MAOMBI / PRAYERS~MWISHO.
- Mch. Gasper Madumla
- Sep 9, 2016
- 3 min read

Na Mch.G. Madumla.
MATOKEO YA MAOMBI / FAIDA ZA MAOMBI.
Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi,
Kawaida kabisa,maombi yana matokeo mazuri siku zote,kwa maana hakuna kupoteza katika maombi wala hakuna hasara katika maombi. MIongoni mwa matokeo y maombi ni kama ifuatavyo;
(i) Kuvikwa silaha na nguvu za kupambana na ulimwengu wa giza.~ Ikumbukwe ya kuwa vita vyetu si juu ya damu na nyama bali ni juu ya falme na mamlaka,juu ya wakuu wa giza hili na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho( Waefeso 6:12). Mwombaji akiomba mara kwa mara,Mungu humvika guvu za umbambanaji zisizo za kawaida. Jaribu sasa uone itakavyokuwa.
(ii). Kukuza imani~ Pamoja na kwamba imani huja kwa kusikia Neno la Kristo,lakini katika maombi,imani inakuzwa. Mfano; Chukulia ulikuwa ukiomba juu ya jambo fulani zito,halafu gafla Bwana akakutendea,basi hapo ujue kiwango chako cha kumwamini Mungu kitaongezeka mara mbili ya kile cha kwanza.
(iii). Huleta ajabu na miujiza ya kweli.~ ( Mathayo 7:7) Biblia imeeleza wazi wazi kwamba “ombeni nanyi mtapewa…” Hii ikiwa ina maana kila aombaye amepewa ahadi ya kupewa. Miujiza ya kweli imefichwa kwenye maombi katika jina la Yesu Kristo. Ukitaka kumuona Mungu akikutendea makuu mpaka ushangae,basi ishi maisha ya maombi,na hapo utaiona miujiza mingi sana.
(iv). Lango la kuja kwa Kristo ~ Maombi ya toba hutuleta kwa Kristo na hatimaye tunaokoka. Lakini ni kazi ya maombi hiyo.
(v). Huleta ujasiri wa kukabili msalaba (Au changamoto).~ (Luka 22:40). Ni kawaida kwa kila mwombaji kupata ujasiri wa kuvuka kila jaribu apitialo kwa sababu tu ya maombi ayafanyayo. Yesu naye wakati alipoomba alipokea nguvu,ili kuukabili msalaba. Wewe Je msalaba wako ukoje?
(vi). Kanisa linaimarishwa.~Kanisa haliwezi kuwa imara likikosa maombi moto moto. Kila kanisa la Kristo linapaswa kuegema katika maombi ya kumaanisha kwa maana vita bado ipo.
(vii). Tunapata kumsikia Mungu na maelekezo yake.~ Kwa kuwa maombi ni “mazungumzo kati yetu na Mungu” kwa njia hiyo tunapata nafasi ya kusikia kile asemacho Mungu. Mfano;ukiwa ni mwombaji mzuri kuna kipindi weweza kusikia sauti ya Mungu na maelekezo mbali mbali ya kikanisa,kijamii na hata kitaifa na unaambiwa uyafanyie kazi. Mtazame Ibrahimu ( Mwanzo 18:1-33)
(ix). Tunapokea majibu,na uhakika wa maisha ya sasa na ya baadae.~Tukiomba; Bwana hutujibu;mwombaji uweza kuyaona mambo ya sasa lakini pia kuweza kuyaona yale ya baadae katika ulimwengu wa roho. Hivyo huwa na uhakika wa sasa na wa baadae. Ni ili ni jambo jema sana.
11.ATHALI ZA KUISHI BILA MAOMBI.
(i) Kuvamiwa mara kwa mara na nguvu za giza.~ Watu wengi leo wanaishi maisha ya kuonewa na kuteswa kwa nguvu za giza. Wanateswa hivyo sio kwa sababu hawendi kanisani,bali wanaenda na wengine wameokoka kabisa lakini shida yao ni kwamba hawaombi,wao huenda kanisani kama desturi. Usimpe nafasi ibilisi kwenye maisha yako kwa kuishi bila mfumo wa maombi kila siku.
(ii) Kukosa imani ya kweli.~ Kwa sababu maombi yamekosekanika kabisa,humfanya mtu akose pakushika katika imani yake. Anaamini kidogo sana,lakini hawezi kumuamini Mungu katika viwango vya juu,sababu ndani yake asemi na Mungu. Maombi yakikosekana ni hatari sana.
(iii) Kukwama katika mambo mengi kimaisha.~ Mambo mengi yanakwama,kila ukipangacho hakiendi au kama kitaenda basi ujue ni kwa kitambo tu,then kinakwamba kwa sababu hakuna nguvu ya kusukuma kiende. Usione mambo mengine yanafanikiwa ukadhani yanaenda yenyewe,Hapana! Imo nguvu inayosukuma yaende. Ukiona kwako mambo yako hayaendi,rudi kwanza ujiulize na kujikagua katika kipengele cha “ maombi” je wewe ni mwombaji kweli?
(iv) Kupambana kwa jinsi ya mwili zaidi kuliko kiroho.~Nimeshuhudia watu wengi wanaoishi bila mfumo wa maombi wakipambana kwa kutumia nguvu za mwilini wala si za rohoni. Hii ni hatari kabisa! Ukimuona mkristo yeyote anatumia nguvu zake za mwili zaidi ya kutumia za rohoni basi ujue huyo si mwombaji. Laiti kama ni mwombaji ni lazima ataongeza nguvu za rohoni na mpenyo utaonekana tu.
(v) Kukosa imani ya kushinda .~Watu wengi wasioishi maisha ya maombi ndio wa kwanza kuona wanashindwa kabla ya kushindwa kwenyewe alafu,wakianzisha jambo hawafikagi mwisho ni lazima wanakata tamaa wakiona kwamba haiwezekani. Hii ni mbaya sana!
(vi) Kushindwa kuelewa nyakati ulizopo.~Ukiwa sio mwombaji,basi utaona kila kitu ni sawa tu,hata kama utaona kuna mikwamo fulani,basi utajua ni Mungu ndio amekukwamisha. Hujui kwamba yupo shetani anayesababisha hayo yote,wewe unalidhika haraka haraka kwa maana hujui ni wakati gani upo. Shughulikia hilo,jiulize kwa nini imekuwa hivyo kisha chukua hatua ya kuomba mbele za Mungu akuoneshe yale yaliyojificha ( Yeremia 33:3)
(vii) Kuishi maisha ya kutosamehe,(maisha ya visasi)~ Sheria ya jino kwa jino ( Kutoka 21:24) ni ya wale watu wa mwilini wasioishi maisha ya maombi.
(viii) Kushindwa kutofautisha kazi ya Mungu na ya shetani.~ikiwa huna utaratibu wa kuzungumza na Mungu mara kwa mara,huwezi kuijua sauti yake. Utashindwa kujua lipi ni la Mungu na lipi ni la shetani. Chukua hatua sasa,anza kuishi maisha ya maombi.
Waweza nipigia sasa tuweze kuomba pamoja,maana inawezekana hata kiu ya maombi imekosekana kwako,basi tushirikishane kuomba pamoja. Piga kwa;
Kwa huduma ya maombezi piga sasa; +255 683 877 900
What’s app +255 746 446 446
MWISHO.
Mchungaji G.Madumla.
UBARIKIWE.
Commentaires