MAOMBI / PRAYERS~09
- Mch. Gasper Madumla
- Jul 26, 2016
- 3 min read

Na Mchungaji Gasper Madumla.
(VI) MAOMBI YA MAPATANO/UMOJA.
Siku zote umoja ni nguvu. Maombi ya mapatano ni maombi ya kiagano kati ya pande mbili au zaidi. Haya ni maombi yanapaswa kufanyika kwa umakini sana kwa maana nguvu ya maombi haya hutegemea mapatano yenu.Hatari ya maombi haya ni kubwa pale mmoja wenu au baadhi yenu watakapoenda kinyume cha mapatano yenu,hapo mtapigwa na adui.!!!
Mfano ; chukulia kwamba mmekubaliana mfunge siku 7 na mkutane kwenye maombi kila siku muda fulani,lakini ikatokea mmoja wenu au wawili wenu wakawa wanadanganya/wanachiti kama vile wamefunga lakini hajafunga wala hawapo na ninyi katika maombi,hali ya namna hii itawaangusha.
Unajua kwamba,Mungu uheshimu sana mapatano tunayojiwekea. Lakini tukiwa kinyume na mapatano yetu wenyewe basi hapo ndipo tunapotengeneza hatari/mwanya wa kutokusikilizana. Mfano wa maombi haya tunayaona kipindi cha Esta kwenye kitabu cha Esta sura 4:16,alipotangaza mbiu ya kufunga kwa Wayahudi wote. Yalikuwa ni maombi ya mapatano kwa Wayahudi wote,lakini pia tunaona vile Danieli akiingia kwenye maombi na wenzake katika Danieli 2 baada ya Nebukadreza kutaka kuwaangamiza wenye Hekima.Maombi ya mapatano ni Muhimu kuwa na nia moja/lengo moja.
“ Ndipo Danieli akaenda nyumbani kwake, akawapasha habari kina Hanania, na Mishaeli, na Azaria wenzake;ili waombe rehema kwa Mungu wa mbinguni kwa habari ya siri hiyo, ili kwamba Danieli na wenzake wasiangamizwe pamoja na wenye hekima wa Babeli.” Danieli 2:17-18
Andiko hili linatupa picha ya kwamba akina Danieli walinia mamoja katika maombi yao. Walifanya maombi ya mapatano ambayo Mungu alionekana akimjibu Danieli. Si kana kwamba Danieli alikuwa hawezi kuomba yeye mwenyewe,la! bali alikuwa anajua nini faida ya maombi ya umoja.
Je kwa nini maombi ya mapatano? Kwani Mungu hakusikii pale uombapo peke yako?
Tukumbuke jambo hili,Mungu huangalia moyo wa mwombaji na wala haangalii idadi ya waombaji. Hii ikiwa na maana kwamba Bwana Mungu husikia maombi yako binafsi ukiomba katika moyo.
Pia,kumbuka kwamba imo nguvu kubwa pale mfanyapo maombi ya mapatano ikiwa wote mpo rohoni na mpo na muambatano wa roho;yaani kile ulichonacho kinashabiana na mwenzako au wenzako (lakini isiwe wengi,mara nyingi ni wachache). Tazama vile Bwana Yesu akisema;
“Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.“Mathayo 18:19
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA MAOMBI HAYA;
(a) Usafi wa kiroho kwa wale watakao patana katika maombi~ kama utapatana na mwezako msimame katika nia moja ya maombi,basi hakikisha kwanza wewe uwe na usafi wa rohoni pia mwanzako lazima awe na usafi wa rohoni la sivyo ni bora msipatane.
Mfano;Chukulia mpo katika mfungo wa siku tatu wa maombi wewe na mwenzako mkiombea ajenda fulani kwa kumaanisha lakini papo hapo mwenzako akakosa uaminifu akawa ni muongo akijifanya anafunga huku anakula kinyemela nyemela pale mnapokuwa mmeachana kila mmoja anarudi kwake. Hapo maombi yenu ni sawa na bure kwa sababu mmoja amekosa uaminifu katika patano lenu.
(b) Hakikisha wewe huna kinyongo na mtu yeyote yule(hujamshikilia mtu yoyote yule,umesamehe wote) na mwenzako ni vivyo hivyo. ~Ukiomba huku humemshikilia mtu ndani ya moyo,basi ni heri usingeliomba hata mwenzako naye ni vivyo hivyo ni lazima awe safi. Muombe toba kabla ya kuanza maombi yenu.
(c) Hakikisha mnaelewana vizuri katika semi zenu. ~Yaani isiwe wewe unasema hivi,yeye anasema vile au mara mwenzako anakupinga anataka ya kwake tu ndio yasikilizwe na kufanyiwa kazi. Au isiwe anayakubali ya kwako kishingo upande,yaani ~afanyeje aah basi tu!
(d) Wote wawili mkubali kuongozwa na Roho mtakatifu. Mjishushe wote wawili na kumruhusu Roho mtakatifu atawale.Epuka story nyingi,zitazuia uwepo wa Bwana.
(e) Ni vyema muwe mnafunga kwa maombi. Kwa maana ikiwa mtaaitabisha miili yenu kwa kuinyima chakula basi ni dhahili mtaweza kuwa pamoja kwa umoja.N.K
ITAENDELEA…
Kwa maombezi,piga sasa +255 683 877 900.
What’s app ni+255 746 446 446
MchungajiG.Madumla.
UBARIKIWE.
コメント