajiendea kimpango wake,hata waamini ndani ya kanisa moja tu wamekosa umoja.

02. Kipindi cha huduma za nje.

Kanisa likatoka kuanzia Yerusalemu kama kitovu kuelekea Antiokia na Shamu. Na huko ndiko tunakoona matendo makuu ya Roho mtakatifu kuonesha kwamba yupo halisi,tena akitenda kazi. Katika kipindi hiki,tunayaona matukio matano kama ifuatavyo;

01. Tukio la awali la huduma za nje / matukio ya kwanza.

  1. Huduma ya Filipo katika Samaria ( akishabiana na Petro na Yohana) – 8:5-25

  2. Kuokoka kwa Sauli hata kuwa mtume Paulo ( 9:1-30)

  3. Huduma ya Petro kwa wamataifa huko Kaiseria ( 10:1-43)

  4. Barinabas katika huduma huko Antiokia ( mwakilishi wa kanisa la Yerusalemu) 11:22-24

  5. Antiokia “wakristo wa kwanza kuitwa” Barnaba alimleta Paulo wakashirikiana na kufungua huduma ( 11:25-26)

02. Kutumwa kwa Paulo na Barnaba kama wamisionary kutoka kanisa la Antiokia. Lakini Yohana Marko akaambatana nao ( 13:1-5)

03. Safari za mtume Paulo.

Paulo alikuwa na “safari tatu kubwa” za huduma yake. Hata hivyo katika safari zake hakuwa peke yake bali alikuwa na watenda kazi pamoja naye. Mmoja kati ya watenda kazi mkubwa kuliko wote alikuwa ni Roho mtakatifu ambaye kwa hiyo aliongoza safaru nzima. Bila huyo,safari zote za Paulo hazingekuwa na maana yoyote ile,wala pasingekuwa na matokeo yenye maana. Hata sasa,bado tunaona umuhimu wa kuwa naye Roho mtakatifu katika safari za huduma zetu.

Tunaona matendo, ishara na ajabu kubwa zikifanyika katika safari zote za akina Paulo na wenzake wachache,lakini ukweli ni kwamba mbele na nyuma yao alikuwepo Roho mtakatifu akizitenda zote,na wao wakaonekana kana kwamba ndio watendao. Lakini waliwaeleza wazi wazi kwamba si wao watendao,bali ni Mungu ndiye atendaye…

ITAENDELEA…

Ikiwa umebarikiwa nifahamishe tumtukuze Mungu pamoja. Kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga kwa +255 683 877 900

Na.Mch. G.Madumla

Whatsapp namba+255 746 446 446 .

UBARIKIWE.

Comentários


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page