top of page

MAOMBI / PRAYERS~01

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi…


Mch.Madumla.

Na Mch.G.Madumla


 “ Ilikuwa ni majira ya mchana ambapo bwana Hamisi ( mwenye nyumba) alipokuwa nyumbani kwake.Baada muda fulani kupita mpangaji wake mmoja alirudi kutoka matembezini,maana alikuwa na wapangaji wanne. Gafla,yule mpangaji akaenda kuchota maji kama ilivyo desturi yake. Bomba la maji lilikuwa uwani,wapangaji wote pamoja na familia ya bwana Hamisi walishirikiana matumizi ya bomba,na choo pia.

Pale ambapo mpangaji alipokuwa akienda kuchota maji,bwana Hamisi alikuwa akimchungulia dirishani mwake kuona jinsi atakavyoweza kunamsa huyo mama (mpangaji) na mtego wake aliouweka pale bombani. Kumbe Hamisi ! alikuwa ni mchawi mkubwa sana,mwenye kujificha ficha  katika uchawi wake. Alimtupia uchawi mpangaji wake pale bombani,kusudi lake yule mpangaji akanyage uchawi huo ili amnase katika mtego wake .

Basi,mpangaji alipoenda kuchota maji,ni kweli alikanyaga hizo dawa alizoweka Hamis bila kujua, na akaenda zake bafuni kuoga,akaoga na hatimaye akatoka bafuni bila kudhulika na lolote.Sasa. Hapo likatimia lile Neno katika Marko 16:18 lisemalo kwamba watashika nyoka hata wakinywa kitu cha kufisha,hakitawadhuru kabisa… Na ndivyo ilivyotokea kwa mpangaji huyu.

Akaendelea kumsikilizia kuona labda dawa itafanya kazi baadae,lakini wapi! Yule mpangaji wake alipomaliza shughuli zake akatoka akiwa mzima na kurudi baadae jioni akiwa mzima wa afya. Siri kubwa ya huyu mama ilikuwa ni MAOMBI na kupitia maombi Bwana alimlinda- Zab.121:7-8

Hivyo,uchawi wa mwenye nyumba ulidunda na wala haukufanikiwa kwa sababu,huyu ndugu alikuwa ameokoka na ni mwombaji mzuri. Baada ya kuyasikia hayo,nikajifunza kwamba iko haja ya kujifunza juu ya undani wa maombi.

Maombi ni somo lisiloepukika kwa mkristo. Fikiri maisha yanakuaje pasipo maombi? Kilicho bora katika maisha ya mwanadamu ni maombi,ni afadhali mtu akunyime vyote lakini asikunyime muda wa maombi. Maombi ndio kila kitu!Kumbuka ya kwamba;kiu uliyonayo ya kukua kiroho,kiu ya ushindi wa kiroho,kiu ya kumiliki mambo yako mbali mbali,yote hayo yamefichwa katika maombi.  Hivyo,utagundua kwamba maombi yamebeba siri za mambo mengi sana. ”

Madhumuni makubwa ya somo hili la maombi ni kukupa maarifa kamili kuhusu maombi kwa ujumla na kukufundisha namna ya kuomba vizuri. Ili sasa,ubadili ufahamu wako kuhusu maombi. Yakobo 4:1-3,inaeleza juu ya watu ambao wamejisahau kuomba,watu wa namna hii sio kwamba hawana muda wa kuomba,lah! isipokuwa suala la kuomba kwao sio kipaumbele. Lakini pia Yakobo anawataja watu ambao ni waombaji wenye kuomba vibaya. Sasa namna ya kuomba vibaya kukoje? Ni muhimu kujifunza vyema ili na wewe usije ukafanya makosa kama waliyofanya hawa ndugu.

01.MAOMBI NI NINI?

(i) Maombi ni mazungumzo kati ya roho ya mwombaji na Mungu wake katika kushukuru,kusifu na kuabudu,kutubu dhambi pamoja na haja binafsi.

“Maombi” ni agenda ya Mungu mwenyewe,kwa maana ni Yeye ndiye mwasisi wa maombi,tangu bustani ya Edeni hata sasa Mungu  ndiye mwenye kutafuta kuongea nasi kwa maana anajua sisi hatuwezi bila yeye. Ni mfano wa mzazi mwenye kumtafuta mwana akijua kwamba mwana wake hayawezi maisha bila uwepo wake (mzazi). Tangu Adamu katika bustanini,Mungu alikuwa na uhusiano wa karibu na mwanadamu wa kuongea naye (Mwanzo 3:8) 

Lakini tufahamu hili,maombi ni zaidi ya mazungumzo ya kawaida baina ya pande mbili. Tunasema ni mazungumzo yasiyokuwa ya kawaida kwa sababu,mazungumzo haya yapo kiroho kwa maana Bwana Mungu ni Roho lakini pia mwanadamu ni roho. Sasa ikiwa maombi ni mazungumzo ya kiroho,basi ni dhahili kabisa inatakiwa pande zote mbili zinapaswa kuwa rohoni ili kusudi kukamilisha mawasiliano hayo. Ikitokea pande mojawapo itakuwa kiroho na nyingine ikawa kimwili,basi hapo hawataelewana kabisa. Ni sawa na mchina mwenye kuongea kichina awasiliane na mswahili mwenye kuongea kiswahili,hapo ujue hao wawili hawataelewana kabisa kwa maana kila mmoja anaongea lugha yake anayoielewa na tena haelewi mwenzake anasema nini.

Na ndivyo ilivyo Yeye Mungu ni wa rohoni wakati wote,hivyo wewe mwombaji huna budi kuwa rohoni wakati wote ili kukamilisha mawasiliano yenu. Yesu naye aliweza kukamilisha mawasiliano yake na Mungu kwa maana naye alikuwa rohoni wakati wote,tena Yeye mwenyewe anasema“Mimi na Baba tu umoja.” Yoh. 10:30

Maombi sio“omba omba” ni namna ya kusifu ukuu wa uungu wake,na ndio maana neno “maombi limetokana na neno “praise – prayer” . Mwombaji mzuri hatahitaji kuomba atendewe tu,bali wakati mwingi atamsifu Mungu na kuutafakari uweza wake…

ITAENDELEA..

Kwa mawasiliano ya maombi na ushauri,piga +255 683 877 900.

What’s app number +255 746 446 446

Na Mch.Gasper Madumla.

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page