MAOMBI / PRAYERS~12
- Mch. Gasper Madumla
- Aug 11, 2016
- 5 min read

Na mchungaji Madumla.
Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi,
Kuna baadhi ya vizuizi/pingamizi katika maombi. Pingamizi hizi zinaweza kuletwa na Ibilisi au wakati mwingine mwombaji anaweza akajiwekea mwenyewe pingamizi kwa kujua au piasipo kujua. mfano baadhi tu ya pingamizi/vizuizi hivyo ni kama ifuatavyo;
(i) Dhambi tunazoendelea kutenda.
Tunafahamu ya kwamba dhambi ni ukuta wa kukuzuia kuomba,tena hata kupoteza imani ya kupokea kile ukiombacho. Kuna dhambi ambazo zimewangangania watu,kwa sababu watu hao kwanza hawajaamua (kuziacha wanazipenda). Na kwa sababu hiyo,dhambi husimama kama ukuta mkubwa wa kukwamisha maombi. Ebu chunguza hili kwenye maisha yako! “lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.” Isaya 59:2
Mfano mdogo ni huu; chukulia wewe ni mfanyakazi fulani kwenye kampuni fulani,kisha unahitaji kumuomba jambo fulani boss wako,labda tuseme unataka umuombe apitishe maombi yako ya kwenda kusoma,lakini ile unaingia tu ofisini mwake kabla hujamsalimia,gafla anageuka upande wa pili na kiti chake cha kuzunguka kwamba hataki kukuona,akipindukia ukutani;tena asitake kukusikiliza.
Kinachofuta unajua ni nini? Utaondoka mwenyewe kwa maana boss wako ameuficha uso wake asikusikilize ingawa hitaji lako lipo ndani ya uwezo wake. Na hali ndivyo ilivyo kwa mtu mpenda kutenda dhambi kinyemela kinyemela yaani ukimtazama juu juu anaonekana ni mtakatifu,lakini kumbe ni mwenyekiti wa kutenda dhambi kwa maana anazipenda kila atendapo.
Kumbuka sisemi kwamba mimi ni mtakatifu zaidi yako,lah! Bali kile nikisemacho hapa ni kwamba,wapo watu wenye kupenda kuzikumbatia dhambi na hawana haja ya kutubu na kuziacha. Sasa lazima uchukue maamuzi makubwa ya kuacha dhambi kwa maana mengine yapo katika uwezo wako.
Mfano;utakuta mwombaji ni mzinzi kifogo,msengenyaji kidogo,mwenye hasira,mnafiki,mvutaji sigara au pombe N.K papo hapo mtu huyo utakuta akimuomba BWANA amuinue katika karama yake,au ampe karama. Sasa,swali huyo Roho mtakatifu aje akae wapi ndani ya mtu huyo? Kwa maana nyumba(mwili) yake imekwisha jaa!! Umeona?
Ni jambo la kuaminika tena lafaa kuhubiriwa kwamba;“ Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.” 1 Yoh.2:15
Kwa sababu hiyo ya kupenda dunia na mambo yake,maombi ya wengi hayajibiwi. Na kufanya watu kujiuliza kwamba,kwa nini hawajibiwi? Au kwa nini kuna shida kubwa sana wakati wa maombi? Jibu ni jepesi kabisa;jikague mausiano yako na Mungu;yapo sawa? Utagundua kwamba mausiano yako na Mungu hayako sawa,thus unateseka kujibiwa maombi yako.
Tujifunze kwa Yesu Yeye aliyekuwa asilimia mia moja Mungu,na asilimia mia moja mwanadamu lakini hakutenda dhambi. Mausiano ya Yesu na Mungu wake yalikuwa mazuri kiasi kwamba walikuwa wakielewana. “Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile.” Yoh.5:19
Ifike wakati tumuogope Mungu,maana Mungu hadhiakiwi wala Yeye sio wa michanganyo. Ukiamua kutumika kwake,basi amua kweli kweli,yaachilie yote ya dunia na tamaa zake kwa maana dunia na vyote vinapita tu.
(ii) Kushindwa kusamehe wakosa wako.
Hii pia ni sababu kubwa sana inayowazuilia wengi washindwe kuomba ipasavyo am hata kujibiwa maombi yao. Biblia imeeleza wazi wazi kabisa kuhusu mtu yeyote asiyesamehe na yeye hatasamehewa pia (Mathayo 6:14-15). Kuna watu ambao wameshindwa kuwasamehe wakosa wao,kwa kisingizio kwamba wameumizwa sana hali hawajui na wao hawatasamehewa. Chukulia kwamba umemshikilia mtu moyoni mwako kwa muda fulani hivi,nawe papo hapo unaomba Mungu akuonekanie kwenye mambo yako. Nakumbia hataonekana kwako,kwa maana wewe pia hujawasamehe wengine.
Hii ni kazi ya shetani kuweka uchungu ndani yako kwa sababu tu ya makosa madogo madogo ili na wewe usisamahewe akupate vizuri. Kuna kipindi unaweza ukafikili umelogwa,lakini ukweli ni kwamba shida kumbe ni wewe mwenyewe hutaki kuwasamehe wale waliokukosa.
Sasa jaribu kujihoji nafsi yako uone kwamba kama kuna mtu yeyote umemshikilia moyoni,kisha muachilie,kisha ndipo sasa uombe. Nami nataka nikuambie utaona mabadiliko makubwa ikiwa utafanya hivyo.
(iii) Kuomba vibaya.
Moja wapo ya sababu ya kutojibiwa maombi ya wengi ni vile waombavyo,wengi huomba vibaya. Kuomba vibaya ni pale muombaji anapoomba kinyume na mapenzi ya Mungu. Mfano neno linasema wapendeni adui zenu,waombeeni wanaowaudhi (Mathayo 5:44). Lakini mtu huomba kifo kwa adui zake na wale wote wanaomuudhi.
Jamani!kwani kwa nini usimuombee mema adui yako ili abadilike awe upande wa Bwana. Tena akiishi; ili aweze kukuona unavyongara na Bwana. Biblia inasema; “ Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu” Yakobo 4:3
Kwa sababu shetani yupo,anaweza akayatimiliza maombi mabaya uombayo,nawe usijue kama upo upande wa shetani. Kwani ni mara ngapi wakristo huomba kinyume na matakwa ya Mungu nao hupata? Mfano mtu anaweza kuomba kwamba mwenzake afukuzwe kazi,lakini badae kweli hufukuzwa kwa sababu ipo roho ile ya giza ikifanya kazi kinyume na Mungu,
Jitahidi siku zote kuomba sawa sawa na mapenzi ya Mungu.
(iv) Kukosa subira.
Waombaji wengi wanakinzana na kizuizi hiki,kwa maana waombapo hupanga kabisa muda wa kupokea majibu yao kitu ambacho kiimani sio vibaya,lakini lazima tujue kwamba huwezi kumpangia Mungu akujibu utakavyo hata kama uliomba. Sasa wengine hawana muda wa kusubiri majibu ya Bwana na hatimaye hujikuta wakitafuta njia zao pale wanapoona kana kwamba Mungu amechelewa kuwajibu,lakini wanasahau neno hili kwamba Mungu hawahi wala hachelewi kutimiza ahadi zake – 2 Petro 3:9. Pia tunapaswa tunyenyekee tu,wakati wake ukifikaatatujibu maana biblia inasema tena ;“ Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake;” 1 Petro 5:6
Neno “nyenyekeeni” maana yake “endelea kushuka,endelea kuwepo uweponi mwa BWANA” Ili wakati wake akunyanyue mahali ulipo. Nikisomaga andiko hili ninahisi kupata nguvu ya kusonga mbele nikijua kwamba kuna wakati wa Bwana wa kupandishwa kwangu.
Je hivi unajua hata Daudi alipopakwa mafuta hakuwa mfalme siku hiyo hiyo? Bali aliendelea kuwahudumia ndugu zake kama mtoto wa kawaida,lakini nataka nikuambie ulipofika wakati wa Bwana Sauli alishindwa kumzuia Daudi,naye akawa ni mfalme.
Hata leo,waweza kutafuta nafasi fulani usipate,basi usilazimishe kutumia akili zako mwenyewe bali endelea kuwa uweponi kwa maana upo wakati wa BWANA,ukifika huo hakuna awezaye kuzuia,hata kama itakuwaje,Bwana akikuinua amekuinua tu…
(v)Upungufu wa imani.
Neno “pungufu “maana yake isiyotimilika,iliyopungua. Hivyo imani pungufu ni imani haba,ni imani yenye mashaka fulani. Upungu wa imani ni mojawapo ya sababu kubwa inayozuia majibu ya maombi yetu. Haimanishi mtu mwenye imani haba hana imani,hapana;
mtu mwenye imani haba ni yule mwenye imani lakini hana uhakika ya mambo anayoyatarajia. Tujikumbushe habari ya wanafunzi wa Yesu waliposhindwa kupata majibu yao kwa sababu ya ungufu wa imani.
“ Nikamleta kwa wanafunzi wako, wasiweze kumponya.Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu…“Mathayo 17:16 & 20a
Wanafunzi wa Bwana,walikuwa na imani lakini imani yao haikuwa na uhakika wa uponyaji;hawakuweza kumponya kwa sababu hiyo. Waombaji wengi wamekwama eneo hili,kuomba wanaomba lakini hawaamini sana kile walichoomba.
Utakuta mwombaji anaombea kuhusu ndoa yake,lakini alafu anajiuliza “ hivi kweli mume wangu atabadilika? Mmhh yaani naona haitawezekana,maana kila kukicha ni ugomvi...”
Kwa mfano huo,inaonesha kwamba muombaji ana mashaka na uponyaji wa ndoa yake. Sasa angalia kile kinachotokea,majibu hayaji kwa maana mwombaji amejawa na mashaka.Hivyo kuwa na imani haba ni changamoto kubwa sana wakati wa maombi. Hakikisha una imani timilifu pale uombapo,amini kwamba kile ukiombacho umepokea tayari.
(vi) roho ya mazoea
Kuna watu wamezoelea wokovu kiasi kwamba suala la maombi halina maana sana kwao,hivyo wanaweza kweli wakaomba,lakini kuomba kwao kukawa kwa kawaida kawaida fulani hivi,yaani tofauti ni walipokuwa wakiomba mwanzoni. Ukiona watu wa namna hii,basi ujue kinachowasumbua ni ile roho ya mazoea.Nayo hiyo roho ni kikwako kikubwa sana katika maombi yao. Ukitaka ufanikiwe katika wokovu hasa wakati wa maombi,basi epuka kuzoelea wokovu.
Kwa huduma ya maombezi piga sasa; +255 655 111 149,+255 683 877 900 ( What’s app+255 655 111 149)
ITAENDELEA…
Mchungaji G.Madumla.
UBARIKIWE.
Comments