top of page

MAOMBI / PRAYERS~07

(IV) MAOMBI YA VITA


hqdefault

Na Mchungaji Gasper Madumla.


Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi..

Tafsiri nyepesi ya neno “vita” lina maana ya mapigano/mashindano/mapambano baina ya pande pili. Na katika vita kuna mawili tu,kushinda au kushindwa hakuna cha kutoka droo ( Kama ilivyo vita katika ulimwengu wa damu na nyama ndivyo ilivyo katika ulimwengu wa roho) Na ukumbe vita ni vita,hakuna vita ndogo!!!

Tabia ya vita,ni lazima kuwe na ugomvi/uchokozi au kuwe na upinzani usiowezekana kutatuliwa mpaka kupigana,mshindi ndiye atakaye muongoza mnyonge wake.  Vita yoyote ile ni lazima itumie silaha,wapiganaji na uwanja wa kupigana.

Hayo matatu ni muhimu sana katika kila aina ya vita. Lakini ikumbukwe hili; kiongozi wa vita ni muhimu sana na lazima awepo katika kila aina ya vita. Lakini mpaka vita kupiganwa ujue kuna sababu. 

Katika uzoefu wangu mdogo,sijawahi kuona mpiganaji ndani ya vita anayekata tamaa. Huwa sikuzote wapiganaji hawakati tamaa wakiamini watashinda. Kule kuamini ushindi ndiko kunakowapa nguvu ya kusonga mbele kupigana.

Labda tujikumbushe yale ya kitambo yaliyowahi kutokea katika nchi yetu katika utawala wake Mwl. pale alipotangaza kumpiga Iddi Amin dada,alisema~ uwezo,nia na nguvu tunazo za kumpiga Iddi Amini. Hii inatuonesha kwamba mpiganaji hujiamini kwamba atashinda kumpiga mpinzani wake. Kwa maelezo hayo,sasa tujiulize swali hili;

Nasi watu wa Mungu tuna vita dhidi ya ibilisi na wafuasi wake wote,lakini uzuri ni kwamba vita yetu ni ya Bwana pia kwa maana ni Yeye ndiye atupiganiaye pale tunapompa nafasi ya kwanza katika uwanja wa mapambano. Kupitia maombi ya vita / maombi ya kupambana,hapo ndipo tunapopigania na hatimaye na kushinda.Tunafanya maombi ya vita kwa sababu tunayo vita dhidi ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kumbe,kuna falme ya giza ya yule mwovu twapasa kuipiga,kuwapiga tena wakuu wa giza hili(Wachawi,waganga,majini n.k),tena tuwapige majeshi ya mapepo katika ulimwengu wa roho.(Waefeso 6:12)

Ukitambua ya kwamba,shetani yupo,naye yupo akishindana nasi basi ni lazima utangangana kujua namna ya kupambana naye katika ulimwengu wa roho. Kile ninachotaka ujue kwamba maisha yako si salama kwa maana yana vita, tena yeyote aliyeokoka ametangaza vita dhidi ya falme na mamlaka,dhidi ya mapepo. Hivyo basi huna budi kupigana!

Rejea maelezo ya vita ya hapo juu, kisha linganisha sasa;sisi wakristo tunayo vita na jeshi la shetani. Ugomvi wetu mkubwa ni kwamba yeye shetani anataka kutuangusha tumtumikie lakini sisi hatupo tayari kwa maana wakutumikiwa ni mmoja tu naye ni JEHOVA pekee.

Uwanja wetu wa mapigano ni katika ulimwengu wa roho,huku tukitumia silaha za rohoni katika maombi. Nia tunayo,nguvu tunazo na uwezo pia tunao wa kumpinga naye atatukimbia tu. Tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge,tunasoma;

Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.” Luka 10:19

Sasa,utagundua kwamba kupigana kwetu si juu ya damu na nyama bali katika ulimwengu wa roho. Tunapigana na falme ya giza na majeshi yake. Tunazo silaha za kutosha kumpiga shetani katika maisha yetu katika jina la Yesu Kristo. Lakini sharti tuwe kwa Bwana,kwa maana Yeye Bwana ndie apiganaye.

Maombi ya vita ni maombi kupambana na kila aina ya nguvu ya giza katika ulimwengu wa roho,maombi haya ujulikana pia kwa jina la “maombi ya kuvunja na kuharibu utawala wa kipepo“. Pale uonapo mambo hayaendi,pale uonapo roho ya magonjwa imeachiliwa kwako hata katika familia,ukoo N.K

pale uonapo roho za mauti ndani yako,N.K Hapo ushtuke ukijua kwamba huyo ni adui,amerusha mishale,nawe usikae kimya,amka na kupambana naye kwa njia ya maombi katika ulimwengu wa roho.

Wapo watu wasiojua undani wa maombi haya kiasi kwamba warushiwapo mishale na yule muovu,wao hudhania ni Mungu kawapiga kumbe sivyo,ni shetani tu mwenye kuvuruga maisha yao. Si kila gumu linaachiliwa na Mungu,mengi hutoka kwa shetani akikukinga usije ukafanikiwa. Leo,huna budi kumshughulikia adui yako katika maombi ya vita kwa mamlaka na nguvu ya jina la Yesu pekee na damu yake.

Siku moja,wakati naongea na mtu mmoja aliyekuwa akivamiwa na mishale ya kipepo. Aliniambia akiona wanakuja usiku yeye uamka na kumwaga maji ya baraka kisha umwaga hayo maji kwenye kona kona ya chumba chake akiamini kwamba hayo maji ya baraka yatamkinga na uvamizi wa kipepo,kisha hurudi kulala.

Sasa angalia matokeo yake;

mapepo yalikuwa yakiingia kama kawaida,na kumtesa vile wapendavyo wao. Yale maji hayakuwa na msaada wowote ule. Lakini emu jiulize sasa,kwamba shetani utamzuia kwa maji ya baraka? Kwa hiyo ni kama vile alikuwa akimbariki shetani azidi kuingia!!! Huu ni utoto kwa kweli.

Angalia shetani alivyopofusha akili za wengi,utakuta mtu anatumia maji kama ulinzi badala la jina la Yesu Kristo. Alufu naye shetani hujifanya kama vile anatoka ili yule anayetumia maji kama ulinzi wake,aamini na kumuacha Yesu mwenye nguvu. Ifike wakati sasa tutambue ya kwamba hatuwezi kulindwa na chochote isipokuwa jina la Yesu tu.

Maombi ya vita ni muhimu sana kufanywa kila wakati ili uweze kushinda vita unayopitia….

ITAENDELEA…

Kwa maombi na ushauri,usisite kunipigia sasa kwa namba hii +255 683 877 900.

What’s app number ni +255 746 446 446

Na Mch.G.Madumla

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page