MAOMBI / PRAYERS~08
- Mch. Gasper Madumla
- Jul 21, 2016
- 3 min read

Na Mch.Gasper Madumla.
(V) MAOMBI YA NADHIRI.
Neno nadhiri ni ahadi. Hivyo Maombi ya nadhiri ni aina ya maombi ya kuweka ahadi mbele za Mungu. Mfano “Ee Mungu naomba unisaidie kupata kazi nzuri,nitakapoipata kazi hiyo basi mshara wangu wa kwanza wote nitakupa wewe/au nitatoa 500,000 kwa ajili ya kazi yako hapa kanisani ninapoabudu…” Ahadi hizo unazoziweka pale Bwana atakapokutendea huitwa nadhiri.
Biblia inasema nini juu ya maombi ya nadhiri?
Neno la Mungu linaeleza juu ya watumishi ambao walimwekea Bwana nadhiri,mfano mke wa Manoa alimwekea Bwana nadhiri ya kumtoa mwanaye Samsoni kwa Bwana,Pia Hana alimwekea Bwana Nadhiri kwa kumtoa mwanaye Samweli
“ Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamwomba BWANA akalia sana.Akaweka nadhiri, akasema, Ee BWANA wa majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo mimi nitakapompa BWANA huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikilia kichwani kamwe.” 1 Samweli 1:10-11
Je maombi haya yapo mpaka leo?
Lakini ni muhimu kuzingatia kwamba Neno linasema ni afadhali usiweke nadhiri kama huwezi kuiondoa kwa maana hugeuka dhambi. Tumeshuhudia mara nyingi watu wakiweka nadhiri kwa Mungu tuwapo kanisani,na kwa sababu hii;watu wengi wamefungwa kwa sababu wengine wameshindwa kuzitoa au kuzitimiliza. Biblia inasema;
“ Utakapoweka nadhiri kwa BWANA, Mungu wako, usiwe mlegevu katika kuiondoa; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, hataacha kuitaka kwako; nayo hivi itakuwa dhambi kwako.” Kumb.23:21
Kumbe ni dhambi kwa yule aliyeweka nadhiri kisha hakuiondoa. Ni heri usingeliweka maana haitakuwa dhambi kwako( Kumb.23:22). Watu wengi leo wameingia katika dhambi hii pasipo kujua,na wengine wameingia wakijua kwamba ni dhambi.
Angalia mfano huu halisi ;katika changizo kanisani; utakuta mtu yupo mbele za madhabahu ya Bwana kisha anaahidi mchango wa kiasi kikubwa cha pesa ambacho hana uwezo nacho,ili mradi watu wamuone,wamsifie lakini ukweli ni kwamba watu wengi wa namna hii wanakuwa hawatoi hizo pesa,au la kama wakitoa basi itachukua muda mrefu sana mpaka akamilishe mchango wake.
Sasa hii ni dhambi sana,kwa nini usiweke ahadi nzuri ya kawaida ambayo roho yako inaridhika,kusudi usije ukaingia katika dhambi? Lakini wengi walioweka ahadi za pesa mbele za Bwana,si kana kwamba hawapati pesa hizo ili wazitoe nadhiri zao la hasha! Mungu ni mwaminifu Yeye huwapa pesa hizo ili waweze kutimiliza ahadi zao.
Tatizo linakuja pale,mtu anapopata pesa hizo,hula zote.Anajikuta akizila kwa matumizi mengine ambayo ni kinyume kabisa na kusudio la pesa hizo. Mfano; Umeweka ahadi ya pesa ya tshs 200,000/= alafu kwa kuwa Mungu ni mwaminifu,akaanza kukupa kidogo kidogo. Leo akakupa Tshs 50,000,/= ikapita wiki mbili,akakupa tshs 130,000/= then baada ya muda fulani hivi akakumalizia tshs 20,000/= .
Sasa angalia,pale alipoanza kukupa elfu hamsini,wewe ukamega hiyo pesa,ukajinunulia viatu. Baadae ulipopata pesa ingine,ukaona gauni zuri,ukanunua,mara ukachukua pesa hiyo hiyo ukaenda saloni kusuka N.K( na kwa wanaume ni vivyo hivyo.) Gafla ukajikuta umekosa pesa ya kulipa ahadi yako,nayo ahadi sasa hugeuka kuwa dhambi.
Ifike wakati sasa tuwe makini na semi zetu haswa tuwapo mbele za Bwana. Tuache roho ya mazoea mbele Bwana,ni dhambi mbaya sana.
Wapo watu,wala hawajalogwa,wala hakuna uchawi,wala si shetani bali wanateseka kwa sababu hawajaziondoa nadhiri zao. Hivyo hujikuta wakistrago sana katika maisha yao kwa maana wamejisahau kuziondoa ahadi na nadhiri zao walizoziweka.
Maombi haya hayafanywi kiholela olela tu!,ni lazima uzingatie yafuatayo;
(a) Uwe na akili timamu juu ya kile unachotaka kuweka nadhiri.
(b) Umuombe Roho mtakatifu akupe amani juu ya nadhiri utakayoiweka. La! Kama umekosa amani usiweke nadhiri kabisa.
(c)Ukiwa una mwenzi wako wa ndoa,au mtu wa karibu yako,basi umshirikishe ili wote wawili mkumbuke nadhiri yenu au yako.
(d)Ni lazima uandike nadhiri yako,kwa sababu usije ukaisahau na ikawa ni dhambi.
(e)Uwe mwaminifu kutoa kile ulichomuahidi Mungu. N.K
Je ufanye nini ikiwa ulimwekea Bwana ahadi na umeshindwa kuitoa?
~Jambo la kwanza kabisa,ni kufanya toba kwa damu ya Yesu….
ITAENDELEA…
Kwa huduma ya maombezi,piga sasa +255 683 877 900.
What’s app number ni +255 746 446 446
Mch.Madumla.
UBARIKIWE.
Hozzászólások